Haya si maandamano ya amani, hizi ni vurugu sasa

Haya yaliyotokea jana kwenye miji ya majimbo mbalimbali si maandamano.

Hayakuwa maandamano ya kudai haki.

Zile zilikuwa ni vurugu.

Sasa kinachobamba kwenye habari si kifo cha George Floyd. Ni hizo vurugu za hao wapumbavu.

Majitu yanaenda yanavunja maduka na kuiba pombe, nguo, masufuria, nepi za watoto, na chochote kile kiwezacho kubebwa!

Jana makao makuu ya CNN nayo yakashambuliwa. Sasa CNN inahusikaje, kwa mfano?

CNN siku hizi imekuwa ya hovyo kabisa. Si ile CNN ya akina Bernard Shaw, Riz Khan, na magwiji wengineo wa tasnia ya habari waliotufanya tuiamini kama chombo cha uhakika cha habari. CNN ya siku hizi imekuwa chombo cha uanaharakati wa kisiasa. Siipendi kabisa CNN.

Lakini, licha ya hivyo, kilichotokea jana kwenye makao makuu yake siwezi kukikubali hata kidogo.

Na heko kwa mapolisi wote walioonyesha ‘restraint’ ya hali ya juu sana, wakiwemo Secret Service police kwenye viunga vya White House.

View attachment 1463527View attachment 1463528View attachment 1463529View attachment 1463530

Siungi mkono wanachofanya Polisi wa Marekani kwa raia weusi

Siungi mkono uharibifu wanaofanya waandamaji kwenye mali za watu

Naunga mkono taharuki hii ichochee mwamko wa watu ikifika mwezi wa November wafanye uamuzi sahihi kwenye box la kura
 
Siungi mkono wanachofanya Polisi wa Marekani kwa raia weusi

Siungi mkono unaharibifu wanaofanya waandamaji kwenye mali za watu

Naunga mkono taharuki hii ichochee mwamko wa watu ikifika mwezi wa November wafanye uamuzi sahihi kwenye box la kura

Kwako uamuzi sahihi ndo upi?
 
Haya yaliyotokea jana kwenye miji ya majimbo mbalimbali si maandamano.

Hayakuwa maandamano ya kudai haki.

Zile zilikuwa ni vurugu.

Sasa kinachobamba kwenye habari si kifo cha George Floyd. Ni hizo vurugu za hao wapumbavu.

Majitu yanaenda yanavunja maduka na kuiba pombe, nguo, masufuria, nepi za watoto, na chochote kile kiwezacho kubebwa!

Jana makao makuu ya CNN nayo yakashambuliwa. Sasa CNN inahusikaje, kwa mfano?

CNN siku hizi imekuwa ya hovyo kabisa. Si ile CNN ya akina Bernard Shaw, Riz Khan, na magwiji wengineo wa tasnia ya habari waliotufanya tuiamini kama chombo cha uhakika cha habari. CNN ya siku hizi imekuwa chombo cha uanaharakati wa kisiasa. Siipendi kabisa CNN.

Lakini, licha ya hivyo, kilichotokea jana kwenye makao makuu yake siwezi kukikubali hata kidogo.

Na heko kwa mapolisi wote walioonyesha ‘restraint’ ya hali ya juu sana, wakiwemo Secret Service police kwenye viunga vya White House.

View attachment 1463527View attachment 1463528View attachment 1463529View attachment 1463530
Siungi mkono mtu kubaguliwa na kuuawa kwa sababu ya rangi yake au sababu nyingine isipokuwa kama ni bahati mbaya au aliyeuawa ilikuwa ni katika hali ya kujilinda. Pia siungi mkono mtu akiuliwa, watu waandamane kwa fujo. Kuandamana kwa amani bila kuharibu mali au kuzuia watumiaji wengine wa barabara naunga mkono kwa lengo la kuonyesha hisia au kupeleka ujumbe kwa watawala wachukue hatua naunga mkono maana mauaji kama haya bila kuyapinga yanakuwa mazoea na mazoea yanakuwa kama sheria (yana shida).
 
💯%!
 
Kama wangewakamata wale Askari watatu immediately baada ya kuwafuta kazi huenda haya yanayotokea leo yasingetokea. I hope the message is loud enough na wahusika wanachukua notes.
 
Kwa maoni yangu, tatizo sio kukamatwa kwa wale askari watatu, kinachotakiwa kufanywa ni KUTOKOMEZWA kabisa tabia ya kibaguzi ya vyombo vya usalama vinapo deal na watu weusi na pale inapo deal na watu weupe

Kuwe na usawa, kila mtu ashugulikiwe kwa haki, pale inapobainika / kuhisiwa kuwa kafanya kosa bila ya kujali rangi yake
 
CNN walinidanganya kipindi cha uchaguzi na Trump akashinda. Walinidanganya mno kilichotokea ni kama RT walivotarajia. Nimekuja kuwajaribu tena walipodai Kim kafa, wao ndo walikuwa wa kwanza kabisa. Nikajizuia nisiwaamini na kweli hakuwa kafa. Nina gundu nao.
 
Haya yaliyotokea jana kwenye miji ya majimbo mbalimbali si maandamano.

Hayakuwa maandamano ya kudai haki.

Zile zilikuwa ni vurugu.

Sasa kinachobamba kwenye habari si kifo cha George Floyd. Ni hizo vurugu za hao wapumbavu.

Majitu yanaenda yanavunja maduka na kuiba pombe, nguo, masufuria, nepi za watoto, na chochote kile kiwezacho kubebwa!

Jana makao makuu ya CNN nayo yakashambuliwa. Sasa CNN inahusikaje, kwa mfano?

CNN siku hizi imekuwa ya hovyo kabisa. Si ile CNN ya akina Bernard Shaw, Riz Khan, na magwiji wengineo wa tasnia ya habari waliotufanya tuiamini kama chombo cha uhakika cha habari. CNN ya siku hizi imekuwa chombo cha uanaharakati wa kisiasa. Siipendi kabisa CNN.

Lakini, licha ya hivyo, kilichotokea jana kwenye makao makuu yake siwezi kukikubali hata kidogo.

Na heko kwa mapolisi wote walioonyesha ‘restraint’ ya hali ya juu sana, wakiwemo Secret Service police kwenye viunga vya White House.

View attachment 1463527View attachment 1463528View attachment 1463529View attachment 1463530
Wewe endelea kukaa ndani!! Wewe si unaishi US kimakosa angalia usije ukakamatwa na kurudishwa kwenu Misungwi tuache sisi tuendelee kuwanyosha hawa mabeberu uchwara!
 
Kwa hiyo unachotaka kusema ni kwamba ukiwa mtu mweusi Marekani, wewe ndo basi tena? Utabaguliwa kila sehemu? Hutapewa haki ya kuishi [nini maana yake?]

Ushawahi kuishi Marekani wewe?
Nachosema ukitoka Afrika kama mtu mzima ukaenda Marekani hutaweza kuelewa ile system inavyo wa affect hao black americans. Nimeona Waafrika wengi wakifanya hilo kosa la kujilinganisha na wao. Hao watu wasingepambana hata hizo haki unazopata sasa usingepata kama Mtu mweusi hapo Marekani una kila sababu ya kuwaheshimu na kuwapa support. Unajua kwanini upo huko lakini unafuatilia mambo ya huku Tanzania? Halafu kujibu swali lako nimeishi miaka miwili na ushee huko, pia nimetembea mabara yote kasoro Antartica na South America. Nimesema hivi uelewe nina angalia hili suala la ubaguzi kwenye lense ya dunia nzima na jinsi mtu mweusi anavyopata shida kwenye dunia kisa rangi yake.
 
Umeishi miaka miwili na ushee tu?

That explains it all...
 
I don't blame them. Hatuwezi kuamulia watu jinsi ya kutoa hasira zao ilhali maandamano ya amani yameonekana kutozaa matunda na watu kila siku wanazidi kuuwawa kinyama mikononi mwa watu walioapa kuwalinda.
 
Atlanta na Minneapolis naona kumechafukwa sasa

Ah wapi!

Leo waandamanaji wana adabu.

Gov. Kemp, Mayor Bottoms, na Police Chief Erica Shields leo hawana utani na mtu.

Wale wajuba wa prison riots wapo tayari kushikisha watu adabu. Na jamaa huwa hawana mchezo.

Ila la muhimu zaidi ni kwamba, watu walio wengi wamekemea ule uhalifu uliofanywa jana usiku. Na kwenye hili la kukemea hakuna mgawanyiko wowote ule katika misingi ya kisiasa. Watu wengi wapo pamoja.

8FA67614-8121-41D4-8782-3EB0552490F2.jpeg
7FE2D094-1FE6-4CFE-AD29-2E52182668FD.jpeg
692F79E6-6DE0-4FE5-9346-874810AFDD9A.jpeg
 
Back
Top Bottom