Haya ni mambo yaliyonisisimua huko Nanjilinji

Haya ni mambo yaliyonisisimua huko Nanjilinji

Mkuu hiki kijj msimu wa pesa huanza mwez wa tano pind wanakjj wanapoanza kukata ufuta na msimu wa pesa huchanganya mwez wa sits katikat hapo pesa huwa nyingi kwan walioweng huwa wamevuna ufuta na kuuza kama unataka pesa kwa wwe mgen wekeza kwenye mavazi nguo za dukan na nguo za akina mama pia vyombo vya ndan bila kusahau viatu vya watoto na watu wazima hapa usiumize kichwa tafuta vile viatu vinavyoitwa yeboyebo hakika utafurahi mwenyewe na kumbuka msimu unaisha mwez wa nane mwishon hapo maisha hurud karka hali ya kawaida na ikifka disemba watu huamia mashamban kumbuka kuna best zakufikia
Pia hata biashara ya Chakula kama kufungua Cafe n.k. Ukienda na kafriji kasola
huko mbona utafurahi!
 
Nikifika huko dondoo muhimu kama hizi zitanisaidia sana.
Vipi minada ya ng'ombe ipo huko ?
Tatizo lenu wafugaji na ndo kitu nakiona maeneo mengi huku kusini
ni Wajeuri hamuheshimu mazao ya watu, waweza kuta sehemu ina
nyasi na majani ya kutosha lakini bado munaingiza mifugo Mashambani!
 
Tatizo lenu wafugaji na ndo kitu nakiona maeneo mengi huku kusini
ni Wajeuri hamuheshimu mazao ya watu, waweza kuta sehemu ina
nyasi na majani ya kutosha lakini bado munaingiza mifugo Mashambani!
Hao ni wafugaji wajinga mfugaji halisi hawezi kufanya upumbavu wa namna hiyo.
Hasa wamasai ambao hawalimi ndiyo hufanya hivyo lakini wasukuma tunalima na kufuga hatuwezi kulisha mashamba ya watu
 
Mkuu umesema kwa laki2 unapata ardhi ya ekari 50 had I 100 he hii ni kwa kukodi ama kununua ama umekosea kuandika mkuu
Mkuu kama ni kununua waweza pata heka 5 mpaka 10 kwa laki moja, hakuna
bei maalumu bei inapungua kadri unavyosogea mbali na kijiji na ili uweze
kumiliki vizuri hilo eneo unatakiwa kupanda mazao ya kawaida angalau miti
miwili mitatu hii inakusaidia kudhibiti, unaweza kupanda minazi au mikorosho
 
Hao ni wafugaji wajinga mfugaji halisi hawezi kufanya upumbavu wa namna hiyo.
Hasa wamasai ambao hawalimi ndiyo hufanya hivyo lakini wasukuma tunalima na kufuga hatuwezi kulisha mashamba ya watu
Kweli mkuu wasukuma wanaishi vizuri na wenyeji kule labda tatizo ninaloliona
kuna wale walioweka makazi kule maporini hawataki kupeleka watoto shule
Kuna kijana mmoja nilikuwa namuhoji pale NAKIU anasema yeye anachunga
halafu baadae anapewa ng'ombe na baba yake nayeye anamiliki mji wake
hakuna habari ya shule tena.
 
Karibu mkuu tutafutane utakapoenda ntakupa ushaur juu ya huku
Mkuu we uko wapi? nataka nikifika nikutafute Nakiu, Nanjilinji, Nambiranje, Mkaranga, Mauswega, Mbuyu wa Rangi, Njete, Mandojo, Naungo, Nandanga au kule kwenye msikiti wa Majini?
 
Mkuu we uko wapi? nataka nikifika nikutafute Nakiu, Nanjilinji, Nambiranje, Mkaranga, Mauswega, Mbuyu wa Rangi, Njete, Mandojo, Naungo, Nandanga au kule kwenye msikiti wa Majini?
Mm n mtumish wa serikali sema kule nimewekeza mkuu hvyo hasa wikend huwa naenda Mara kwa Mara nambiranje naungo n wilaya ya ruangwa hiyo wik hii ntakuwa huko kufanya mavuno na kupeleka mzgo pia wa dukan ukipata nafas ntafute
 
Mkuu kuna Naungo kijijini na kule msituni, huko kijijini sikujui mimi nilikuwa
naingia kwenye ule Msitu ambao inapatikana sana miti ya Mipingo. Ok
Nitakutafuta mkuu.
 
Mkuu kuna Naungo kijijini na kule msituni, huko kijijini sikujui mimi nilikuwa
naingia kwenye ule Msitu ambao inapatikana sana miti ya Mipingo. Ok
Nitakutafuta mkuu.
Ucjar mkuu mm nipo naungo kuna machimbo huko mandojo pia kama ukifuata ile njia inayokwenda ruangwa kifup kama upo serious. Kuna LA kujifunza huko maisha s mjini tu binafs naishi DSM lakin maisha yapo nanjirinji
 
Mkuu kama ni kununua waweza pata heka 5 mpaka 10 kwa laki moja, hakuna
bei maalumu bei inapungua kadri unavyosogea mbali na kijiji na ili uweze
kumiliki vizuri hilo eneo unatakiwa kupanda mazao ya kawaida angalau miti
miwili mitatu hii inakusaidia kudhibiti, unaweza kupanda minazi au mikorosho
Asante sana mkuu nakushukuru kwa maelezo mazuri ngoja nijipange kuzifuata fursa zilipo
 
Ucjar mkuu mm nipo naungo kuna machimbo huko mandojo pia kama ukifuata ile njia inayokwenda ruangwa kifup kama upo serious. Kuna LA kujifunza huko maisha s mjini tu binafs naishi DSM lakin maisha yapo nanjirinji
Vipi ardhi ya huko inasapoti kilimo cha miti ya mbao?
 
Wengi hukitaja Kijiji hiki kwa namna fulani ya Utani, hususani wanapotaka
kuwatania watu wa kusini. Umaarufu wa kijiji hiki kwenye midomo ya watu
ulinifanya nipange safari ya kutembelea huko mwaka 2015.

1.Ni kijiji ambacho kina fursa kubwa sana za kiuchumi kiasi kwamba nimekuta makabila tofauti huko kama Wahehe, wasukuma, Wamasai n.k (Wasukuma niliwakuta wakiwa wengi sana na wamejenga ngome zao jirani na kijiji hicho katika kijiji kidogo cha NAKIU huko wanalima mpunga na kufuga
wanyama kama ng'ombe na mbuzi)

2. Ni eneo ambalo ufuta hustawi kwa wingi sana na pia hakuna ugumu wa upatikanaji wa ardhi, kwa pesa ndogo unapata eneo kubwa la ardhi. Kwa laki 2 unaweza kujikuta unapata mpaka ekari 50 au 100 kutegemea na umbali wa hapo lilipo shamba mpaka kijijini.

3. Kuna baadhi ya maeneo yana madini, eneo kama Mandojo ambako dhahabu hupatikana huko lakini wachimbaji wake wengi huchimba
kienyeji sana, sina uhakika kama mpaka leo bado wanachimba.

4. Kijiji hukusanya mapato makubwa sana kiasi kwamba mwanafunzi anapoanza darasa la kwanza gharama zote za maandalizi pesa hutolewa na kijiji'

5.Mwanamke mjamzito hupewa pesa na kijiji anapoanza kliniki.

NB. Nilifanya kazi ndogo tu kwa wiki 3 nikaingiza kiasi cha 3,700,000.

Ifahamike kuwa wakati wa mvua maisha ya huko ni magumu sana.

Mengine wataongezea wadau.
Wasukuma sio watu wa kisport sport popote wafikapo lazima wenyeji wajue kutumia ardhi, ukiachilia kazikazini pande zingine zote za tanzania wametapakaa na wanavitongoji vyao kabisaa na wanajua kuishi vizuri na wenyeji kinachowashinda kwenda kazikazini ni ubinafsi wa watuwa kule.pia msukuma na jamii ya kimasai ni mashariki na magaharibi.
In morogoro voice!
 
Wadau mliouliza maswali nitakuja kuwajibu simu yangu imeisha chaji, hapa natumia hii ya 2g inasumbua.
Ila hukuwahi kûishi Nanjililinji. Acha usanii Mwenyewe unajua unachokifanya hapa jukwaani
 
Back
Top Bottom