Roman Israel Esq
JF-Expert Member
- Nov 23, 2017
- 2,024
- 3,283
Nani kakudanganya?Ukiona watu hawataki kulima jua maisha ni rahisi
Nani kakudanganya?Ukiona watu hawataki kulima jua maisha ni rahisi
Ni kweli ameisaidia sana kata ile hasa barabara kituo cha afya alikuwa na lundo LA vyeo diwan mwenyekit halmashaur kilwa mwenyekit ccm Lindi mwenyekiti wa wenyeviti ccm taifa kwa ambao walikuwa hawamfahamu ndio alikuwa rafk wa kingunge ngombare mwiru kwenye msiba wake alipewa nafas ya kuongea neno kama mzee wa familia RIP ALLY MOHAMED MTOPARIP mzee mtopa Diwani wa Muda mrefu wa nanjilinji kama ukiweza kuweka misingi ya kuwalipia wanafunzi na wakina mama wanapo jifungua
Shoga me nshatangulia,fanya hima ukuje nawwShoga twende nanjilinji tukalime mpunga naona kuna fursa huko
Nshatangulia mie,Fanya uje na Ww shosti anguNaomba twende
Hahahahaha! HayaaaaaaaShoga me nshatangulia,fanya hima ukuje naww
Mbona umefurahi hivyoo...lolHahahahaha! Hayaaaaaaa
Nawangoja nanjilinjiiMbona umefurahi hivyoo...lol
[emoji4][emoji28]Nawangoja nanjilinjii
Nshatangulia mie,Fanya uje na Ww shosti angu
Karibu mamiiNakuja maa
Wadau mliouliza maswali nitakuja kuwajibu simu yangu imeisha chaji, hapa natumia hii ya 2g inasumbua.
Nimekiangalia kijiji hicho kwenye google sijakiona bali nimeeishia kujua kuwa kipo Kilwa, ukiona msukuma kahamia huko basi jua kuna malisho ya ng'ombe, pana sehemu ya kulima na ni pazuri kupata mke wa bei chee
Wahini mapema mpige Pesa Jamaa kakaa wiki Tatu kaokota milioni Tatu, muwahi msimu wa ufuta,ukiisha mnangojea tena msimu wa korosho kusini kucheleeeh!!!!Nshatangulia mie,Fanya uje na Ww shosti angu
Kucheleeeh!!!!Wahini mapema mpige Pesa Jamaa kakaa wiki Tatu kaokota milioni Tatu, muwahi msimu wa ufuta,ukiisha mnangojea tena msimu wa korosho kusini kucheleeeh!!!!
Ishu ya dhahabu ni kila sehemu Tz hii shida ni vyombo vya uchimbaji.Na pia pana dhahabu.
Mkuu, kuna vitu hatutakiwa kukatishana tamaa mtu anapotoa mada kamaTumeshakuchangia tayari hiyo charge, je umerudi hewani utudanganye tena?
Mkuu, utasababisha Nanjilinji kujaa Yeboyebo mwaka huu.Mkuu hiki kijj msimu wa pesa huanza mwez wa tano pind wanakjj wanapoanza kukata ufuta na msimu wa pesa huchanganya mwez wa sits katikat hapo pesa huwa nyingi kwan walioweng huwa wamevuna ufuta na kuuza kama unataka pesa kwa wwe mgen wekeza kwenye mavazi nguo za dukan na nguo za akina mama pia vyombo vya ndan bila kusahau viatu vya watoto na watu wazima hapa usiumize kichwa tafuta vile viatu vinavyoitwa yeboyebo hakika utafurahi mwenyewe na kumbuka msimu unaisha mwez wa nane mwishon hapo maisha hurud karka hali ya kawaida na ikifka disemba watu huamia mashamban kumbuka kuna best zakufikia
Umesahau pia ni kijiji cha tatu kwa ubora ulimwenguni.Wengi hukitaja Kijiji hiki kwa namna fulani ya Utani, hususani wanapotaka
kuwatania watu wa kusini. Umaarufu wa kijiji hiki kwenye midomo ya watu
ulinifanya nipange safari ya kutembelea huko mwaka 2015.
1.Ni kijiji ambacho kina fursa kubwa sana za kiuchumi kiasi kwamba nimekuta makabila tofauti huko kama Wahehe, wasukuma, Wamasai n.k (Wasukuma niliwakuta wakiwa wengi sana na wamejenga ngome zao jirani na kijiji hicho katika kijiji kidogo cha NAKIU huko wanalima mpunga na kufuga
wanyama kama ng'ombe na mbuzi)
2. Ni eneo ambalo ufuta hustawi kwa wingi sana na pia hakuna ugumu wa upatikanaji wa ardhi, kwa pesa ndogo unapata eneo kubwa la ardhi. Kwa laki 2 unaweza kujikuta unapata mpaka ekari 50 au 100 kutegemea na umbali wa hapo lilipo shamba mpaka kijijini.
3. Kuna baadhi ya maeneo yana madini, eneo kama Mandojo ambako dhahabu hupatikana huko lakini wachimbaji wake wengi huchimba
kienyeji sana, sina uhakika kama mpaka leo bado wanachimba.
4. Kijiji hukusanya mapato makubwa sana kiasi kwamba mwanafunzi anapoanza darasa la kwanza gharama zote za maandalizi pesa hutolewa na kijiji'
5.Mwanamke mjamzito hupewa pesa na kijiji anapoanza kliniki.
NB. Nilifanya kazi ndogo tu kwa wiki 3 nikaingiza kiasi cha 3,700,000.
Ifahamike kuwa wakati wa mvua maisha ya huko ni magumu sana.
Mengine wataongezea wadau.