GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,773
Wengi hukitaja Kijiji hiki kwa namna fulani ya Utani, hususani wanapotaka
kuwatania watu wa kusini. Umaarufu wa kijiji hiki kwenye midomo ya watu
ulinifanya nipange safari ya kutembelea huko mwaka 2015.
1.Ni kijiji ambacho kina fursa kubwa sana za kiuchumi kiasi kwamba nimekuta makabila tofauti huko kama Wahehe, wasukuma, Wamasai n.k (Wasukuma niliwakuta wakiwa wengi sana na wamejenga ngome zao jirani na kijiji hicho katika kijiji kidogo cha NAKIU huko wanalima mpunga na kufuga
wanyama kama ng'ombe na mbuzi)
2. Ni eneo ambalo ufuta hustawi kwa wingi sana na pia hakuna ugumu wa upatikanaji wa ardhi, kwa pesa ndogo unapata eneo kubwa la ardhi. Kwa laki 2 unaweza kujikuta unapata mpaka ekari 50 au 100 kutegemea na umbali wa hapo lilipo shamba mpaka kijijini.
3. Kuna baadhi ya maeneo yana madini, eneo kama Mandojo ambako dhahabu hupatikana huko lakini wachimbaji wake wengi huchimba
kienyeji sana, sina uhakika kama mpaka leo bado wanachimba.
4. Kijiji hukusanya mapato makubwa sana kiasi kwamba mwanafunzi anapoanza darasa la kwanza gharama zote za maandalizi pesa hutolewa na kijiji'
5.Mwanamke mjamzito hupewa pesa na kijiji anapoanza kliniki.
NB. Nilifanya kazi ndogo tu kwa wiki 3 nikaingiza kiasi cha 3,700,000.
Ifahamike kuwa wakati wa mvua maisha ya huko ni magumu sana.
Mengine wataongezea wadau.