Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Haya ndiyo maoni ya gazeti letu 'TUKUFU' la Rai
Ufisadi usitufumbe Macho
katika kipindi cha takribani miezi minne hivi,hapa nchini yametoke mambo ya kusikitisha.
Tumeshuhudia baadhi ya viongozi wetu wa serikali wakijiuzulu nyadhifa zao kutokana na tuhuma za ufujaji wa fedha za umma. Sababu kuu zinazoelezwa za kujiuzulu kwa viongozi hao,ni matumizi mabaya ya nyadhifa zao. Hali hiyo imesababisha baadhi ya yao kujikuta wakidaiwa kutumbukia katika mitego ya rushwa hali inayosababishwa na tamaa ya kujilimbikizia mali.
kutokana na misingi ya utawala bora,iliyoimarishwa zaidi katika serikali ya awamu ya nne,viongozi wote waliohusishwa na kashifa za ubadhirifu wa fedha za umma ,bila kujali iwapo wamehusika au la,wamewajibika kisiasa. Hilo ni jambo jema kwa taifa letu.
Ingawa viongozi hao wamejiuzulu kwa ridhaa yao kama hatua ya kutimiza misingi ya demokrasia na utawala bora,tungependa kuona hatua moja mbele zaidi. Hatua hii ni kuwachunguza na kubaini nani anahusika vipi.Tunapenda sheria ichukue mkondo wake,ambapo wote watakaobainika kuhusika watatiwa hatiani na kutumikia adhabu zao kwa mujibu wa sheria.
Hatuwezi kuhukumu,ila tunayo maswali ya kuuliza. Tunajiuliza iwapo waliojiuzulu kweli walihusika na hayo waliyotuhumiwa nayo,je, taifa hili lina viongozi wa aina gani? viongozi wetu wanajenga picha gani kwa Rais Jakaya Kikwete aliyewateua?
Pia kuna jambo la kusikitisha. Kwa sasa katika mfumo wea siasa za vingi ni rahisi kukinyooshea kidole chama tawala,CCM.Ni rahisi zaidi kuinyooshea serikali iliyopo madarakani . Ni rahisi mno kusema kwamba serikali haitekelezi wajibu wake ipasavyo.
Hili si jambo la kheri. Ni hatari kwani hali inavyoelekea taifa hili linakaribia kutumbukia katika mtego. Kwamba tumeacha mkondo wa kuzungumzia maendeleo, tumejikita katika ufisadi.
Ingawa wahenga walisema kuwa samaki mmoja akioza wote wameoza, si lazima usemi huu uwe sahihi kwa hili la mafisadi. Ukweli unabaki kuwa wapo viongozi wengine wanaotambua wajibu wao na wenye uchungu na nchi yao. Tusiwachafue hawa kwa uozo wa wenzao. Tusiwachafue kwa tope la ufisadi.
Kama taifa tunahitaji tafsiri mpya ya neno ufisadi. Ufisadi umekuwa msamiati maarufu kweli katika taifa hili, na kila kona kuna msukumo(pressure) wa kuaminisha jamii kuwa kwa sasa kila mwanasiasa ni fisadi.
tumejiingiza katika mijadala isiyotoa majibu kwa matatizo yanayotukabili. Ni vyema sasa tuanze kubainisha njia nzuri za kukuza uchumi wa taifa hili. Serikali nayo ifike mahali ijue kuwa hakuna uhuru usio na mipaka. Kuwaachia watu wakaendelea na mjadala wa ufisadi huku wakipotosha ajenda ya maendeleo hakulisaidii taifa hili.
Kwamba serikali nayo sasa inaelekea kutumia muda wake mwingi kujadili ufisadi,badala ya kutueleza jinsi ya kujenga visima vya maji,barabara.zahanati,shule za sekondari na bila kusahau madawati katika shule za msingi,ni hatari pia.wakati umefika sasa tubadilike, au tutabadilishwa na upepo tusioujua si muda mrefu.
tunapaswa kutambua kuwa tumebakiza muda kidogo kabla ya serikali ya awamu ya nne kumaliza kipindi cha kwanza cha miaka mitano. Katika kipindi hiki tunapaswa kurejea katika ilani ya uchaguzi na kujiuliza serikali iliahidi nini na mpaka sasa imetekeleza nini. Huu utakuwa mjadala sahihi kwa ustawi wa taifa hili.
kutonakana na hali hiyo,watanzania tunapaswa kufumbua macho na kuangalia mbele kuhusu matatizo mengine ya kijamii. Ufisadi ni tatizo mojawapo ndiyo,tunasema usifumbiwe macho,ila usitupofushe katika matatizo mengine. Kama tupo kwenye mapambano ya kweli dhidi ya matatizo yanayolikabili taifa letu ni wazi mkakati wa sasa wa ufisadi hatufikishi tutakako. Mungu Ibariki Tanzania.