Haya ndiyo malambo makubwa zaidi ya kuzalisha umeme katika Afrika

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,238
12,751
Hii ni orodha ya malambo kumi makubwa katika Afrika kwa kuangalia kiasi cha umeme yanachozalisha:

1. The Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) – 6,450 MW -Ethiopia
2. Aswan High Dam – 2,100 MW-Misri
3. Cahora Basa Dam – 2,070 MW-Msumbiji
4. Gilgel Gibe III Dam – 1,870 MW-Ethiopia
5. Inga Dams – 1,775 MW-DRC
6. The Kariba Dam – 1,626 MW-Zimbabwe/Zambia
7. Merowe Dam – 1,250 MW-Sudan
8. Tekezé Dam – 1,200 MW-Ethiopia
9. Akosombo Dam – 1,020 MW-Ghana
10. Kainji Dam – 760 MW-Nigeria
 
Ethiopia wana Megawatts kama 10,000 hivi. Sisi nafikiri hata Stigler gorge ikiisha hatupiti 3000MW.

Baada ya miaka kumi tunakuwa na upungufu tena wa umeme. Ukizingatia vitu vingi vitakuwa vinatumia umeme, SGR, magari, Viwanda vikubwa, watu wanaongezeka nk.
 
Hili suala la kujenga malambo ya kuzalisha umeme linatakiwa kuwa endelevu. Bado tuna potential kubwa sana ya umeme wa maji.
 
yaliyotajwa hapo ni sababu inasaidiwa na mito mikubwa isiyoweza kufa wala kupungua kiasi cha maji.mfano ziwa victoria likipeka maji yake nile pale uganda jinja uwezi kusikia umeme unakasheshe kama january makamba
 
Hivi The Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) limeanza kuzalisha umeme?. Au Mimi ndio kingereza Cha Al Jazeera kinanipiga chenga.
 
Hili suala la kujenga malambo ya kuzalisha umeme linatakiwa kuwa endelevu. Bado tuna potential kubwa sana ya umeme wa maji.

Upo sahihi, tuwe na mipango ya miaka 20, 50, 100. Mwekezaji anataka kujenga kiwanda Afrika cha kutengeneza viatu kutumia ngozi, au kusindikiza matunda, cement, kutengeneza magari, simu, laptop.

Anapanga mipango ya miaka 30. Akiangalia mazingira umeme, maji, government policies, rushwa. Atachagua wapi?
 
Hili bwawa la Nyerere ni bwawa la maono,nchi ilifikia mahali ni lazima iwe na bwawa kama lile,kinyume cha hapo hali ingekuwa mbaya sana,hata hivyo hatuko pabaya 2500 MW ni nyingi sana...
Ni nyingi sana ukiwa na mawazo finyu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom