Haya ndio ya kuzingatia katika akaunti zako za mitandao ya kijamii

Nov 2, 2020
68
90
Wakuu Habari,

Nimeona nikushirikishe wewe kijana mwenzangu ambae bado uko Chuo, Mtaani au tayari kwenye suala la Ajira.

Ni muhimu kuzingatia ni kwa njia gani unaishirikisha jamii ili tu uweze kutoka sehemu moja kwenda nyingine kimaisha.

Mfano mzuri, kama unatafuta kazi kwa njia ya kutuma maombi sehemu tofauti, Kumbuka kujichunguza pia kupitia mitandao yako ya kijamii.

Hapa namaanisha unachopost kila siku kina nafasi na maamuzi ya kwa nini UAJIRIWE au USIAJIRIWE sehemu fulani.

Kuna baadhi ya waajiri hawana haja ya kusumbuka kutafuta wadhamini wako wathibitishe tabia ulionayo, ila wanaenda moja kwa moja kwenda account zako na kuangalia nini unapost au unapenda sana kuishirikisha jamii.

Wengine account zao ndio sehemu ya kujimwaga na viguo vya ajabu, matanuzi na bata za kutosha au ndio sehemu ya kupost vichekesho mwanzo mwisho kama ndio kazi zao.

Simaanishi usipost, ila tumia mitandao yako kuwa sehemu ya kuwafundisha wengine juu ya nini wanaweza fanya kutumia lugha nyepesi isiyo ya kitaalam.

Kile unachokijua jamii inakihitajia, inategemea na kwa vipi unaipa kipaumbele na mfano wa hayo.
 
MOSI

Social Network mbalimbali mfano nzuri FACEBOOK ni Social Network tuliyokuwa nayo kutokea inaanza mpaka leo ni Real Profile of life, most rafiki zangu wamejiunga miaka ya 2011 so kwa mantiki yako kutooea mwaka 2011 mpaka leo mtu anajibana cha kuposti eti kisa miaka 15, 20 mbele muajiri mbele atakuja kuangalia PROFILE yake.

Upumbavu na utumwa wa kiwango ambacho sijapata kuona.

Kufunga jela maisha yako yote kisa ajira ajira ya kijinga na namna hii sihiitaji.

PILI
Hiko ulichosema ni tone la maji katika bahari inabidi uombe ajira 1000,0000 Duniani ndio upate 1 ambayo Boss atafanya ujinga huo.
 
Back
Top Bottom