Haya ndio nitakayoyafanya 2024 afe kipa afe beki, wewe je?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Nilichogundua ni kwamba kwa hii kazi niliyonayo nisipowaza nje ya box nitakua msindikizaji tu na kushuhudia watu wakipiga hatua huku Mimi umri unaenda, kwa trending jinsi ilivyo historia ya maisha yangu itakua ni kumiliki nyumba wakati huo msoto wa utumishi ukiwa ni mgumu kwa kutokufanya vitu ninavyotaka kwa kukosa pesa.
kwa miaka miwili Sasa ndani ya game sioni chochote Cha kujivunia saana zaidi ya watu kukuchukulia poa tu, namaanisha hakuna mtu ambaye anaweza "kupay" attention kwako kama huna pesa Sasa huu mwaka naingia na mambo yafuatayo.

Nitajitahidi nikae na watu waliopiga hatua hata kidogo, nimekaa na watu walewale kwa miaka miwili sijaona jambo lolote jipya zaidi ya majungu na kupotezeana muda tu, nitajitahidi nijiassociate na watu waliopiga hatua kidogo naweza kupata a,bc za jambo flani ambalo litakua msaada kwangu najua itakua ni ngumu kwa sababu wengi waliopiga hatua ni wagumu kutoa mafanikio yao.

Nitakua mpole zaidi na nitajitahidi niwe na tabia kama za mtoto mdogo, nimekua mtu wa hasira, short temperd, visasi mwaka huu hata mtu akinitemea mate usoni nitatabasamu sitaki ugomvi na watu nitapunguza na kuondoa ukorofi kabisa,nitaacha kulalamika kabisa nataka niwe mtu wa furaha siku zote.

Nitawekeza kwenye elimu zaidi juu ya jambo ninalotaka kufanya, kukosa elimu au kua na elimu ndogo juu ya mradi/biashara inachangia Sana kwa watumishi au mtu yoyote yule mitaji yao kuanguka, kwahiyo nitajipa miezi 3/6/9 kuchunguza jambo ninalotaka kufanya nipate elimu vizuri nizisome changamoto zake ili pesa zisipotee.

Nitaongeza ujuzi mwingine kabisa nje ya kazi yangu, either mambo ya IT(graphics design n.k) Mwaka huu nimeweza kumaster Excell kwa kiasi chake upande wa data entry, kutengeneza mifumo mbali mbali ya matokeo, student report n.k kwahiyo mwakani naweza kujikita kwenye ufundi magari, fundi aluminium, fundi umeme, uchomeleaji n.k nitajitajidi nichague jambo ambalo litanisaidia siku nikiamua kufanya nakua na ujuzi wa jambo husika.

Mwisho nitaenda bank kuchukua hela zote, sitojenga maana nimeona watu wengi wakikopa na kujenga na kujikuta wanaishi maisha magumu kupita maelezo, nitakopa then niwekeze kwenye jambo langu ninalolipenda la biashara ya mazao, nafukuzia mikopo ya hazina jambo ukiritimba ni mwingi Sana huku halmashauri lakini hata nisipopata lazima nikakombe Hela zote huko NMB.

NOTE: Kwa wafanyabiashara wa nafaka wakubwa mwakani naomba mnichangie maana mwakani lazima nitafanya biashara ya nafaka kwa ukubwa wake, nitajikita kwenye karanga, ufuta, mtama, mahindi, Mchele n.k kwahiyo nitarudi hapa kutafuta masoko zaidi.

Hivyo ndivyo nitaingia 2024.
 
Hii mipango mizuri Sana , kujenga nyumba inapendeza uwe na cash flow ,hela inayozunguka . baadae ndo unajenga.

Yeah kazini wengi naona wanachukua mikopo na kujenga nyumba inafika nusu anasubiri miaka mingine 6 mkopo uishe akope Tena, wakati akisubiri mkopo uishe msoto anaopitia ni mkubwa sana , Sasa Mimi sitaki hiyo
 
Kama utaweza au Una ndugu yako mwenye pesa mwambie akupe mil 5 bila riba then uwekeze , biashara ikianza kutoa returning unamrudishia.

Biashara ya nafaka ukilisoma vizuri unapiga hela maana ndo biashara nafanya sasahivi hapa DSM.
 
Hapo kwa ndugu ndio uongo Sasa, ningependa nikuulize mambo matatu ikiwezakena nitakutafuta zaidi DM, Una sehemu unauza? Au unakusanya shambani then unawapelekea hao wafanyabiashara hapo dsm
 
Mimi ni middle broker

Nawasiliana na mfanyabiashara nasikiliza bei Yake then nawasiliana na mkulima nasikiliza bei Yake.

Hivyo unachotakiwa Kuwa nacho ni information tu. Namba za wakulima na namba za wafanyabiashara hivyo ukifanya haukai na mzigo unanunua na kuuza MTU Kati.

Wakulima watz hawa wadogo wapo broke Sana hivyo faida unapata kwa style hiyo maana akili zao ndo hizo wanauza mazao ili wajenge nyumba na kuoa plus watoto kibao.

Pia hakikisha Una nidhamu ya PESA sana
 
Kuhusu nidhamu ilo naliweza kwa 100% wakati ukifika nitakucheck kwa speed ya 5g.
 
Yeah kazini wengi naona wanachukua mikopo na kujenga nyumba inafika nusu anasubiri miaka mingine 6 mkopo uishe akope Tena, wakati akisubiri mkopo uishe msoto anaopitia ni mkubwa sana , Sasa Mimi sitaki hiyo
Akili za watanzania wengi zinafanana ndio maana kupata atakayeleta mapinduzi sio rahisi ...Huo ndio mtindo kila mtu kuchukua mkopo kwenda kujenga huku miaka sita yote akiishi kwa kukopa kwa watu wengine.

Kama unaweza chukua mkopo then secure kiwanja ,nyingine kafanye mishe zao kama akili yako inavyokutuma.
 
Basi utaendelea kuteseka, tulitegemea jambo la kwanza ni utafanya vp kutanua kipato chako?? Jambo la pili ungezungumzia saving, utatunza vp kila shiling unayo ipata. Poverty mind ni kitu kibaya sana.
 
Mkuu kwa mwaka huu mmoja nimesave million 2 upande wa saving Niko vizuri lakini saving bila ya kuongeza kipato ni zero, maana kwa salary yangu nachezea kwenye negative.
 
Back
Top Bottom