Haya matukio ya mauaji ya wanawake ndani ya wiki moja tunaenda wapi wee mapenzi?

Haya matukio ya mauaji ya wanawake ndani ya wiki moja tunaenda wapi wee mapenzi?

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,085
Reaction score
38,460
Mwanasheria Keneth Nkiko (28) anatuhumiwa kumuua Magreth Richard (22), mfanyabiashara na mkazi wa Manispaa ya Musoma. Uchunguzi wa awali kutoka Jeshi la Polisi, umebaini chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mpenzi wake huyo kuwa na mahusiano na wanaume wengine.


Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Laurent Kweka anatuhumiwa kumuua Mkewe, aliyefahamika kwa jina la Jenipher, kwa kumpiga risasi nyumbani kwao Bunju A, Mtaa wa Mkoani, Zone ya Senzele, Dar es salaam.

Tukio la kusikitisha limetokea Mzambarauni Gongo La Mboto, Dar es Salaam. Kijana aliyefahamika kwa Jina La Dickson Leonard Msigwa anadaiwa kumchoma visu mpenzi wake hadi kupelekea kifo chake.

NB: Matukio yote 3 yameripotiwa ndani ya wiki moja. Tuzungumze uhalisia ili kuinusuru jamii, Tatizo lipo wapi..?
 
Mkiona kuna wanaume wanaishi bila mke mjue hawataki shida/hawataki msongo wa mawazo kuishi na wanawake wakorofi wasio na adabu na waume zao. Wanaume waoe tu ila wakiona kuna viashiria vya hatari ndani ya ndoa ni bora wasepe kimya kimya kujinusuru wasije wakaua wakaishia pabaya. Acha hata jumba kwa usalama wako ndoa isiwe taabu
 
Wanawake wamekuwa hawana heshima na ndoa zao, huingia ndoani kimaslahi kuchuma mali huku wakiendelea kuzisaliti ndoa zao. Wanaume hawako tayari kusalitiwa, ukioa labda ufahamu tu kuwa umeoa tapeli fulani tu kuja kukuchuna, ujue umeoa malaya fulani hivi wa kuja kukusaliti pengine wivu utapungua utamchukulia poa hata akisepa roho haiumi
 
Mkiona single mother wanazidi msishangae, kuna wanaume wamewatema wanawake hao, hawataki stress
 
Mbona wengi ni Wagalatia ,,, tamko la MKE na MUME mmoja inawezekana likawa linachangia kwa kiasi fulani hisia za umiliki uliopitiliza,,,
 
Mbona wengi ni Wagalatia ,,, tamko la MKE na MUME mmoja inawezekana likawa linachangia kwa kiasi fulani hisia za umiliki uliopitiliza,,,
Huu ndio ukweli ambao wanaukimbia na ingekuwa upande ule ungeona chuki za kidini zilivyojuu ya upeo wa akili,

Suala la mwili mmoja ni tatizo katika maisha, mwanamke akifahamu kuwa akileta ujuaji unaoa wa pili na watatu lazima atulize akili.
 
Suluhisho Ni kutopenda kupita Kiasi hakuna kingine,mpende mtu kawaida,kuna mtu ananapenda Hadi kero 😂
 
Back
Top Bottom