Haya maisha bhana!!

Haya maisha bhana!!

Wahenga walisema kua uyaone na kweli nimeyaona natamani hata nisingekuwepo duniani. Nimepiga kitabu kwa bidii diploma G.P.A ya 4 degree 4.0 na sioni muelekeo wowote.

Wakuu kitaa ni kugumu natamani hata niyeyuke nilisoma accounting and finance na sioni ikininufaisha kwa chochote, nawaza kwanini nilizaliwa
Mkuu usikate tamaa, kusoma ni kuelimika..ukielimika unajua cha kufanya.
Usikariri lazima uajiriwe.. .
Fungua macho..........
 
Pole mkuu,
Mimi ni kati ya watu waliomaliza chuo wakiwa na gpa ndogo kweli. Nlisoma kozi siipendi kwa shinikizo la mzee plus nikafika chuo nikawa na mambo mengi. Sup za kutosha kila semister na course ilikuwa ngumu kweli watu kibao waka disco nashangaa hata nlitoboaje miaka 3.
Sasa kwakuwa nilijua gpa yangu ni ndogo sana nlijua siwezi compete na wenye ma gpa yao.
Niliamua kutafta njia zangu na kufanya vitu vingine. Luckily baada ya hapo nimewahi kuajiriwa sehemu 3 na kote huko sikuwahi kuulizwa cheti maana bali tu watu wananiajiri kwa experience au reference.
So, mkuu usikate tamaa maisha ni kupambana mlango huu ukizingua unacheki hata dirisha kama unaweza kupenya
Dit bila shaka 😀
 
Kwani umemaliza chuo lini?


Maisha sio rahisi tena wa kiume pambana maana wa kike hafiki mwaka kashapata bwana mweny pesa anaolewa ,yale maisha magumu bye bye!!

Maisha sio rahisi ila ukipata mwanga tu utatusua na utaona umuhimu wa elimu ,mapema mno kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom