Hawa Wabunge wasio na chama wapo Bungeni kwa sheria ipi? Nani anawalipa?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
WABUNGE WALIOJIPELEKA BUNGENI NANI ANAWALIPA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Jana baada ya Mchango wa Mhe Halima Mdee Bungeni ambao binafsi niliupenda sana kutokana na umahili wake wa kujenga hoja, baadae alisimama Mhe Kunambi na Mhe Jerry Silaa ambao ni Wabunge wa CCM kujaribu kupinga hoja zake.

Mhe Silaa akiwa anaenda kuhitimisha hoja yake alisema kuna Wabunge wapo Bungeni hata vyama vyao vinawakana. Hapa ndipo nitajenga msingi wa hoja yangu.

Turudi kidogo nyuma kwa maana ya misingi ya kisheria inayoongozwa na sheria Mama ambayo ni Katiba ya JMT. Kwa mjibu wa Ibara ya 66(1) imetaja aina ya Wabunge watakao paswa kuwepo Bungeni kuwa ni watano. Lakini mgogoro uliupo sasa ni Wabunge wanaotajwa katika Ibara ya 66(1)(b) Wabunge wanawake.

Mwanzoni baada ya majina yale kuapishwa tuliambiwa yameletwa na CHADEMA. Hata CHADEMA walipokataa kuwa hatujaleta Spika na Tume ya Uchaguzi walisema yametoka CHADEMA.

Ibara ya 67(1) inazungumzia juu ya sifa anazopaswa kuwa nazo mtu anayeitwa Mbunge. Sifa moja wapo kati ya sifa hizo kuu tatu ni sifa inayotajwa katika Ibara ya 67(1)(b) inasema lazima AWE MWANACHAMA wa Chama cha Siasa.

Sambamba na hoja hizo, Ibara ya 78 bado inazungumzia Wabunge wa Viti maalum ambao ndio msingi wa hoja yangu hapo chini. Ibara ya 78(1) inazungumzia namna vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi vitakavyo pendekeza majina kwa Tume ya Uchaguzi. Lakini pia Ibara hiyo hiyo ya 78(4) inayotanguliwa na Ibara ndogo ya (3) inasema "Orodha ya majina ya wagombea wanawake iliyowasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi na kila Chama kwa ajili ya Uchaguzi mkuu ndiyo itakayotumiwa na Tume ya Uchaguzi baada ya KUSHAURIANA NA CHAMA KINACHOHUSIKA.....

Baada ya kunukuu Ibara ya 66, 67 na 78 ninaomba kuuliza Tume ya Uchaguzi na Ofisi ya Spika Mhe Job Yustin Ndugai. Kwa nini jana wakati Mhe Silaa anawakashifu Wabunge kuwa vyama vyao vinawakaa hukuwatetea? Je ni sheria ipi inayoruhusu mtu kuwa Mbunge bila kuwa na Chama cha Siasa? Je, Silaa ni mwongo, mzushi na mfitini na hali ya kukataliwa siyo kweli? Kama ni kweli wamekataliwa,je kwa mjibu wa Ibara ya 78(4) inayosema Chama cha Siasa kitashauriana na Tume, je Tume ilishauriana na Viongozi wa CHADEMA? Je, kama tume haikushauriana na CHADEMA walitumia sheria ipi kuwafanya watu wasio na Chama kuwa Wabunge?

Wapo wanaojaribu kutumia precedent ya Zitto kama case study ya hawa Wabunge wanaosemekana hawana Chama kilichowadhamini, ukweli ni kuwa kesi ya Mhe Zitto Zuber Kabwe ilikuwa mahakamani na ndio maana kulitokea hiyo injuction. Je hawa wamefungua kesi mahakamani?

Sheria hizi zilitungwa na Bunge, je kama mliotunga sheria mnashindwa kuziheshimu vipi kwa ambao si washiriki wa kutunga hizo sheria. Ninadhani ni muda mwafaka kujitokeza hadharani watu wa Tume ili kuweka uhalali wa hawa watu kuendelea kuitwa Wabunge. Kinyume na hapo Wabunge wako wataendelea kudhalilishana kuitana majina ya hovyo. Lakini hata sisi walipa kodi tunataka kujua kama kodi zetu zinawalipa Wabunge halali au Wabunge wa kutengenezwa.

Ahasante.
 
Hawa wabunge wa ushirika haramu wa "Mwendazake na Job". Jambo nililo na uhakika nalo ni kwamba Job alilewa madaraka na hakutegemea kama Mwendazake anaweza akaondoka na kumuachia "msala huu" ambao natumai kwa sasa kila siku akiamka asubuhi jambo hili linamuumiza saana akili yake kwani limemuwekea doa moja baya saana katika uongozi wake wa bunge kwani haijawahi kutokea na haitokaa itokee tena kuwa na wabunge wasio kuwa na chama au kuteuliwa na Rais.
 
Hivi hakuna sheria inayoweza kuwabana wote waliotufanyia huu ujinga wa kulichafua bunge?
Tulifanya dua kubwa tarehe 27/10/2020 wakati tunahitimisha kampeni,tulimuomba Mungu asiwaache salama wooooote walioshiriki kuvuruga mchakato wa uchaguzi na kuiba kura,kwa hiyo Mungu yupo kazini.
 
Hawa wabunge wa Mwendazake na Job.Kitu nilichona uhakika nacho kwamba JoB alilewa madarka na hakutegemea kama Mwendazake anaweza akaaondoka na kumuachia msala huu ambao natumai kila siku akiamka asubuhi hili jambo linamuumiza saana kwani limemuwekea doa moja kubwa saana katika uongozi wake wa bunge kwani haijawahi kutyokea na haitokaa itokee tena kuwa na wabunge wasio kuwa na chama au kuteuliwa na Rais.
Hivi kwamfano rais wa sasa anaweza kumuamuri spika kuwaondoa hao wabunge kwa kukosa sifa?
 
Tulifanya dua kubwa tarehe 27/10/2020 wakati tunahitimisha kampeni,tulimuomba Mungu asiwaache salama wooooote walioshiriki kuvuruga mchakato wa uchaguzi na kuiba kura,kwa hiyo Mungu yupo kazini.
Tayari ameshaanza kutekeleza hukumu yake.

Mtazame Bashiru leo hii pamoja na mali zake lkn sononeko la moyo linamnyima raha kabisa .

Maana kashuushwa kama embe boribo za tanga zinavyo poromoka kutoka juu hadi chini.
 
WABUNGE WALIOJIPELEKA BUNGENI NANI ANAWALIPA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Jana baada ya Mchango wa Mhe Halima Mdee Bungeni ambao binafsi niliupenda sana kutokana na umahili wake wa kujenga hoja, baadae alisimama Mhe Kunambi na Mhe Jerry Silaa ambao ni Wabunge wa CCM kujaribu kupinga hoja zake.

Mhe Silaa akiwa anaenda kuhitimisha hoja yake alisema kuna Wabunge wapo Bungeni hata vyama vyao vinawakana. Hapa ndipo nitajenga msingi wa hoja yangu.

Turudi kidogo nyuma kwa maana ya misingi ya kisheria inayoongozwa na sheria Mama ambayo ni Katiba ya JMT. Kwa mjibu wa Ibara ya 66(1) imetaja aina ya Wabunge watakao paswa kuwepo Bungeni kuwa ni watano. Lakini mgogoro uliupo sasa ni Wabunge wanaotajwa katika Ibara ya 66(1)(b) Wabunge wanawake.

Mwanzoni baada ya majina yale kuapishwa tuliambiwa yameletwa na CHADEMA. Hata CHADEMA walipokataa kuwa hatujaleta Spika na Tume ya Uchaguzi walisema yametoka CHADEMA.

Ibara ya 67(1) inazungumzia juu ya sifa anazopaswa kuwa nazo mtu anayeitwa Mbunge. Sifa moja wapo kati ya sifa hizo kuu tatu ni sifa inayotajwa katika Ibara ya 67(1)(b) inasema lazima AWE MWANACHAMA wa Chama cha Siasa.

Sambamba na hoja hizo, Ibara ya 78 bado inazungumzia Wabunge wa Viti maalum ambao ndio msingi wa hoja yangu hapo chini. Ibara ya 78(1) inazungumzia namna vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi vitakavyo pendekeza majina kwa Tume ya Uchaguzi. Lakini pia Ibara hiyo hiyo ya 78(4) inayotanguliwa na Ibara ndogo ya (3) inasema "Orodha ya majina ya wagombea wanawake iliyowasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi na kila Chama kwa ajili ya Uchaguzi mkuu ndiyo itakayotumiwa na Tume ya Uchaguzi baada ya KUSHAURIANA NA CHAMA KINACHOHUSIKA.....

Baada ya kunukuu Ibara ya 66, 67 na 78 ninaomba kuuliza Tume ya Uchaguzi na Ofisi ya Spika Mhe Job Yustin Ndugai. Kwa nini jana wakati Mhe Silaa anawakashifu Wabunge kuwa vyama vyao vinawakaa hukuwatetea? Je ni sheria ipi inayoruhusu mtu kuwa Mbunge bila kuwa na Chama cha Siasa? Je, Silaa ni mwongo, mzushi na mfitini na hali ya kukataliwa siyo kweli? Kama ni kweli wamekataliwa,je kwa mjibu wa Ibara ya 78(4) inayosema Chama cha Siasa kitashauriana na Tume, je Tume ilishauriana na Viongozi wa CHADEMA? Je, kama tume haikushauriana na CHADEMA walitumia sheria ipi kuwafanya watu wasio na Chama kuwa Wabunge?

Wapo wanaojaribu kutumia precedent ya Zitto kama case study ya hawa Wabunge wanaosemekana hawana Chama kilichowadhamini, ukweli ni kuwa kesi ya Mhe Zitto Zuber Kabwe ilikuwa mahakamani na ndio maana kulitokea hiyo injuction. Je hawa wamefungua kesi mahakamani?

Sheria hizi zilitungwa na Bunge, je kama mliotunga sheria mnashindwa kuziheshimu vipi kwa ambao si washiriki wa kutunga hizo sheria. Ninadhani ni muda mwafaka kujitokeza hadharani watu wa Tume ili kuweka uhalali wa hawa watu kuendelea kuitwa Wabunge. Kinyume na hapo Wabunge wako wataendelea kudhalilishana kuitana majina ya hovyo. Lakini hata sisi walipa kodi tunataka kujua kama kodi zetu zinawalipa Wabunge halali au Wabunge wa kutengenezwa.

Ahasante.
Anything goes! Wavunja nchi ni wananchi!
 
Back
Top Bottom