Hawa ndio Kamati Kuu ya CCM ambao maweshika roho za watia nia, TAKUKURU watawezana?

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
29,947
2,000
20200723_165150150720.jpg


Huu ndo wakati wa Kamati Kuu kuchanua,wagombea na watia nia wanahaha kuweka mambo vizuri kwa wajumbe. Kuna watu wametoshana kwenye kura, kuna watu wana tuhuma za rushwa hawana uhakika wa jina kurudi.

Itoshe tu kusema kwamba wajumbe ndio wakati wao huu wa kunyenyekewa na kula vya bure. Anayesema rushwa zinaishia ngazi za chini anyooshe mkono.

CCM si ndio hawahawa? Tuseme PCCB hamjasikia michakato ya kuwawinda wajumbe hawa? Nimeambiwa kigezo cha kuwaengua waliotoa rushwa kinakuwa kigumu kwa sababu hakuna aliyepita bila rushwa. Ukiwatoa ina maana umewatoa wote.
 

Mingoi

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
11,233
2,000
Kamati kuu imeshaishiwa pumzi walitegemea rushwa ingetolewa na makapuku. Shida hiki kipindi wenye tuhuma ni wake za Marais wastaafu, watoto wao, wabunge waandamizi, makada na watoto wa mageneral wa jeshi. Kazi kwenu KAMATI KUU kupasua mtungi na kuumua nyoka au muuinamishe halafu nyoka atoke auawe. Haki ikitendeka itazaliwa CCM MPYA tuliyoihubiri na kutoa machapisho na matamko mengi.
 

katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
640
500
Kamati kuu imeshaishiwa pumzi walitegemea rushwa ingetolewa na makapuku. Shida hiki kipindi wenye tuhuma ni wake za Marais wastaafu, watoto wao, wabunge waandamizi, makada na watoto wa mageneral wa jeshi. Kazi kwenu KAMATI KUU kupasua mtungi na kuumua nyoka au muuinamishe halafu nyoka atoke auawe.
Hakuna kiongozi wa kisiasa anayegombea bila kutoa rushwa. Hayupo hata mmoja awe wa CCM au upinzani. Tofauti ni kwamba mtoaji ametoa kiasi gani na kwa nafasi gani lkn wote ni watoa rushwa.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,121
2,000
CCM sio Tena chama Cha wakulima na wafanyakazi, Sasa ni chama Cha majangili Kama yule aliyekutwa na lundo la silaha na bado amepitishwa kwa kura nyingi kugombea ubunge.
Sisiemu ifyeke mijitu ya aina hii
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
2,305
2,000
Kila la kheri!

Samahani mkuu. Hapo umemaanisha wapokea rushwa ni wakina nani?
 

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
12,966
2,000
Hapo hoja ni kujaribu kuchafua watu na kazi zao

Hebu tufikirie utaratibu wa vyama kutaka wagombea wathibitishwe na hiyo kamati ndio wa hovyo kabisa


Chadema wametangaza watakuwa na Mkutano mkuu wa kuthibitisha wagombea wao hivi walio piga kura majimbo husika wakasikia mtu wao amekatwa huoni utaratibu wa kamati kuu ni kuweka watu watao wanyenyekea


Kamati kuu kwenye vyama vya siasa ni mbinu ya kupachika wa kwao ufutwe tu

Wajumbe wanatosha
 

ikipendaroho

JF-Expert Member
Jul 26, 2015
3,493
2,000
Nimeutizama Muundo wa hiyo kamati kuu.kwa juu juu nimegunduwa kuna mwaka itatokezea kuwa na wajumbe wengi kutoka Zanzibar. Lakini wa Zanzibar hawawezi kupunguwa zaidi ya hapo katika mfumo huu wa sasa. Kuna siku Speaker wa bunge la JMT, Waziri mkuu, Katibu mkuu na katibu uenezi, Wenyeviti wa Jumuia za chama baadhi yao wakiwa Wazanzibar.
 

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
2,999
2,000
Kwakua wajumbe hawalipwi ushauri chama kiseme kura za maoni zirudiweina maana wale watoa pesa mda huu pesa hawana watahonga nini wajumbe,

Sema sasa uko kigamboni kwenyewe usirudiwe chonde chonde😂😂
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,921
2,000
CCM sio Tena chama Cha wakulima na wafanyakazi, Sasa ni chama Cha majangili Kama yule aliyekutwa na lundo la silaha na bado amepitishwa kwa kura nyingi kugombea ubunge.
Sisiemu ifyeke mijitu ya aina hii
Unaweza kukuta hapo kuna wajumbe wa KK ambao wameshapokea bahasha. CCM hawaaminiki tena
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom