Kuhusu Rushwa kura za maoni CCM: Wahojiwe Wajumbe wenyewe na siyo kusubiri ushahidi wa TAKUKURU

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Katika kitu ambacho CCM kitabugi ni kupata ushahidi kutoka TAKUKURU ambao tumeona maeneo mengi kabisa nchini wameshindwa kuwajibika ipasavyo.

TAKUKURU maeneo mengi rushwa zimetolewa wazi wazi na wanaangalia bila kuchukua hatua yeyote. Mimi natoka Wilaya ya Singida Vijijini, lakini Wilaya zote za mkoa wangu zikiongozwa na Itamba, Mkalama, Ikungi, Singida vijijini hali ilikua inatisha Mungu anasikia ninachokiandika hapa.

Watia nia walikua wanashindana kwa madau ya mapema kwa wajumbe. Kama ni kuwajibishwa tuanze na kamanda wa TAKUKURU wa mkoa ameshindwa kabisa kuwajibika. Kamati zote za siasa za wilaya na mkoa ziwajibishwe ipasavyo.

Rais Magufuli wa kumvusha ni wale wanaopenda haki na sio hawanaogawa na kupokea rushwa. Majina ya walioshinda kwa rushwa yakirushwa nawaambieni wapinzani watapigiwa kura za hasira na watashinda.

Sasa cha kufanya ni nini?

Chama tumieni vyanzo vyenu vya Chama kuhoji wajumbe moja kwa moja, msisubiri TAKUKURU hawa ambao kutwa tunawaona wako mitaani na walalamikiwa. Kuna kitu wao wanaita kusawazisha, yaani kusawazisha maana yake ni kuhakikisha kua vyombo vyote vya udhibiti wao wanavidhibiti sawa sawa, jiulize vinasawazishwa kivipi? Swali kwako msomaji. Sasa hatujui haya malalamiko ya RUSHWA nchi nzima ndio kweli vyombo hivi kudhibitiwa na watoa rushwa kweli?

Nilisikia chama pia kimechomeka watu wake kujifanya nao ni watia nia kumbe wako kwenye majukumu. Ngoja tuone maamuzi kama ni kweli yataakishi yaliyosemwa na kina Dkt. Bashir na Pole Pole.

Ni hayo tu kwa uchache.
 
Kuna mgombania mmoja wa CCM alisema kama babalao kampa hawara nyumba, kwao haitakuwa dhambi kuwahonga wajumbe.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom