Hizi ndizo sababu kuu za mafuriko ya watia nia CCM

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Mwaka 2019 rafiki yangu wa karibu alinishauri ifikapo 2020 nigombee ubunge. Baada ya kukataa ushauri wake alisema ndani ya CCM hususana serikali ya awamu ya 5 hata ukishindwa ubunge unaweza fikiriwa nafasi nyingine za uteuzi kama ukurugenzi, ukuu wa mkoa, wilaya na makatibu tawala mikoa na wilaya kama ilivyotokea 2015

Hizi hapa ndizo sababu kuu za mafuriko ya watia nia na wachukua fomu ndani ya CCM.

1. Wana CCM wengi wanaamini hata wakishindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama au kwenye kinyang'anyiro chenyewe wanauhakika wa kuteuliwa na rais kwenye nafasi mbalimbali kama ilivyotokea 2015

2. Wana CCM wengi wanaamini uchaguzi wa mwaka huu 2020 utakuwa rahisi sana na usio na gharama kubwa za kampeni kwani ukishapitishwa ndani ya chama unakuwa tayari mshindi kwani hakuna mpinzani atakayeshinda mwaka huu. Jana rafiki yangu aliyetia nia kwenye ubunge alinambia "Siunajua mwaka huu kama uchaguzi wa serikali za mitaa, chama kikikupitisha umeshashinda tayari.

3. Wanachama wengi wa CCM wanaamini kutangaza tu nia ya kugombea ubunge au udiwani unaweza pata pesa/ hongo na mpinzani wako ndani ya chama au nje ya chama hasa majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wakongwe, vihiyo na wahindi. Wanaposikia tu unataka kugombea wanaweza kukufuata na mpunga wa kutosha iliusigombee. Kumbe kutia nia tu ni mtaji hata kama hutagombea.

Hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, haya mafuriko ya watia nia wa CCM wametengenezwa 2015 na rais, hivyo kazi ni kwake kuwateua wote mara baada ya uchaguzi ( 2020)

Swali, je haya mafuriko ya watia jimbo moja tu 80 atawateua wote? Kama atafanya hivyo basi inawezekana mpaka watendaji wa vijiji watateuliwa na rais ili kuwezesha kila mtia ni apate nafasi kama kweli hili lipo.

Mungu ibari Tz, Mungu ibariki Afrika.
 
Ubunge ni kazi rahisi sana, ambayo hata vilaza wanaweza fanya

Ulishaona nigeria, south africa, USA, vilaza wa la saba wanaingia bungeni??

Waweke hata vigezo basi, ubunge unaenda kuonekana ni kazi ya hovyo kabisa.
 
Ubunge imekuwa kazi rahisi sana.
1.Kuimba NDIOOOOO na kugonga meza sana kwa lolote litakiwalo na serikali
2.Kujadili udaku kama spika anavyotaka badala ya maendeleo.
3.Kujitenga na kuisimamia serikali.
4.Kushangilia na kumpongeza YESU wa Burigi hata kwa kunywa maji
 
Mwaka 2019 rafiki yangu wa karibu alinishauri ifikapo 2020 nigombee ubunge. Baada ya kukataa ushauri wake alisema ndani ya CCM hususana serikali ya awamu ya 5 hata ukishindwa ubunge unaweza fikiriwa nafasi nyingine za uteuzi kama ukurugenzi, ukuu wa mkoa, wilaya na makatibu tawala mikoa na wilaya kama ilivyotokea 2015

Hizi hapa ndizo sababu kuu za mafuriko ya watia nia na wachukua fomu ndani ya CCM.

1. Wana CCM wengi wanaamini hata wakishindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama au kwenye kinyang'anyiro chenyewe wanauhakika wa kuteuliwa na rais kwenye nafasi mbalimbali kama ilivyotokea 2015

2. Wana CCM wengi wanaamini uchaguzi wa mwaka huu 2020 utakuwa rahisi sana na usio na gharama kubwa za kampeni kwani ukishapitishwa ndani ya chama unakuwa tayari mshindi kwani hakuna mpinzani atakayeshinda mwaka huu. Jana rafiki yangu aliyetia nia kwenye ubunge alinambia "Siunajua mwaka huu kama uchaguzi wa serikali za mitaa, chama kikikupitisha umeshashinda tayari.

3. Wanachama wengi wa CCM wanaamini kutangaza tu nia ya kugombea ubunge au udiwani unaweza pata pesa/ hongo na mpinzani wako ndani ya chama au nje ya chama hasa majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wakongwe, vihiyo na wahindi. Wanaposikia tu unataka kugombea wanaweza kukufuata na mpunga wa kutosha iliusigombee. Kumbe kutia nia tu ni mtaji hata kama hutagombea.

Hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, haya mafuriko ya watia nia wa CCM wametengenezwa 2015 na rais, hivyo kazi ni kwake kuwateua wote mara baada ya uchaguzi ( 2020)

Swali, je haya mafuriko ya watia jimbo moja tu 80 atawateua wote? Kama atafanya hivyo basi inawezekana mpaka watendaji wa vijiji watateuliwa na rais ili kuwezesha kila mtia ni apate nafasi kama kweli hili lipo.

Mungu ibari Tz, Mungu ibariki Afrika.
Wapo CCM kimwili lakini akili zao zipo Chadema
 
Back
Top Bottom