Maamuzi ya kamati kuu CCM kuhusu wateule itakuwa ndio fyuzi ya kulipua bomu linalotokota CCM

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Huko CCM kuna bomu linatokota. Bomu hili linaitwa kwa majina tofauti. Umaarufu wake 'WAJUMBE"

Ni wazi kuwa kuna mchanganyiko wa sababu. Zikiwemo mtifuano wa CCM mpya na kongwe.

Rushwa na nguvu ya pesa.

Vita ya madaraka kuelekea 2025 ndani ya CCM.

Amini kwamba maamuzi ya Kamati kuu kuhusu wajumbe waliopitishwa yataleta madhara mbali mbali na itategemea hoja hizo tatu na vipi chama kama kilipokea taarifa sahihi kutoka chini.

Mkiwaamini TAKUKURU mjuwe wako walionunuliwa na wao vile vile wana mapenzi yao na watu wao kwenye chama.

Malalamiko ni mengi na mchanganyiko.

Kuna hatari Kamati kuu ikawa na wajumbe ambao wote wakawa na mlengo mmoja wa ama kuwa wanaunga mkono WANA CCM MPYA, ama wanaojipanga kuweka safu mpya ya madaraka baada ya utawala wa sasa na hivyo kwa namna moja ama nyengine kuathiri mchakato na kuacha uhalisia huko majimboni.

Kauli za Mwenezi Polepole sio kwamba zinaashiria kukoleza joto la kufyatuka kwa fyuzi lakini ziaashiria vile vile kuifanya fyuzi ikomae zaidi.

Huko majimboni kuna habari nyingi na kutegemea taarifa za TAKUKURU PEKEE na wale vijana wea Usalama wa chama bila kuwa na njia nyengine si rahisi UKWELI kujulikana kutokana na mazingira ya sasa.

Hapa tunataka kupima umakini wa viongozi wa CCM. Kilicho wazi kweli rushwa imetumika sana mara hii LAKINI na Fitna ya CCM mpya na Kongwe ndiyo sababu kuu. Kunahitajika maamuzi sahihi na kuwepo taarifa sahihi.

Wako watu wanaomuunga Mkono Mwenyekiti na wameshika nafasi nyeti serikalini lakini kwenye mchakato walitoa rushwa ya wazi na hao hao ndio CCM mpya. Je, jicho la haki litasimamia ukweli?

Tunasubiri muda uhukumu.

Tunawatakia maamuzi mema.

"Kweli wajumbe sio watu"

Kishada
 
4
 
Wajumbe wametoa dira tu
Subirini kuchukua makapu Kama kawaida yenu
Puuzeni maoni ya Wajumbe mkione cha moto
Mjumbe alika kuku kwa mrija kwa gharama ya mgombea.  Endelea kujipatia Kitabu ch ( 799 X 640 ).jpg
 
Wajumbe wametoa dira tu
Subirini kuchukua makapu Kama kawaida yenu
Umetumia kilevi gani man? Maana uko nje ya mada. Teuzi za upoinzani zimeshakamilika kwa ngazi zote.
Mada inaongelea watu kama Dr. Kigwangalla, Dr. Tulia na Dr. Mwanjelwa waliotoa rushwa waziwazi na kugawia wajumbe basikel, bodaboda na mikopo nafuu. Hawa ndio ambao Polepole alikuwa anawaongelea jana, kwamba je watatoboa kwenye hili sakata?
 
Mambo ya ccm mwaka huu yapo interesting mpaka wapinzani mnafuatilia kweli mwaka huu magafuli anapita bila shida.
 
Magufuli ataweka watu wake watakao mpigia debe la kusalia madarakani baada ya 2025.
 
Sipati picha kule ambapo aliyeongoza kura za maoni ana tuhuma wazi za rushwa mpaka kuhojiwa na takukuru wakati anayemfuatia anatuhumiwa kuwa nyumba andamizi ya
m/tiki.
Ukimuengua huyu wa kwanza kwa visingizio vya kutoa rushwa lazima ukabiliane na tuhuma za kuwa ulipanga toka mwanzoni kumpendelea huyu nyumba andamizi ambayo pia ni rushwa.

Yajayo yanasisimua.
 
[SUP]kaka mbona unawatonya mapema???? Membe anamaliza kazi.....[/SUP]

[SUP]hii ni sukuma mlevi [/SUP]
 
Kuna mtu unamwonea huruma?
Chama kina utaratibu wake yale yalikua maoni na si maamuzi.
Pili chama kina dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa hivyo hata kingempitisha mtu wa thelathini na kitu hakita ogopa kuwapelekea wananchi watu Safi na sahii.
 
Ndio tukaandika hapa ili wahusika watende haki. Hofu yangu isije ikawa taarifa walizopelekewa ikawa zilifika kwa misingi ile ile ya hizi hoja tatu hapo juu.
 
Ukiyajua yaliyoko field huko majimboni, unasisimka. Kuna wakubwa huwezi amini imekuwa kama icon ya chama lakini amepita kwa mizengwe. Amini nakwambia baadhi ya majimbo kashfa zinarudi hadi kwa wagombea wa kitaifa. Jee najiuliza haki itatendeka?
 
Back
Top Bottom