Uchaguzi 2020 Watia nia wengi CCM wameshakosa sifa za kuteuliwa

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
WATIA NIA WENGI CCM WAMESHAKOSA SIFA ZA KUTEULIWA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Twende na Kanuni ya 35 ya Kanuni za uchaguzi wa Ccm za 2017.

Kwanza katika kanuni hizi ambazo ndio msaafu wa maelekezo ya kupatikana kwa viongozi ccm hakuna kitu kinaitwa kutangaza/kutia nia.

Tukiachana na hilo, ni kosa kwa mujibu wa Kanuni hizi mgombea yeyote kujitambulisha kwa wale wanaotarajia kumpigia kura.

Nanukuu Kanuni ya 35(16)
" Ni marufuku kwa mgombea wa ngazi yoyote kuzunguka Matawini, Katani, Wilayani na Mikoani kukutana na wajumbe wa Mkutano utakaomchagua kwa kisingizio cha KUJITAMBULISHA , kuwasalimu wajumbe, au kuwapa nauli. Mgombea atakayethibitika anazunguka ataondolewa katika orodha ya wagombea".

Kwa nukuu hii nawaona watangaza nia wengi kama sio wote wakikosa sifa. Watangaza nia wengi hasa wa ubunge wako Matawini na Katani wakiwapitia wajumbe ama kwa WATIA NIA WENGI CCM WAMESHAKOSA SIFA ZA KUTEULIWA. au kuwasalimia.

Sio siri hali ya kujitambulisha kwa Wajumbe ilivyo kwa watia nia huwezi amini kama kuna Kanuni ya namna hii.

Kwa ufupi, kama kweli chama kinasimamia nidham na kanuni kama kinavyojinasibu, hakuna shaka watu hawa wataondolewa katika orodha kama kanuni yenyewe inavyoelekeza.

Nanukuu kanuni nyingine ya 35(12),
" Ni mwiko kutumia makaratasi ya kampeni nje ya utaratibu wa chama au kutumia vishawishi vya aina yoyote kwa minajili ya kupata kura".

Watia nia wengi ķama sio wote wametengeneza makaratasi/vipeperushi vya kampeni nje kabisa ya utaratibu. Vipeperushi hivi pia ni ushawishi unaokatazwa na kanuni hapo juu. Vinasambazwa whatsap, facebook na kila pahala.

Wengine wamethubutu hata kuomba kura kwenye vipeperushi hivyo, achilia mbali wale wanaovitumia kunadi sera za nini watafanya. Ni hatari. Wanafanya hivi kinyume cha utaratibu na wakati ambapo kampeni hazijaruhusiwa. Wanacheza rafu bila soni.

Watu wamepagawa kama vile chama hakina taratibu za kampeni na uchaguzi. Heri yao waliokaa kimya, huenda hili likawa neema kwao.

Matumaini yangu ni kuwa, kwa watu wa aina hii wote Chama Cha Mapinduzi ambacho kinajitanabaisha kulinda Nidham,Utangamano,Miiko, Maadili na Kanuni kitajielekeza katika Kanuni ya 36 kushughulika na watu wa namna hii, kama inavyonukuliwa hapa, "Kiongozi au Mwanachama yeyote atayethibitika kuwa amevunja kifungu chochote cha miiko hii atathibitiwa. Ikibidi atanyang'anywa ushindi alioupata na kukatazwa kugombea uongozi kwa muda utakaowekwa".

Angalizo langu kanuni hizi lazima zifuatwe. Ziliwekwa kwa makusudi maalum. Kujitambulisha tambulisha huku ndiko kunakozaa rushwa. Kimsingi ndiyo rushwa yenyewe.

Mchakato mzima wa uchaguzi unaweza kuchafuliwa na kuchafua sura nzima ya chama ikiwa mambo haya yatafanywa ya kawaida na kutokuchukuliwa hatua. Kanuni zimeshaelekeza watu wa namna hii wafanywe nini hivyo hatutarajii zaidi ama chini ya hapo.

Mwisho, ili uwe kiongozi hauhitaji tu kujua nini utafanya kwa watu, bali pia ni njia gani itakufikisha huko. Kanuni na miiko ni gari muhimu kukusafirisha hadi kileleni mwa uongozi . Ni dhahiri watu wanataka kugombea lakini hawajui kabisa kama kuna kitu kinaitwa KANUNI ZA UCHAGUZI.
 
Mkuu kuchukua fomu tar 14 kurudisha July 17, kura za maoni tar 23 July ni muda mfupi sana kumfahamu mtu, angalao huku kujipitishapitisha ambayo kiukweli ndio kutangaza nia kutatufanya tuwagahamu potential candidates, na sijaona limit iliyowekwa kwenye kujipitishapitisha huku. Zaidi ya kutofanya campaign au kutoa zawadi zozote. Hivyo vipeperushi kama umeandika jina na picha yako bila kuweka maneno ya campaign sioni shida. Hata kutembelea matawi for 5 to 10 minutes wakujue bila kufanya mkutano wa campaign sioni shida ingawa kiukweli kutangaza nia ni kama kakampaign kadogo hivi. I stand to be corrected.
 
Ile issue ya mitandao YA SIMU KUWAIBIA WATEJA iliishia wapi? Au ile principle ya PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA!
 
Mkuu kuchukua fomu tar 14 kurudisha July 17, kura za maoni tar 23 July ni muda mfupi sana kumfahamu mtu, angalao huku kujipitishapitisha ambayo kiukweli ndio kutangaza nia kutatufanya tuwagahamu potential candidates na sijaona limit iliyowekwa kwenye kujipitishapitisha huku zaidi ya kutofanya campaign au kutoa zawadi zozote. Hivyo vipeperushi kama umeandika jina na picha yako bila kuweka maneno ya campaign sioni shida, hata kutembelea matawi for 5 to 10 minutes wakujue bila kufanya mkutano wa campaign sioni shida ingawa kiukweli kutangaza nia ni kama kakampaign kadogo hivi. I stand to be corrected.

Hivi miaka iliyopita ilikuwa hivi au? Watu kwa sasa, wamedaka code ya Mkulu kiurahisiiiiii
 
WATIA NIA WENGI CCM WAMESHAKOSA SIFA ZA KUTEULIWA.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Twende na Kanuni ya 35 ya Kanuni za uchaguzi wa Ccm za 2017.

Kwanza katika kanuni hizi ambazo ndio msaafu wa maelekezo ya kupatikana kwa viongozi ccm hakuna kitu kinaitwa kutangaza/kutia nia.

Tukiachana na hilo, ni kosa kwa mujibu wa Kanuni hizi mgombea yeyote kujitambulisha kwa wale wanaotarajia kumpigia kura.

Nanukuu Kanuni ya 35(16)
" Ni marufuku kwa mgombea wa ngazi yoyote kuzunguka Matawini, Katani, Wilayani na Mikoani kukutana na wajumbe wa Mkutano utakaomchagua kwa kisingizio cha KUJITAMBULISHA , kuwasalimu wajumbe, au kuwapa nauli. Mgombea atakayethibitika anazunguka ataondolewa katika orodha ya wagombea".

Kwa nukuu hii nawaona watangaza nia wengi kama sio wote wakikosa sifa. Watangaza nia wengi hasa wa ubunge wako Matawini na Katani wakiwapitia wajumbe ama kwa WATIA NIA WENGI CCM WAMESHAKOSA SIFA ZA KUTEULIWA. au kuwasalimia.

Sio siri hali ya kujitambulisha kwa Wajumbe ilivyo kwa watia nia huwezi amini kama kuna Kanuni ya namna hii.

Kwa ufupi, kama kweli chama kinasimamia nidham na kanuni kama kinavyojinasibu, hakuna shaka watu hawa wataondolewa katika orodha kama kanuni yenyewe inavyoelekeza.

Nanukuu kanuni nyingine ya 35(12),
" Ni mwiko kutumia makaratasi ya kampeni nje ya utaratibu wa chama au kutumia vishawishi vya aina yoyote kwa minajili ya kupata kura".

Watia nia wengi ķama sio wote wametengeneza makaratasi/vipeperushi vya kampeni nje kabisa ya utaratibu. Vipeperushi hivi pia ni ushawishi unaokatazwa na kanuni hapo juu. Vinasambazwa whatsap, facebook na kila pahala.

Wengine wamethubutu hata kuomba kura kwenye vipeperushi hivyo, achilia mbali wale wanaovitumia kunadi sera za nini watafanya. Ni hatari. Wanafanya hivi kinyume cha utaratibu na wakati ambapo kampeni hazijaruhusiwa. Wanacheza rafu bila soni.

Watu wamepagawa kama vile chama hakina taratibu za kampeni na uchaguzi. Heri yao waliokaa kimya, huenda hili likawa neema kwao.

Matumaini yangu ni kuwa, kwa watu wa aina hii wote Chama Cha Mapinduzi ambacho kinajitanabaisha kulinda Nidham,Utangamano,Miiko, Maadili na Kanuni kitajielekeza katika Kanuni ya 36 kushughulika na watu wa namna hii, kama inavyonukuliwa hapa, "Kiongozi au Mwanachama yeyote atayethibitika kuwa amevunja kifungu chochote cha miiko hii atathibitiwa. Ikibidi atanyang'anywa ushindi alioupata na kukatazwa kugombea uongozi kwa muda utakaowekwa".

Angalizo langu kanuni hizi lazima zifuatwe. Ziliwekwa kwa makusudi maalum. Kujitambulisha tambulisha huku ndiko kunakozaa rushwa. Kimsingi ndiyo rushwa yenyewe.

Mchakato mzima wa uchaguzi unaweza kuchafuliwa na kuchafua sura nzima ya chama ikiwa mambo haya yatafanywa ya kawaida na kutokuchukuliwa hatua. Kanuni zimeshaelekeza watu wa namna hii wafanywe nini hivyo hatutarajii zaidi ama chini ya hapo.

Mwisho, ili uwe kiongozi hauhitaji tu kujua nini utafanya kwa watu, bali pia ni njia gani itakufikisha huko. Kanuni na miiko ni gari muhimu kukusafirisha hadi kileleni mwa uongozi . Ni dhahiri watu wanataka kugombea lakini hawajui kabisa kama kuna kitu kinaitwa KANUNI ZA UCHAGUZI.
Ccm iliyokuwa inatumia hizo kanuni ilishakufa siku nyingi kuanzia 2015 mpaka hii CCM mpya ni mwendo wa matamko hakuna cha kanuni wala sheria
 
Back
Top Bottom