Hawa Celebrity Wako Wapi Siku Hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa Celebrity Wako Wapi Siku Hizi?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Ndallo, Feb 25, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Amina Ngaluma
  [​IMG]
  Badi Bakule Jogoo la mujini!
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wako TOT Plus na Mwl Komba aka Capt Komba!
   
 3. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Aah, Amina Ngaluma a.k.a Japanese! Kwani TOT Plus bado ipo? Inasherehesha wapi siku hizi??
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Walinikuna sana enzi hizo hawa jamaa!
   
 5. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani Badi Bakule bado yupo TOT sema TOT yenyewe haivumi na wala haimo.
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  TOT haiwezi kuvuma kwa wakati huu kwani kisima cha hela kimekauka na ndio maana hata kwenye uchaguzi uliopita hawakusikika sana kwani kulikuwa hakuna EPA!!
   
 7. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na kweli ndo maana captain kaamua kuchagua njia ya maombi bungeni badala ya kuchangia hoja ili siku ziwe nzuri kama zamani.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu, ungemaliza kama ungekuwa umemweka na mtu alikuwa akitwa SHAABAN MWEZINGO SIKU HIZO.

  nAKUmbuka jinsi Badi Bakule alivyoimba shairi la MGUMBA:  nAKUSIHI WALA USITIE KUFURU MWENZANGU EE
  Kupata na kukosa ni kazi yake maulanaa
  Elewa MUNGU ana mitihani yakeee
  Kaumba matajiri na mafukara kama mimi,
  kaumbva vilema na wazima
  Matasa au Wagumba, yote ni kazi yakeeeee   
 9. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mkuu nadhani anaitwa RASHID MWENZINGO!
   
 10. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,719
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  wamefulia..........:wink2:
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  duu halafu anaingia muumini, iiiiiii iiiiiiiiiiiii iiiiiii mgumba we
   
 12. movingtarget

  movingtarget Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahaha...watu mna hisia kali kweli....
   
 13. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  pitia pitia mitaa ya mwananyamala hutowakosa...
   
 14. GP

  GP JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hebu jikumbushe wimbo wao maarufu enzi hizo wa MTEGEMEA CHA NDUGU:

  intro.....

  chandeeeeeee, asubuhi kumekucha kumepambazuka Chandeeeee,
  Chandeeeee eeh, tuamke kumekucha tukajitafutie riziki yetuu,
  Ooh ooh Chandeeee,
  aah Shabani Bakule, mamaa leticia Kato, sema na Adam, Omar Baraka, Almas,
  Chande, japokua wanasema riziki haivutwi kwa kamba Chande,
  lakini usipoitafuta huwezi kupata, kwa vile mafanikio hayaji ndoto OOH,
  aaah mwenda pole, Mr K.H Ngaluma, Kocha wa dunia,

  Chande, japokua wanasema riziki haivutwi kwa kamba Chande,
  lakini usipoitafuta huwezi kupata, kwa vile mafanikio hayaji ndoto,

  sema saaana lakini utakua mpole ghafla,
  maisha mtego, ukisepetuka umenasa,
  maisha popote, maisha mahesabu,

  Chorus,,,,,,,,,

  kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
  elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,
  kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
  elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,

  [BADI BAKULE,,,,,,,,,]

  oooh, Badi mi nasema, inakupasa uelewe ya kuwa umri haurudi nyuma,
  miaka inazidi kwenda mbele maisha ni mapambano,
  ona wenzetu wanavyo yatafuta maisha chande,kila kunapokucha pilikapilika haziishi,
  wengine maofisini, wakulima mashambani,
  na wafanya biashara nao pilikapilika,
  wengine ujerumani, wengine south africa, na wengine america katika kujitafutia aaah aaah,
  ooh mama leleee, muheshimiwa Richard Ndassa, mueleze Chande ajitafutie kama sisi eeh,
  John Badi na Badi Bakule mueleze Chande ajitafutie kama sisi eeh,
  na Baraka Musilwa mueleze Chande ajitafutie kama sisi,
  kila kunapokucha pilikapilika haziishi, za kutafuta maisha yetu ya leo na kesho,
  usipojitafutia hakuna wa kukutafutia,
  kwa vile maisha ya sasa ni vuta nikuvute kila mmoja huvutia kwake (ya muamba ngoma), ooh mama iyeee,
  utakuja kumulilia nani eeh, wakati umekwishapinda mgongo ooh, na nguvu za kutafuta tena huna,
  ukitazama nyuma mzigo mkubwa wa familia eeh, we bwana umekuelemea,

  [RASHIDI MWENZINGO,,,,,,,,,,,]

  yoyooo, rafiki Chande ananishangaza sana,
  yoyooo, rafiki Chande ananihuzunisha sana eeh,
  kazi nyingi anazozipata anashindwa kufanya, anategemea cha ndugu wakati uwezo hana iyoyoyo kaka,
  kazi yake ni kula kulala kwa kaka yake Mwenzingo,
  kazi yake ni kula kulala kwa mjomba wake Bakule,
  kazi yake ni kula kulala kwa dada yake Amina,
  kazi yake ni kula kulala kwa shangazi Asha Baraka, yoyoo Chande yatakushinda kaka,

  [BADI BAKULE,,,,,,,,,]

  aah iyoyoyoo eeh yatakushinda Chande,

  [AMINA NGALUMA,,,,,,,,,]

  hata sisi dadazako, tunakushangaa kwa tabia yako,
  unavyojiendekeza kwa kupenda vya bwerereeeee, aibu eeeh


  [MUUMIN MWINJUMA,,,,,,,,,]

  sure eeh,
  ooh ooh Chande weeh,
  ooh ooh Chande eeh,
  wanihuzunisha kwa vitendo vyako rafiki yangu,
  nimesikia kazi yako ni kushinda sebuleni tu,,,, wangoja kuitwa
  mara ooh Chande chai tayari huku,,,,, wangoja kuitwa
  mchana unauliza shemeji lunchi imewiva,,, alaah,,,,,,,, wangoja kuitwa,
  hata kazi ndogo ndogo zinakushinda Chande,
  hata jite riziki kidogo ana afadhali,
  wacha kutuliza boli, chakalika ndugu yangu, changamkia tenda,

  Chorus,,,,,,,,,

  kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
  elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,
  kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
  elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,


  ,,,,,,,,,
   
 15. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  We jamaa mkare mbayaa! Umenkumbusha mbali kwa kweli! Big up man!
   
 16. GP

  GP JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hii bendi kwa mwaka ule ilikua ni TISHIO kuzidi hata kaka zao twanga pepeta!, kwamaana jamaa walivutwa toka uarabuni na kenya wakawa kama ma-proo. Album nzima ilitisha kwa ujumbe mzito mwanzo mpaka mwisho.
   
 17. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  amina ngaluma yuko thailand....badi bakule ana kama miezi 2 toka arudi twanga akitokea levante musica ya morogoro hiyo ilikuwa baada ya kutoka TOT
   
 18. GP

  GP JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa kama alihama TOT kweli basi TOT ilikua imeishiwa!, Badi Bakule ni mmoja wa wanamuzi wenye historia ya kukaa bendi moja kwa muda mrefu sana bila kuhama hama.
   
 19. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,484
  Likes Received: 4,756
  Trophy Points: 280
  Badi Bakule-Twanga Pepeta Internationally
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Duh, hivi muumini anatanga na njia wapi? Manake kwa kuaga kashindikana.
   
Loading...