Havel azikwa mjini Prague

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Aliekuwa* Rais* wa Jamhuri* ya Czeck Vaclav Havel alizikwa jana mjini Prague na maalfu ya watu ikiwa pamoja na wanasiasa mashuhuri kutoka duniani kote.

Rais Sarkozy wa Ufaransa alikuwa miongoni mwa walioyahudhuria maziko hayo.

Wengine walikuwa Waziri wa mambo ya nje wa* Marekani* Hillary* Clinton* na* mumewe , Bill* Clinton aliekuwa Rais wa Marekani.

Rais wa Ujerumani Christian Wulff , Kansela Angela Merkel na Rais wa Kamisheni ya Umoja* wa Ulaya Jose Manuel Barosso pia walikuwapo mjini Prague kwa* ajili za maziko ya Vaclav Havel.

Hayati Havel, aliekuwa* mwandishi mashuhuri wa** tamthilia aliziongoza harakati za kuleta mabadiliko* ya kidemokrasia mnamo mwaka wa 1989 wakati nchi yake ilipokuwa ya kisoshalisti iiyokuwa inaitwa Czechoslovakia. Pia alitoa mchango* mkubwa katika Ulaya* ya mashariki baada* ya Umoja wa* Kisoviet,* Urusi* ya* zamani kusambaratika.
 
Thanks for the news..bourne identity,supremacy,ultimatum..do u know this also with this ID??'jasonbourne' in JF?
 
Umemsahau Madelaine Albright aliezaliwa huko na ambaye ndiye aliyetumiwa na Marekani kuisambaratisha Chekoslovakia kwa kumtumia huyu mzee kibaraka.
 
Back
Top Bottom