Obama, Hillary Clinton, pamoja na vyombo vyao vya habari Walikua wanamchukulia Gaddafi alikuwa dikteta

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,201
2,000
OBAMA SIO BINADAM WA KAWAIDA

Muammar Gaddafi alimpenda Barrack Obama kama mtoto wake wa kiume.

Wakati Obama alipokuwa rais wa Amerika , Gaddafi alikuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa Kiafrika ambao walimpongeza na kumsifu.

Gaddafi aliamini unabii wake umetimia, kwa sababu aliandika katika Kitabu chake cha Green kilichochapishwa mwaka 1975 kwamba, "Watu weusi watatawala ulimwengu".

Gaddafi pia alitoa msaada wake kwa watu Weusi huko Amerika mwaka 1985, aliwahakikishia atawasaidia kuwa na serikali yao huru na uchumi.

Kipindi Waziri Louis Farrakhan alipokutana na Gaddafi miaka ya 1980, alitoa msaada wake wa kifedha kusaidia kudumisha jamii zingine za Watu weusi kiuchumi huko Amerika, Gaddafi alitoa karibu dola milioni 5 na riba ya 0% kusaidia watu weusi huko Amerika.

Gaddafi alisimama na Waafrika Kusini wakati wa vita vyao dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini 🇿🇦 -aliwaunga mkono kijeshi, kimaadili na kifedha! Aliunga mkono kila harakati za ukombozi wa Watu weusi barani Afrika - na wana Diaspora!

Muammar Gaddafi alichukua urithi wa malengo ya aliekuwa Pan-Africanism na Waziri Mkuu wa kwanza wa Ghana Dk Kwame Nkrumah kwamba Afrika lazima iungane (United States Of Africa).

Gaddafi alitaka Africa liyofadhiliwa na Umoja wa Afrika ili kuilinda Afrika dhidi ya ushawishi wa wakoloni.

Gadafi alisaidia kuweka setilaiti ya kwanza ya mawasiliano inayo milikiwa na Afrika ilikuwezesha Waafrika kupata huduma rahisi ya mtandao na kuepusha kulipa zaidi ya dola milioni 500 Ulaya kila mwaka!

Gaddafi alifurahi kushirikana na viongozi wengi weusi kama Robert Mugabe wa Zimbabwe 🇿🇼, Nelson Mandela wa Afrika Kusini 🇿🇦, Thomas Sankara wa Burkina Faso 🇧🇫, Idi Amin Dada wa Uganda 🇺🇬, Sani Abacha wa Nigeria - nk. , alikuwa rafiki mzuri wa bondia mashuhuri 🥊 Muhammed Ali ,alikuwa mfuasi wa harakati za Malcolm X na Martin Luther King Jr nk* Gaddafi aliushtumu Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa 2009, kwa kutofanya uchunguzi sahihi au kuwashtaki wale waliohusika katika mauaji ya Martin Luther King Jr.

Wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2009, Gaddafi kwa mara nyingine tena alimpongeza Obama na kumsifu na hata kumuita mwana.

Walibya wanasema sisi WaLibya wa kweli hatuwezi kupima wala kuhesabu mazuri, upendo na fursa ambazo Gaddafi alitupatia, hatukumwua, tulimpenda na bado tunafanya hivyo - vyombo vya habari vya magharibi vilisema uwongo na uchonganishi mkubwa juu ya Gaddafi na wanachi wa Libya mwaka 2011.

Sisi kama wana Libya sauti zetu hazikusikika, hatukupewa nafasi ya kuzungumza wenyewe, wale waliomuua kiongozi wa brother ndio hao hudhibiti vyombo vya habari, na siku hizi yule anayedhibiti vyombo vya habari anatawala ulimwengu.
Ndio Gaddafi hakuwa mkamilifu, lakini hakuwa mtu mbaya kwani madikteta si ndio hao watu wa magharibi wakiamua kukuita gaidi ,dikteta basi kila chombo cha habari kitakuita majina hayo mabaya!

Hakukuwa na ubaguzi kati ya Waarabu, Watu weusi au Mzungu katika Libya ya Gaddafi, sisi sote tuliishi pamoja tukiwa kitu kimoja, hata utumwa ulimalizwa kwa kifo huko Libya.

Hata leo wale ambao wanafanya biashara ya wahamiaji wa Kiafrika katika masoko ya wazi ya watumwa leo sio Walibya, ni walowezi haramu na mamluki wa magaidi ambao jeshi la NATO liliwaleta Libya ili kuuangusha utawala wa Gaddafi! Wanataka kudai Libya kwamba ni ya kwao wenyewe!

Gaddafi alimpenda Obama, labda kwa sababu ya urafiki na mapenzi yake kwa viongozi wa mapinduzi wa Kiafrika ambao alishirikiana nao, na kwa sababu ya ukweli kwamba POTUS nyingine ilimchukulia Gaddafi kuwa adui wa Amerika, aliamini Obama atakuwa tofauti kwani yeye ni Mtu mweusi.

Alimchukulia kama mdogo wake mdogo hakujua kwamba Obama angeungana na jeshi la NATO kuharibu Libya na kumuua
."Ningependa kutumia fursa hii kumpongeza mtoto wetu, Obama, kwa sababu hii ni mara ya kwanza kuhudhuria Mkutano Mkuu wa UN katika nafasi hii kama rais wa Amerika 🇺🇸, na tunamsalimu kwa sababu pia anawakilisha nchi mwenyeji wa mkutano huu ”. Gaddafi na Obama mwaka 2009.

Lakini kwa mtazamo wa Obama, Hillary Clinton na makaa ya mawe ya magharibi, pamoja na vyombo vyao vya habari. Walikua wanamchukulia Gaddafi alikuwa dikteta mwovu na mbwa mwendawazimu wa jangwani.

Watu hawa ndio madikteta wa kweli, wanafiki na waongo wakubwa duniani!
 

kitali

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,475
2,000
Wajerumani wameua sana mababu zako kwenye Vita ya majimaji, Vita ya Kalenga na pia kule Ruvuma waliua kina chief Songea, Mbano na wengine wengi. Usijidai hujui historia yako na kuutukuza uzungu
Gadaf usisahau ndie aliyefadhili vita mbaya na mauaji ya kinyama kule sieralione kwa foday sanko. ndie mfadhil mkuu wa mauaji ya liberia kwa Charles Taylor. yule jamaa alikuwa muuji mzuri.
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,303
2,000
Nilijua umekuja na evidence kuwa obama ni alien.

Kumbuka ktk dunia hii only the stronger will survive and the weak will perish. ( survival for fittiness rule).

Kaa kwa kutulia usije na ww ukaliwa kichwa

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
Survival of the Fittest kaka...na sio Survival of Fittiness!!
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,417
2,000
Wajerumani wameua sana mababu zako kwenye Vita ya majimaji, Vita ya Kalenga na pia kule Ruvuma waliua kina chief Songea, Mbano na wengine wengi. Usijidai hujui historia yako na kuutukuza uzungu
Tatizo wewe huwa mkrupukaji, wapi nimesifia wazungu. Aidha hujui msimamo wangu kuhusu haya maswala
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom