Hawa ndo Wafuasi wa JPM..
Yaani mtu akimkosoa JPM watakuambia una chuki, na wengine watakusindikiza hadi na matusi!!
Hamwezi kujenga hoja nje ya chuki na most importantly, hamna hata FACTS.
OKAY, be prepared kusema kwamba nina chuki na ikibidi leta matusi but below are FACTS
1. UFISADI....
Kila mmoja anafahamu kwamba ufisadi nchi hii unafanywa sana na Top Government Officials (ministers, secretaries, directors) and High Profile Politicians.
Hadi JPM anatangulia mbele za haki, hakumgusa yeyote kutoka kwenye makundi hayo mawili, na kama yupo, NITAJIE
TAJA, manake ni kiroja kudai mtu alikuwa anapambana na ufisadi wakati Hao Architects wa Ufisadi wenyewe hakuwahi kuwagusa!
Hata Rostam ambae aliimbwa sana kwamba ni fisadi ni wakati wa JPM ndio alikuja tena kuibuka na Taifa Gas yake ambayo ilizinduliwa na "Mpiga Vita Ufisadi"
2. MIUNDOMBINU
Wafuasi wa JPM mnataka kuaminisha watu kwamba miundombinu ya nchi kama si Magufuli basi isingekuwepo!
-Wakati mnadanganya watu maelezo kama hayo, wafuatiliaji wanafahamu kwamba Flyovers ambazo mmekuwa mkitolea mfano zipo chini ya Mradi wa BRT ambao Mwasisi wake sio JPM
-Barabara za Dar es salaam zipo chini ya Mradi wa Dar es salaam Metropolitan Dev Project ambao JPM alikuta hadi funding imeshakuwa approved.
-Mchakato wa Tanzanite Bridge ulianza kabla hajawa Rais
-Barabara na madaraja mengi yamejengwa kabla JPM hajawa Rais
- Of course, tutampa Credit zake SGR, Ndege, Busisi, na Bwawa la Nyerere lakini hadi sasa Umeme unaotumika Tanzania JPM kaukuta!
3. UCHUMI...
Mwaka 2017 hatimae Benki ya Dunia ikatutangazia kwamba Tanzania imeingia Uchumi wa Kati (wa chini).
Tukaambiwa Marais WOTE waliotangulia walishindwa kuifikisha Tanzania Uchumi wa Kati lakini JPM aliweza within 2 years.
Ajabu ilikuwa ukiangalia Takwimu za hao hao Benki ya Dunia ambazo zilipanga hizo
GNI by Atlas Method, wakaja na hizi data...
View attachment 2443850
Kupitia data hizo hapo juu, hiyo mishale MITANO kutokea KUSHOTO inawakilisha mwaka 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, na 2020, pamoja na Viwango vyake vya GNI.
Na ukisoma Data, utaona mwaka 1995, GNI ilikuwa USD 170 na mwaka 2000 GNI ilikuwa USD 410.
Kwa maana nyingine, katika miaka 5 yake ya kwanza, Mzee Mkapa aliweza kupandisha GNI from USD 170 to USD 410; yaani kwa alipandisha kwa USD 240.
Aidha, data hizo zinaonesha mwaka 2005 GNI ilikuwa USD 500 na mwaka 2010 GNI ilikuwa USD 720.
Kwa maana nyingine, Mzee wa Msoga aliweza kupandisha GNI kutoka USD 500 ambayo aliikuta hadi USD 720... yaani kwa USD 220.
Hali kadhalika, takwimu hizo zinaonesha mwaka 2015 GNI ilikuwa USD 980 na mwaka 2020 ilikuwa 1080.
Kwa maana nyingine, JPM aliipandisha GNI kutoka USD 980 aliyokuwa ameikuta hadi USD 1080, yaani aliipandisha kwa USD 100.
Kwa maana nyingine, wakati katika miaka yake mitano ya kwanza Mkapa alipandisha GNI kwa 240, na JK kwa USD 220, na JPM kwa USD 100 lakini leo hii mnataka kutuambia "JPM was Tanzanian Knight!!
Takwimu zinaonesha kinyume chake, na ndo maana mnakuwa wakali kama pilipili mkiambiwa ukweli!! Hamna hoja ya maana mtakayotoa zaidi ya "UNA CHUKI NA JPM" na wengine hoja hiyo itafuatia na mitusi juu!!
JADILINI HOJA....