Hatua Nne za Kimkataba Uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

HATUA NNE (04) ZA KIMKATABA UWEKEZAJI BANDARI YA DAR ES SALAAM

1. Makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai - Makubaliano tayari yamesainiwa na kupitishwa na Bunge la Tanzania kwa lengo la kuweka Msingi wa Makubaliano baina ya nchi ili kuwezesha kuingia kwenye majadiliano ya kuingia kwenye Mikataba mbalimbali ya uwekezaji na uendeshaji wa maeneo ya Bandari nchini

2. Mkataba wa Nchi mwenyeji bado haujasainiwa. Lengo ni kuonyesha
  • Aina na Mfumo
  • Utaratibu wa kikodi
  • Namna Tanzania itanufaika na uwekezaji au itapata faida

3. Mikataba ya Miradi bado haijasainiwa. Mamlaka ya Bandari Tanzania ndiyo Mamlaka ya pekee Tanzania yenye Mamlaka kisheria inayoruhusiwa kuendesha Bandari. Lengo ni kuhusisha:
  • Mkataba wa upangishaji
  • Vipimo vya eneo analopewa mwekezaji
  • Gharama ya Malipo

4. Mkataba wa Uendeshaji. Mkataba utaainisha Malipo ya tozo mbalimbali zitakazolipwa na Mwekezaji Serikalini wakati wote anapokuwa anatoa huduma
- Malipo ya tozo mbalimbali, mfano; Tozo kwa kila Kontena. Gharama ya Malipo ushuru wa forodha (TPA)

Serikali inaweka mbele maslahi na usalama wa Nchi na kuhakikisha Watanzania wananufaika kupitia uwekezaji wa kimkakati.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-07-10 at 09.57.38.mp4
    2.8 MB
Wale wale
IMG-20230708-WA0007.jpg
 
Back
Top Bottom