Na kweli hamna mwanacdm mwenye akili ndogo, ndio maana Lowassa aliletwa na kupewa nafasi adhimu ya kugombea urais huku akiwa hawezi hata kusalimia kwa salamu ya chama, na kisha kayakosa hayo madaraka karudi alipotoka na hamuwezi kuchukua hatua kwa ujinga huo.
Pitia post zangu kama kuna popote nilipowahi kuungana na ccm kutaka muda wa Mbowe atoke madarakani. Kumbuka ccm hawakuanza kuona Mbowe atoke sasa, hayo ni madai yao ya muda mrefu, mimi madai yangu ni ya sasa na nina sababu za msingi. Usitake kuchanganya madai yangu na matakwa ya ccm ili ionekane kama mimi ni bendera fuata upepo. Ninajitambua boss na nina matakwa ya msingi. Ondoa maslahi binafsi, jali ukuaji wa taasisi na sio mlo wako.