Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA

Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA

Mimi nasoma comments nabaki nacheka kwa wanaodai kwa bidii kubwa Mbowe atoke si wanachama wa Chadema! Kwa nini wasiwaachie Chadema wenyewe wapige hiyo kelele?
Kwa kweli ni kicheko kikubwa sana.Siku wanachama watakapoamua kuchagua Mwenyekiti mwingine watafanya tu na wala hawatasubiri kuambiwa na wanaCCM
 
Tatizo la wafuasi wa Mbowe wana ubongo wa sisimizi
Kuwaita wale wanaohoji uenyekiti wa mbowe kuwa ni mapandikizi ni kinyume na demokrasia
Chadema wao kuihoji serikali kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza,hawana tabu,ila wao hawataki kabisa kuguswa
 
Mbowe alikuwa na nguvu na uwezo kwa sababu ya Dr Slaa tu. Sasa hivi ana lolote, hana uwezo kwa sababu king maker aliondoka
Na demokrasia lazima ionekane ndani ya chama, otherwise hakuna sababu ya kulalamikia ccm na serikali yake
Sasa wewe kinakuuma nini wanachadema wakichagua mtu asiyefaa kama unavyodai?
 
Tatizo la wafuasi wa Mbowe wana ubongo wa sisimizi
Kuwaita wale wanaohoji uenyekiti wa mbowe kuwa ni mapandikizi ni kinyume na demokrasia
Chadema wao kuihoji serikali kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza,hawana tabu,ila wao hawataki kabisa kuguswa
Tatizo uwezo wenu ni mdogo mno wa kuchambua mambo.Kulinganisha Mbowe na Serikali ni vitu viwili tofauti sana.Nenda shule kidogo ujue tofauti ya haya mambo
 
Mkono wa Mh. Mbowe umeshatema cheche ngoja waje wapiga mapambio wake sasa.

DEMOKRASIA KWA TZ NI NGUMU HAIJARISHI CCM AU UPINZANI.

Nyie watu wa kusini mna akili nyingi sana zakuwashika wajinga jinga.
Mkono wa Mbowe ni upi huo?
 
Wakati Freeman Aikaeli Mbowe⁩ anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.

Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)

Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!

Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'

Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!

Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"

Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half!

Stay blessed Chairman!

Mbowe Tano Tena Uchaguzi Mkuu 2019
The bottomline ni kuwa Mbowe haondoki CDM uenyekiti katika utawala wa Jiwe! Katika udikiteita wa Jiwe na kufa kwa demokrasia, hakuna kuondoka. Ingelikuwa kipindi cha "amani" tuliyoizoea, people could think of that, but not now!
 
Mbowe hakika anafaa kuendelea ila katibu mkuu wake hapana kapoa sana kama maji ya mtungi katibu awe John Mnyika
 
Yaani ndo maana Mimi nashangazwa na demokrasia ndani ya chama nilichofikiri in mbadala mzuri.
Tayari mna mgombea wa urais?
Je mtawanyima wengine nafasi ya kujaribu nafasi hiyo kwa kuwa tayari MNA mgombea?
Naamini ni mawazo yako na sio ya chama.
Halafu pia hakuna ubaya Lissu akigombea uenyekiti na baadaye akagombea urais.
Mbowe aondoke kwa heshima maana ameshatumika vya kutosha.
Aruhusu makamanda wapya na wenye fikra mpya ndani ya uongozi wa chama.
Hivi kuna kitu gani huko kwenye uenyekiti ambacho hamtaki kukiachia ninyi team Mbowe?
Ninaanza kuwaza kuwa kuna kundi dogo linalofaidika na huu uenyekiti wa Mbowe na ndo wanamlazimisha kugombea.
Vijana kama mnakula haramu itawapitia puani
Labda nikuibie siri na iwe siri yako Tu.Lissu ndiye mgombea wetu wa Urais na Mbowe ndiye Mwenyekiti wetu.Tunataka mgawanyo wa madaraka ndani ya chama chetu
 
Asipogombea wataongezeka?
Wanaweza wasiongezeke lakini team Mbowe wamekuwa wakitumia ongezeko LA idadi ya wenyeti wa vitongoji,mitaa/vijiji,madiwani,wabunge kama fimbo kwa wagombea wengine.
Ninachoamini ni kuwa kweli kulikuwa na ongezeko lakini mwakani uchaguzi ukifanyika watapungua mno kama sio kwisha kabisa.
Sasa najiuliza kampeni ya timu Mbowe kwa wagombea wengine itakuwaje?
Turuhusu demokrasia ifanye kazi.
 
Mbowe hakika anafaa kuendelea ila katibu mkuu wake hapana kapoa sana kama maji ya mtungi katibu awe John Mnyika
Hili linazungumzika mkuu.Tunaweza kumshauri Mwenyekiti vizuri wakati atakapofanya uteuzi wa Katibu mkuu mpya.Naamini ataheshimu mawazo ya wengi
 
Wanaweza wasiongezeke lakini team Mbowe wamekuwa wakitumia ongezeko LA idadi ya wenyeti wa vitongoji,mitaa/vijiji,madiwani,wabunge kama fimbo kwa wagombea wengine.
Ninachoamini ni kuwa kweli kulikuwa na ongezeko lakini mwakani uchaguzi ukifanyika watapungua mno kama sio kwisha kabisa.
Sasa najiuliza kampeni ya timu Mbowe kwa wagombea wengine itakuwaje?
Turuhusu demokrasia ifanye kazi.
CDM siyo sawa na CCM.Huku hakuna Team Mbowe.Huku kuna Team CDM
 
Kwani kwa uenyekiti wake amemfanya nn jiwe?
The bottomline ni kuwa Mbowe haondoki CDM uenyekiti katika utawala wa Jiwe! Katika udikiteita wa Jiwe na kufa kwa demokrasia, hakuna kuondoka. Ingelikuwa kipindi cha "amani" tuliyoizoea, people could think of that, but not now!
 
Hili linazungumzika mkuu.Tunaweza kumshauri Mwenyekiti vizuri wakati atakapofanya uteuzi wa Katibu mkuu mpya.Naamini ataheshimu mawazo ya wengi
Huna tofauti na wale Praise Team pale Lumumba.

Huna tofauti na Musiba au Juma Nkamia.
 
Back
Top Bottom