Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA

Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA

Wakati Freeman Aikaeli Mbowe⁩ anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.

Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)

Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!

Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'

Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!

Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"

Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half!

Stay blessed Chairman!

Mbowe Tano Tena Uchaguzi Mkuu 2019
Umeamua kujipigia debe ww mwenyewe!!
 
No matter how good one is, ukifikia point ya saturation unakuwa a saturated solution, you can take no more than you can.

One can be very good and very instrumental ukafanya a lot of good things, lakini akifikia optimum ya uwezo wako, you can do no more good than you did.

Waasisi wa Chadema walioweka kipengele cha ukomo wa uongozi ni vipindi viwili vya miaka 5 mitano, ndani ya katiba ya Chadema, walikuwa na maana yao nzuri tuu, lakini jinsi kipengele hicho kilivyo yeyuka into thin air kwa kunyofolewa kinyemela, leaves much to be desired.

Na ukiizungumzia tuu hoja ya ukomo, wanakushukia kama mwewe!.

P
Hakuna mtakatifu
Kukosolewa na kukujenga
Upinzani wanapitia magumu lakini wamejisahau sana
Ni vyema kuwa muwazi
Wekeni mapato na matumizi wazi
Mkikosoa kubalini kukosolewa haina maana mmeshindwa
Onyesheni mfano kwa lile mnalihubiri
Haya ni mapigo na mapito yapashwa kutokea kuwaamsha kidogo
Kuna baadhi ya wabunge wa upinzani wapo kimya
Mnalipwa mishahara na pesa za kujikimu kwa kodi za wananchi fanyeni kazi ' Uthubutu uko wapi?'
Mnaposema wananchi hawawaungi mkono mnakosea wananchi hawalipwi kufanya kazi ya Ubunge ninyi mnalipwa ' Mliaapa kujitoa muhanga'

* Swala la Mbowe nadhani ndani ya Chama ndio mwenye uthubutu wengi waoga ndio maana wanaona sawa aendelee' Demokrasia mnayoihubiri itekelezeni kwa vitendo
Mbowe itisha mkutano as soon as possible reshuffle inahitajika unaweza kuwa Katibu Mwenezi Selasini Mwenyekiti wengine utawapangua then mtakuwa imara 2020 vinginevyo safari itakuwa ngumu. Lissu akipewa Ukatibu mtakijenga chama then 2025 tukutane magogoni'
Punguzeni kuongea na vyombo vya habari kila kukicha fanyeni kazi
My opinion
Sina chama

Oops pole Mkuu nikuvamia
 
Pakawa kuna hoja nyingine ni za Kihistoria na nyingine ni hisia tu za watu. Kwanza si kweli kwamba Mbowe ni lazima awepo madarakani ili CHADEMA iwepo lakini ni ukweli kwamba kwa CHADEMA Mbowe bado ni kiongozi Imara na shupavu.

Sijui ni nani anayeleta hoja kwamba kuwepo kwa Mbowe kwenye uenyekiti ni kiashiria kwamba CHADEMA inadhoofu ama itashindwa kwenye uchaguzi wa mwakani.

Kwangu mimi uimara wa Mbowe naupima kwa mashambulizi yanayofanywa na CCM kwa kutumia vyombo vya dola dhidi ya CHADEMA. Kama Mbowe si imara kwa hakika kabisa CHADEMA isingekuwa hapa ilipo na wala isingekua hivi ilivyo.

Sielewi ni kwa nini kuna watu mnaona kama vile CHADEMA haipendi kukosolewa. Tofautisheni kukosolewa na kusingiziwa. Ukisingiziwa na wewe ukakaa kimya huo ni udhaifu. Kwa nini mnataka kila baya linalosemwa dhidi ya CHADEMA liwe ni kweli?

Kulipwa mishahara kwa kodi za wananchi hakuhalalishi kujitoa mhanga. Hao wanaopora haki za walioko CHADEMA hawalipwi mishahara kwa kodi za wananchi? Kwa nini msipaze sauti kusema waache kupora haki za CHADEMA kwa kuwa wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi?

CHADEMA wanaonya, wanatoa sera mbadala, wanajenga chama chao, wanakosoa na kuonesha makosa ya CCM jinsi inavyoendesha serikali ulitaka wafanye nini tena? Wananchi wao wenyewe wanapigania haki zao zinazotajwa na CHADEMA kama zinavunjwa na CCM kwa jinsi inavyoendesha serikali?
 
Mkuu sipingani na wewe wala sijasema kama yanayozungumzwa kwenye mitandao ni kweli au si kweli.
Ni kweli Mbowe amekijenga Chama na anastahili pongezi
Ndio maana nikasema katika Chama Mbowe ndio mwenye Uthubutu
Pia nimesema Kukosolewa haina maana ni dhaifu ni Kuwajenga zaidi lakini kwa kujibu tuhuma zilizopo kuepusha sintofahamu
Kama ni matumizi au Mapato yawe wazi.

Mkuu nikupe mfano wa mfanyakazi wa Tanesco Yule wa kurekebisha mitambo nyaya etc Aliomba kazi akijua kuna hatari au ajali kazini (wengi huwa wanapoteza maisha lakini haina maana waliobaki nyuma wataacha kazi watasonga kutimiza malengo)
Kuhusiana na Wabunge wetu wa vyama vyote wanapashwa kuwa Kama mfanyakazi wa Tanesco wanalipwa kwa kodi za Wananchi watimize malengo (kuwafanyia kazi wananchi hata ikibidi kujitoa muhanga)
 
CDM ina Ruzuku, Hujasikia watu wakilalamima kuwa 1.2b imepigwa. hukumbuki Ripoti ya C.A.G. endelea kujitolea Bob!
Kuna shida ya watu kuingilia taaluma, ripoti inaposema ni hati chafu au ya mashaka haimaanishi kuna wizi ila mfano una mali kama magari au Majengo hujayathaminisha hivyo hujui value yake huo nao unarekodiwa ni ufisadi!! Hivyo utapewa hati ya mashaka/chafu. Hayo mambo yapo kiuhasibu zaidi sio necessarily wizi uwepo bali sheria za kiuhasibu/Ukaguzi zifuatwe.

Ila trust me kungekua na wizi kweli CHADEMA wa kiasi hiko kwa jinsi wanavyokitafutia makosa kingeshakuwa kimefutwa au kina mbowe kuburuzwa kortini kwa kesi ya uhujumu uchumi ila kwanini wanaangaliwa tu muda wote then wanapewa vikesi vya kitoto kama Uchochezi na wanaachwa na kesi kubwa kama hizi ambazo zina ushahidi wa ripoti ya CAG??

Ina maana CCM hawajui??
 
Mkuu Zitto jnr, kwanza asante for much respect.
Utungaji katiba is a process, kila kilichokuwepo kwenye katiba ya mwanzo, kilikuwepo kwa sababu, unapotunga katiba mpya, kila kitakacho ondolewa lazima kijadiliwe with minutes written down.

Katika huo utunzi wa katiba mpya hakuna minutes zozote kuhusu kipengele hicho, as if it's an oversight, kwa taarifa kipengele hicho ni moja ya misingi mikuu kwa Chadema kuitwa Chama cha Demokrasia, how can katiba ya Chadema iwe silent?.
P
Unajua pascal unanishangaza sana ni lini ukomo wa madaraka ni indicator ya demokrasia per se?? Russia na Uturuki kulikuwa na ukomo wa madaraka ila umeona watawala walivyouchezea huo mfumo hadi wanabadilisha majina ya vyeo ili waendelee kutawala!!

Putin alikua Rais alipoona ukomo umefika akajipachika uwaziri mkuu ili aendelee kuitawala nchi na kuweka Rais kivuli!!! Hata Erdogan wa Uturuki aliacha uwaziri mkuu akaenda kuwa Rais huku akihamisha mamlaka zote za waziri mkuu kwa Rais!! Hao wana term limits mnaopigania CHADEMA waweke lakini je kuna demokrasia??

Mbowe hajakalia kiti kimabavu, licha ya kuwa hakuna term limits ila kuna uchaguzi wa kitaifa kila baada ya miaka 5 sasa kama wanachama wanaona hafai si anakatwa au usipokua na ukomo huwezi angushwa kwa kura??

CCM (kwa mfano tu sio kulinganisha) ukomo unaweza kuwa by default kila baada ya miaka 5 ila Je umewahi ona nafasi hyo inagombewa?? Zaidi mtu akiwa Rais anapita bila kupingwa sasa hyo ndio demokrasia unayoongelea kwa basing on term limits?? Kenya kuna demokrasia kisa term limits??

Mimi nadhani demokrasia ni suala complex mfano namna kiongozi anavyoingia madarakani ama kudhibitiwa na taasisi husika ila sio exclusively term limits ndio hoja ya kuprove hakuna demokrasia hapo ndio mnaoshinikiza hoja hii mnaponitatiza.

Wewe kama msomi najua fika unafahamu multiple regression analysis inavyofanya kazi kwenye tafiti basi naomba unisaidie je katika ukomo wa madaraka,uchaguzi huru na haki wa ndani,kuwajibikwa kwa watu waliokuchagua NA kiongozi kufuata sheria zilizowekwa na vyombo husika ipi ndio indicator nzuri zaidi ya demokrasia??

Na kama ni ukomo kwanini ndio more related to democracy kuliko zile variable tatu zingine nlizotaja

Karibu mkuu
 
zitto junior tatizo la kina Pascal Mayalla wao kila kinachosemwa na CCM hukikariri kama ni andiko takatifu (Dogma). Ukomo wa muda wa uongozi ni jambo zuri lakini si kigezo cha kuonesha kwamba taasisi ina Demokrasia.

Kwa Afrika ukomo wa muda kwenye Urais umewekwa kwa kuwa uzowefu unaonesha kwamba viongozi wa Afrika huwa hawataki kuondoka madarakani kwa visingizio mbali mbali lakini huku wakikandamiza wapinzani wao kwa kutumia vyombo vya dola na kuwagawa watu wao kwa misingi ya Dini, Kabila, Eneo au Itikadi zao.

Wakati wanang'ang'ania kwamba CHADEMA kuna ukomo wa muda wa uongozi hawasemi kwamba kwenye CCM kuna nini? Juzi tumewahoji ni kwa nini kama wanasema chama chao mtu hatakiwi awe na kofia mbili ni kwa nini Mwenyekiti wao taifa ana kofia mbili, wako kimya mpa leo.

Mbowe siyo Mungu wa CHADEMA iko siku ATATOKA madarakani, lakini hatatoka kwa kuwa tu CCM wanasema ATOKE.
 
Mkuu Pascal Mayalla huwa unaheshimika sana hapa jukwaani na muda mwingine huwa unaongea kwa mafumbo lakini hapa Sidhani kama unaongea kwa parables maana upo clear kuwa CHADEMA imefuta kipengele cha uongozi.

Hili swali aliwahi uliza Nape humu jukwaani na akajibiwa na Dr slaa pamoja na JJ Mnyika kwa hoja na nyaraka kwamba kipengele cha ukomo hakikufutwa ila katika kusaka maoni ya kutunga katiba mpya chini ya Prof Baregu suala hilo halikuwekwa na wanachama.

HIVYO BASI unapojenga hoja kuhusu suala hili usiseme kilinyofolewa bali sema katiba mpya haijazungumzia. Maana mtu anaweza dhani ilifanyiwa amendment ikafuta hiko kipengele.

Pascal upo credible so una uwezo wa kutengeneza au kuharibu so kabla hujachangia lolote keep your facts straight!!

Ni hayo tu mkuu wangu
Mkuu samahani unaposema hakikujadiliwa kwenye katiba pendekezwa au Mpya si n sawa na kunyofolewa?
SA hivi CHADEMA wanatumia katiba ipi?
Hiyo yenye kipengele cha ukomo au ambayo haina kipengele cha ukomo?
Kama ni hiyo yenye kipengele cha ukomo, je Mh. mwenyekiti ametimiza ukomo kikatiba ? Kama ni nyingine je ataendelea hadi lini?
Natumai utanielekeza vizuri hapo.
 
Mwana Taluma mwenzangu kwanza nianze kwa Kukusalimia habari za siku, sikuweza kuwepo jukwani kutokana Na masomo yanayonikabili,

Kwanza nianze kwa kukukumbusha Freeman Mbowe ataondoka pindi wanachama wakisema aondoke si kwa shinikizo kutoka kwa wanaoitakia chadema mabaya pili mbowe amekitoa chadema sehemu ambayo ccm hawakutegemea kuwa leo chadema kitafika kwahiyo freeman mbowe ndio chaguo la wana chadema na Watanzania kwa ujumla

Wasalam
Kwani ukomo wa uongozi kwa CHADEMA ni miaka mingapi?
Je kiongozi akiongeza zaidi inatafsiriwaje?
 
KAMA MBOWE KAFANYA VIZURI NDIO WAJIBU WAKE NA TUNAMSHUKURU SANA LAKINI SIO TIKETI YA KUTOWAPISHA WENGINE
 
Mkuu samahani unaposema hakikujadiliwa kwenye katiba pendekezwa au Mpya si n sawa na kunyofolewa?
SA hivi CHADEMA wanatumia katiba ipi?
Hiyo yenye kipengele cha ukomo au ambayo haina kipengele cha ukomo?
Kama ni hiyo yenye kipengele cha ukomo, je Mh. mwenyekiti ametimiza ukomo kikatiba ? Kama ni nyingine je ataendelea hadi lini?
Natumai utanielekeza vizuri hapo.
1. Mkuu katiba mpya inavyoandikwa ni kusaka maoni upya kabisa, mnakuja na framework mpya kabisa hivyo huwa vipengele vingi sana vipya vinakuja na vingi vya zamani kuondoka. Yaani mfano katiba ya warioba ilikuja na vitu vipya kabisa mfano muundo wa serikali tatu ambayo yalikuwa maaoni ya wananchi sasa kivipi mtu atokee aseme warioba alifuta serikali mbili??? Ilihali alianza kitu kipya kabisaa kwa maoni na mchakato na mfumo mpya. Kwahiyo ni kweli kipengele hicho hakipo kama ambavyo vipengele zaidi ya 100 havipo na vingine zaidi ya 100 vimeongezwa sasa sielewi kwanini hoja ijengewe kwenye kipengele cha ukomo tu na sio vingine?? Na hiyo kamati iliongozwa na Prof Baregu na katibu wake mnyika sasa kivipi tena atajwe mbowe ambaye alikua hana mizizi CHADEMA enzi hizo??

2. Sahivi wanatumia katiba iliyoanza 2006 ambayo haina kipengele cha ukomo cha nafasi ya uenyekiti sababu haikuwemo kwenye maoni ya wanachama kwenye kuandika katiba mpya.

3. Jaman ukomo upo ni kila baada ya miaka mitano uenyekiti unaisha na lazima uchaguzi ufanyike ili uweze kuwa mwenyekiti, tofauti tu ni kwamba Kutokuwepo ukomo wa mihula haimaanishi utawale milele bila iliwekwa ili kutoa fursa ikitokea mtu bado anauwezo kuendelea kuongoza basi anaweza chaguliwa na wanachama kuendelea kuongoza kwa kipindi kingine.

Mbowe kwa minajili hiyo ukomo wa uenyekiti ni mwaka huu na kama atataka kuwa mwenyekiti tena ni lazima wanachama wakubali,wampitishe na agombee na ashinde uchaguzi ambapo ndio demokrasia inapofuatwa hapo na inapopimwa.

Kasome misingi 11 ya demokrasia uone kama ukomo ni mmojawapo alafu urudi hapa kuujengea hoja. Ila CCM wao wana ''ukomo'' wa uenyekiti kila miaka 10 ila je umewahi ona uchaguzi wa mwenyekiti unafanyika kwa watu kuchukua fomu na kugombea?? Je hapo kuna demokrasia licha ya kuwa kuna "ukomo" wa mihula ya kuwa mwenyekiti wao??

Ni hayo tu
 
Wakati Freeman Aikaeli Mbowe⁩ anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.

Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)

Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!

Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'

Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!

Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"

Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half!

Stay blessed Chairman!

Mbowe Tano Tena Uchaguzi Mkuu 2019

Kila kwenye neno chadema weka..Tanzania
kila kwenye neno mbowe weka CCM

wachawi ni sisi
 
Back
Top Bottom