Hatimaye wazee wadai Mustapha Mkullo si mtanzania

malawi hakuna mtu anyeitwa mustapha,majina kama hayo utayakuta libya,somali au kidogo pemba lol
 
sasa wamempitisha anagombea kwenye jimbo lake kupitia sisiem
ingawa yeye kweli sio raia kama wazee wametoswa walikuwa wana
taka kumuharibia thru majungu tu tanzania ni nchi ya kipekee una
weza kuwa kiongozi wakati wewe sio raia.


Hii mbinu si mpya. Hao wazee wamejifunza kutoka CCM. Ni viongozi wangapi wa CCM waliowahi kuitumiikia nchi katika nafasi mbali mbali na kwa miaka lakini baadaye wakaambiwa si Watanzania?, wengine hata kubidi kuomba uraia upya? Nchi ina madudu hii!!!
 

we ni muongo wa kwanza duniani. Ungerelate Somalia tungechangia maana historia ya Babu wa mwalimu iko clear!
 
Siku utasikia Ridhiwani si mtz
 
Nimesoma habari hii kwenye Nipashe. Wazee wa huko kwake Morogogoro wamemwandikia JK barua kudai Mkulo ni Mmalawi .Wana JF hii kweli.?

mtu wakupewa lawama ni Jk Nyerere yeye ndie aliyewapa wageni vyeo ktk nchi hii,kikwete kawakuta wameshaingia kwenye system afanyeje?
 
Hivi nchi hii ndo imeoza ivi! Hata jk nyerere walisema sio mtz, mkapa walisema sio mtz,jenerali ulimwengu wakasema sio mtz,bashe wakasema sio mtz, mkullo sio mtz!!! TUTIMUE VIONGOZ WOTE NINI?? INAWEZEKANA HATA MIJITU YA RITA SIO MITANZANIA! INAPEANA BIRTH CERT KAMA LAMBALAMBA!
 
Jamani mkitaka kuchambua kuhusu uraia inawezekana wengi wetu hatuna asili ya Tanzania......
 
Asilimia zaidi ya 90 ya viongozi wa nchi hii kuanzia boss wao mkuu pale juu wana vyeti feki. Kuna haja ya kuweka mfumo wa kuhakiki elimu za wananchi wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi.
 
Ulimi ni kiungo kidogo sana ila unaweza sababisha maafa kweli. Hivi haya yote yamekuja baada ya kutamka tutakula jasho letu!! asingesema wala kusingekuwa natatizo.

jamani tuombe Mungu, amani iendelee kuwepo.
 

Si kweli, Sitta ni jina la wasukuma na wanyamwezi. Ninachojua, mkewe Samweli ndio mwenye asili ya Malawi huko, surname yake ni Simwanza!
 
Nimesoma habari hii kwenye Nipashe. Wazee wa huko kwake Morogogoro wamemwandikia JK barua kudai Mkulo ni Mmalawi .Wana JF hii kweli.?

Sio kama wana hoja yenye mashiko,kwa hiyo hata Obama kwa kua baba yake alikua ni Mkenya basi nae hakustahili kua rais wa America?sioni kama hiyo kitu ina tija!
 
Hapo sina Hoja, kwa sababu hakuna DNA ya uraia nani anaweza thibitisha. Ila nijuacho kwa maslahi ya watawala , wanapenda viongozi waandamizi wao wawe na utata hasa kwenye masuala ya uraia au kesi za mauaji na Uhaini ili watumie udhaifu huo Kama remote control kwa wasaidizi wao Hao.
 
Hata Abdallah Shaweji ambaye alikuwa mbunge wa huko Kilosa kabla ya Mkullo pia hakuwa raia. Huyu naye alikuja na wazazi wake katika mashamba ya mkonge na baadaye akapanda vyeo hadi kuwa meneja mkuu wa shamba la mkonge pale kimamba-kilosa ambapo pia mkullo anatokea maeneo hayo ya kimamba.

Lakini kwa Kilosa sishangai, kuna mtu anaitwa Omari Abdallah Makumulo naye alishawahi kuwa mbunge miaka ya 80 hadi 90. Kabla ya hapo alikuwa mchumi mkuu mwandamizi wa shirika la posta na simu, huyu naye ilisemekana kuwa hakuwa raia. lilipigwa zengwe hadi akawekwa kando na nafasi yake akachukua bw. Shaweji.
 
Kwa hali hii, Tz hata ipite miaka elfu kumi hatutapata maendeleo. Badala ya kujadili maendeleo mnajadili uraia wa mtu.
 
Sio kama wana hoja yenye mashiko,kwa hiyo hata Obama kwa kua baba yake alikua ni Mkenya basi nae hakustahili kua rais wa America?sioni kama hiyo kitu ina tija!

wamarekani karibu wote sio wenye nchi kwa mtazamo huu,wenyewe ni wahindi wekundu!
 
Umezungumzia ukabila,hoja ni UTAIFA,wewe vp?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…