Hatimaye wazee wadai Mustapha Mkullo si mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye wazee wadai Mustapha Mkullo si mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mfamaji, Aug 13, 2010.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nimesoma habari hii kwenye Nipashe. Wazee wa huko kwake Morogogoro wamemwandikia JK barua kudai Mkulo ni Mmalawi .Wana JF hii kweli.?
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mods . Please sikuwahi kufahamu kuwa ukikosea heading huwezi kuedit . Please the names should be in CAPITAL Letters. Sorry.
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huu sasa ni udako unatoa taarifa halafu unaulizia ukweli wa taarifa sasa tukueleweje?
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukisikia siasa za rafu ndizo hizo. Yaani amekuwa mbunge wao kwa kitambo sasa wanasema si raia. On top, alishiriki sana kuwasaidia wakati wa ile sunami yao halafu leo rushwa inaona si raia. Sasa kama ni rafu ni vema mtu kuchagua rafu isiyo na aibu. Mwaka huu ma-editor watupashao habari watatuletea mengi ya ajabu! Lo, nimesahau huu ni wakati wa mavuno! Nani huyo kanunua hii habari? Nilisikia katika uchambuzi wa habari asubuhi nikacheka sana.

   
 5. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Habari mchanganyiko!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mfamaji,
  Sasa kama ana asili ya Malawi kuna tatizo gani?
  Mkuu wangu hizi ni tuhuma za watu waliolewa mawazo ya bara ambao zamani tulikuwa tukiwaita Washamba. Ushamba ni pamoja na kutooona watu wa makabila mengine wakichanganyikana nanyi.. Hivyo kujichanganya kwao kumeletwa na Nyerere wakati huko pwani watu wa makabila walikuwepo karne na karne kabla hata ya kufikiria huo Uhuru.

  Pili, Huwezi kuzungumzia asili wa mtu kama ndio Uraia wa mhusika. Kabila na Uraia, Vitu hivi havifanani na inaonyesha tena kwamba tunahitaji sana elimu ya Uraia kwani tunarudi katika Makabila kuzungumzia Uraia wa mtu. Na hakika tukifuata hivyo nchi zote duniani zitaingia ktk vita mpya ya Ukabila.
   
 7. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tuna mpaka Wa-Iran sembuse wamalawi
   
 8. M

  Msharika JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na kushgangaza zaid leo Kamati kuu ya CCM ambayo imempa kada wake maarufu Bashe vyeo lukuki imemkana kuwa sio mtanzania. Hivyo ushindi wake wa kura za maoni unatenguliwa. Si wamkamate kwa kukaa nchini kwa kosa la uhamiaji haramu?
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Akiwa Mmalawi so what!!!
  Mtikila vile vile alisema Mkapa kwao Msumbiji.Kumbuka hata Karume, kwao Malawi.
  Nyerere kwao Hima empire, Rwanda huko.
  Hata wewe ulinukuu huu habari miaka ya 1600 huko babu zako hawakuwa hapa.
   
 10. e

  echonza Senior Member

  #10
  Aug 15, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa habari hii ni kama kutuletea udini, ukabila na ubaguzi wa rangi vile. Ni kweli, tunahitaji kuendesha sana mafundisho ya elimu ya uraia kwa wananchi wetu. Ama, kama siyo hivyo, basi humo humo ndani ya thithiem kuna mtu aliyekwenda kuwaambia hao wazee waseme hayo maneno, si unajua tena maisha ya fitina yalivyo?
   
 11. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #11
  Aug 15, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Nadhani unaufahamu ule usemi wa "kufa kufaana..."

  Mkullo ni mwanasiasa, na kila mwanasiasa hutaka kuonekana kwamba anawajibika kwa waliomchagua, hata kama ni kinyume cha ukweli.

  Suala la mafuriko yaliyowakumba wakazi wa Kilosa ni suala la kitaifa. Misaada ilikuwa inatolewa kwa hiari, Mkullo hakuhusika kuitafuta. Usimpe sifa ambazo hastahili. Alionekana wakati wa kupokea, lakini wakati wa kugawa misaada hatujui. Kuonekana kwake wakati huo ni jambo linaloitwa "photo opportunity". Picha zinapigwa, zinatolewa kwenye magazeti na luninga, anaonekana anajali.

  Wakazi wa Kilosa wanamkumbuka sana Mkullo. Aliwahamasisha kujiunga na DECI, matatizo yalipotokea hata kwenda kuwafariji hakufika. Walimshangaa aliposema kwamba DECI ni utapeli. Itakuwaje utapeli wakati yeye ndiye alisimama jukwaani kuwashawishi kujiunga nayo? Au naye alishiriki kwenye utapeli huo?

  Cha kuambiwa, weka na chako pia...

  ./Mwana wa Haki
   
 12. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mwaka wa siasa !
   
 13. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sasa wamempitisha anagombea kwenye jimbo lake kupitia sisiem
  ingawa yeye kweli sio raia kama wazee wametoswa walikuwa wana
  taka kumuharibia thru majungu tu tanzania ni nchi ya kipekee una
  weza kuwa kiongozi wakati wewe sio raia.
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Tunaweza kuuliza swali kama hilo hilo. Hussein Bashe ni msomali so what!/ Jenerali Ulimwengu ni mtusi, so? Umeona yaliyotokea?

  Kweli Mkapa ni mtu wa Msumbji na JK ni mtanzania, so what!

  Ukiangalia kwa undani utajua kuwa huu ni ujinga na ujanja wa kisiasa, kupika majungu kupakua na kuwavuruga watu.
   
 15. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa details nilizo zisikia mahali inavyosemekani ni kweli ni Mmalawi bila ubishi na hakuna source ya chimbuko la wazazi wake. Sasa ndipo hapo napo iuliza CCM,USALAMA WA TAIFA na SERIKALI YAKE, BILA SAHAU VITENGO VYA IKULU VYA PROTOKALI wao kazi zao ni nini ndani ya nchi hii kuibeba CCM na upuuzi wote unaofanyika na wanaoufanya ndani ya serikali kwani wao ndio chama tawala na haya yote yanatokea chini ya uongozi wao, Usio makini wanatufundisha nini? na wao ndio chanzo cha kuvuruga amani nawambieni mtakuja niambia subirini

   
 16. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...malaria sugu, any comment?
   
 17. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Are you saying that Mkulo was NSSF CEO as an Expatriate (TX)?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  duh.. bado tuna kazi; mtu anaweza kuwa "ana asili ya Marekani" na akawa Raia wa Tanzania; au mtu akawa ana asili ya Kenya na akawa raia wa Tanzania. Uasili wa mtu hausemi uraia wake. Kwa sababu uraia ni suala la kisheria siyo suala la kabila, rangi, mipaka au kuonekana.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ni kama comedy

  nakumbuka mkurugenzi wa uhamiaji aliwahi fikishwa
  mahakamani kwa kuwa sio raia...

  Imagine mkurugenzi wa uhamiaji..........
   
 20. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #20
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashangaa leo watu wanashangaa kuwa MKULO si raia wa TANZANIA lakini tunashangaa nini wakati huyu hata hata chembe ya credibility. Nadhani huyu ndiye waziri wa fedha pekee duniani aliyesoma CHUO FEKI na kupata DEGREE FEKI (btw Chuo hicho kinatoa Degrees mpaka kwa MBWA) na leo hii ndiye anakaa kwenye wizara nyet ya Tanzania. Ukimkuta pale Wizarani anavyo wadharau na kuwaendesha puta Wa Tanzania ndio utakubali kuwa hapa tulipo tuko pabaya.

  Sasa kama mnataka kujua ukweli then:

  1. Nendeni Kilosa mkatafute ukoo wake kama mtaupata

  2. Muulizeni alete cheti chake cha kuzaliwa

  3. Muulizeni baba yake alitokea wapi kabla hajahamia kilosa

  4. Muulizeni baba yake alikuwa anafanya nini kabla ya kuhamia Kilosa

  5. Muulizeni baba yake alizaliwa wapi?

  6. Kama mlivyomuuliza kuhusu Baba yake, si vibaya mkamuuliza kuhusu Mama yake

  7. Muulizeni kwa nini wale Mabosi INCLUDING wale senior Govt officials ambao ni wa MALAWI wenzie kwa nini hawataki kumtetea kipindi hiki ambacho yuko kwenye majaribu wakati wanajulikana kwa kuwa OUTSPOKEN?

  7. Msiwalaumu USALAMA kwani file lipo na alishafanyiwa vetting ila si kazi yao kutoa kazi au kukamata kamata.
   
Loading...