Hatimaye wazee wadai Mustapha Mkullo si mtanzania

Watanzania wamekalia majungu tuu wakiona wenzao wanabunya mapesa,nanyi gombeeni kwani chadema hawatoi mapesa?
 
Nilipokuwa na soma gateti moja hii leo, nilipata kusoma swali kwamba je, kama alizaliwa Malawi na baadaye kuhamia hapa na wazazi wake, Je, ni lini Mkulo aliomba uraia wa Tanzania? Maana huko nyuma hata wazazi wake hadi wanalala, hawakuwahi kuomba uraia wa Tanzania. Na kibaya zaidi wazee wanaendelea kufafanua kwa kusema, kule uhamiaji, ambako aliomba hati ya kusafiria amekuwa akikumbushwa kupeleka nyaraka hizo muhimu lakini hajawahi kutekeleza. CCM waangalie kuwapa watu kama hawa mamlaka yenye kushikiria uchumi wa nchi wakati kuna utata na uraia wao. Je, walikuwa wanasubiri kuumbuka? Gazeti limeenda zaidi kwa kusema, wazee wa kilosa walienda hadi kijiji alichotaja alizaliwa kule Tunduru. Jibu lililorudi, hata jina la kijiji hicho hatuna Tanzania. Wako wapi J. Kikwete (aliyemteua na kumpa cheo kikubwa) kushughulikia suala hilo? Lakini sakata hili linanikumbusha EPA, zilipotoka taarifa za ufujaji huo wa fedha hata waziri wa fedha wa kipindi hicho mama Meghji alikana taarifa hizo kwa nguvu utafikiri alikuwa na kila taarifa mkononi mwake. Baada ya uchunguzi yakatoka madudu matupu.

Ni usanii mtupu katika serikali hii iliyoingia 2005, naomba wabadilike!
 
Friends of jk (friendsofjeykey) kazi mnayo si mumwambie tu huyo JK hamumtaki mkulo pale hazina tujue moja!!!!!
 
Majungu hayaendeshi nchi. Kama mgombea amekosa kura za kutosha
asubiri kipindi kingine njia ya mkato ni mbaya kwa uongozi.
 
Mmeishaanza kulana wenyewe. Hii sumu mliingiza kwa Jenerali sasa mtamgeukia kila mtu ambaye anatoka mikoa ya mipakani. Kama vile ilivyokuwa kwa Jenerali, huyu jamaa katumikia taifa lake muda wote huu ila sasa kwa vile mmemechoka ndiyo mnaleta upuuzi huu! Hao mnaowaita wahamiaji ndiyo waliosimama kidete na watanganyika wenzao kugombea uhuru wa nchi hii. Au mmesahau Katibu Mkuu wa kwanza, mzaliwa wa Kwambe, wa TANU alikuwa nani? . Au Dennis Phombeah? Au wakina Dr. Mtawali? Wote hawa na wengine walichangia na walikubalika katika taifa hili bila kujali kama waliongea kiswahili kwa lahfudhi ya kinyasa. Mnasahau kuwa kabla ya uhuru watu wengi tu walienda Nyasaland na Northern Rhodesi kusoma? mnasahau vilevile kuwa wapiganaji wengi walitoka huko kuja kusoma hapa? Katika mazingira yenu ya sasa yanayoendeshwa zaidi na chuki wazalendo kama wakina Amir Jamal, leader Stirling wsingekuwa na nafasi! Mnatia kichefu chefu na aibu.

Mwandameni Mkulo kwa mapungufu yake ( ambayo anayo mengi) lakini si hili la ukabila.

Amandla......
With due respect, yaani mtu ambaye si raia wa nchi hii, akifanya hayo uliyoyaorodhesha hapo juu kwa nchi hii, ndio automatically anakuwa raia? Ni bahati mbaya sana sababu zinazozua mambo haya ni sababu za chuki lakini haziondoi tafsiri ya sheria ya kuwa nani ni raia halali wa URT na asiye raia, afanye nini aupate uraia huo. Kama kuna tatizo na sheria, basi ibadilishwe na kuruhusu watu walioyafanyia makubwa taifa hili, kupata uraia moja kwa moja bila ya kuomba.
 
Mkulo alisoma Degree yake

Almeda University

From Wikipedia, the free encyclopedia


Almeda University (possibly also called Almeda College or Almeda College & University) is an unaccreditedAmerican institution that offers various academic degrees through distance education, including a "Life Experience Degree". Almeda was founded in 1997. Bears' Guide says that they could not locate the physical address of the institution and were told by reception that Almeda University is a "Web only" institution.

Elimu ya Msingi: Kumbukumbu zinaonyesha

Rudewa Primary School-1956-1960
Zombo Midle School-Primary 1961-1964
Mwaka 1965 alikwenda Pugu.

KWA VILE ALIKUWA ANAISHI TANGANYIKA WAKATI WA UHURU NA PIA ALIKUWA NCHINI WAKATI TANZANIA INAZALIWA MWAKA 1964. JE, SHERIA YA URAIA WA TANZANIA INASEMAJE KUHUSU URAIA WAKE?

aisee! Watu wa Kule kilosa haswa maeneo ya Zombo,kikonga,madudumizi na ulaya.wengi wao si wazaliwa wa Tz,wengi wametokea malawi na msumbiji.kuna mzee pale kikonga alinielezea kwamba alitokea msumbiji akajitwalia pori na kuji-establish.
Kwa hiyo hii inaweza kua error by default,tusimuhukumu peke yake.
Hapa ndipo umuhimu wa vitambulisho vya uraia na katiba mpya unapokuja.
 
Wana JamiiForum:

Huyu jamaa simfagilii. Lakini ukweli wa mambo ni mtanzania halisi kama watanzania wengine. Baba yake anayoasili ya Malawi lakini mama yake mzazi ni mtanzania.

Kilosa kuna watu waliokuja kufanya kazi na kuoa wanawake wa kiTanzania na kuanza maisha. Hivyo anazo haki zote kwa kupitia uraia wa mama yake.

Vilevile lazima mzisome sheria za kiraia ambazo zilitangaza uraia wa taifa huru la Tanganyika. Kuna wageni waliopewa uraia kwa sababu walikuwepo Tanganyika wakati nchi inapata uhuru.
 
Hii ya kufukuza watu au kutaka kufukuza kwa sababu si raia ilianza zamni sana tukionacho sasa ni ujukuu wa tabia hii chafu na yenye hila za kifisifisi.
Washenzi wakubwa tena wanaharamu msio na aibu.
Yaani mnajifanya kujua kwamba Mstafa si rai wa Tanzania leo hii karne ya 21??
Kweli Wa TZ hatuna aibu kabisa tunweza kwenda uchi mbele ya mkwe tukiahidiwa pochi.

Mtu wa hadhi ya juu kutimuliwa nchini tanzania kwa madai kwamba si raia wa nchi hii japo alifanya mengi makubwa na muhimu kule Zanzibar ni Marehemu Field Marshal John Okello. John Okello alifukuzwa tanzania kama Mbwa koko na Mwalimu Nyerere akaenda kenya nako wakamfukuza kama mbwa mwizi akarudi kwao uganda.

Hivi watanzania tulidhani Dhambi hii itaishia kwa John Okello tu.
Mpaka leo hii hakuna mtu ndani ya serikali anathubutu kusema neneo juu ya hili la Okello.

Ukiosha kumbuka utaoshwa.
 
Hii ya kufukuza watu au kutaka kufukuza kwa sababu si raia ilianza zamni sana tukionacho sasa ni ujukuu wa tabia hii chafu na yenye hila za kifisifisi.
Washenzi wakubwa tena wanaharamu msio na aibu.
Yaani mnajifanya kujua kwamba Mstafa si rai wa Tanzania leo hii karne ya 21??
Kweli Wa TZ hatuna aibu kabisa tunweza kwenda uchi mbele ya mkwe tukiahidiwa pochi.

Mtu wa hadhi ya juu kutimuliwa nchini tanzania kwa madai kwamba si raia wa nchi hii japo alifanya mengi makubwa na muhimu kule Zanzibar ni Marehemu Field Marshal John Okello. John Okello alifukuzwa tanzania kama Mbwa koko na Mwalimu Nyerere akaenda kenya nako wakamfukuza kama mbwa mwizi akarudi kwao uganda.

Hivi watanzania tulidhani Dhambi hii itaishia kwa John Okello tu.
Mpaka leo hii hakuna mtu ndani ya serikali anathubutu kusema neneo juu ya hili la Okello.

Ukiosha kumbuka utaoshwa.

Interesting!!!
 
If we adhere to the rule of the law, we should be totally subject to the law of the land, more important the constitution. The constitution is clear that anybody who has been born in Tanzania will be a natural citizen of Tanzania. Jenerali Ulimwengu was declared not a citizen because one of his parents was not a citizen at the time he was born (he was born in Tanzania). Mbashe also faced the same situation, we should be precise that regardless of the status of the parents, any body who has been born here is automatic citizen. My concern is that politicians use this ambiguity to supress their challenger, Masha used it to object the candidacy of his opponents and thanks to the NEC that he was reinstated and came back strong to defeat Masha. CCM bosses did not like Mbashe and disqualified him on the ground that he is not a citizen. Had they read the constitution and grasped it, they wouldn't have had excuse to disqualify him since he was born in Tanzania. We should stop demonizing each other. Peace no hate
 
Mkulo ni myao wa Tunduru, Ruvuma baba yake alihamia Kilosa miaka mingi iliyopita ktk huko.
 
1. NENDENI RITA KAMA MTAKUTA CHETI CHAKE CHA KUZALIWA TANZANIA...huyu alizaliwa MALAWI na baba yake alikuwa MIGRANT LABOUR alyetokea MALAWI kwenda kwenye mashamba ya mikonge KILOSA iweje aongope kazaliwa MALAWI?



2. HIKO CHUO ALICHOKISOMA NDKO ALIKOPATA DEGREE FEKI...I MEAN HIKI NDICHO CHUO KINACHOTOA DEGREES MPAKA KWA MBWA!


3. ANADAI ALIKUWA MKURUGENZI WA NSSF lakini ukweli alikuwa kurugenzi wa NPF (i might be wrong)

Hivi kama ulizaliwa bongo before uhuru au ulihamia bongo before uhuru wewe si unakuwa mtanzania automatically?
Mdau jamaa alikuwa Director General wa NSSF kabla ya Dr Dau the currecnt Director General
Speaking of Makunganya the Chief si naye aliktokea Morogoro
Nafikiri sasa mnataka tuongelee akina Sykes and Nyirenda, the issue here is only the fake University
Nawasilisha
 
Kitu ninachopendea Tanzania unaweza kuishi na mtu hata zaidi ya miaka kumi na usimuulize wewe ni kabila gani au unatokea sehemu gani huu ndio uridhi aliotuacha Baba wetu wa taifa! Zidumu fikra za mwalimu Nyerere:whoo:
 
Sina ubaya na huyu mtu lakini katika kutaka kujilizusha na ufahamu juu ya hiyo shutuma ya degree, nimekutana na hii habari.

  • Connecticut: According to the Connecticut Department of Higher Education, Almeda was ordered to cease operating in Connecticut in October 2001. After an investigation in 2002 indicated that Almeda was continuing to advertise its programs in Connecticut, the Department of Higher Education sent Almeda a second cease and desist letter and referred the issue to the Connecticut Attorney General for possible legal action.[10]
  • Florida: In 2003 the Florida Department of Education made an agreement with Almeda to cease operating in the state. Although Floridians can still get a degree from the online university, Almeda warns Floridians that its degrees may not be valid for public employment in Florida.[11]
  • Texas: Almeda is on the Texas Higher Education Coordinating Boardlist of "Institutions Whose Degrees are Illegal to Use in Texas."[2]
  • Other states: Almeda's website also warns Almeda degrees may not be valid for public employment in Illinois, Oregon, New Jersey, North Dakota, Washington and Idaho.[7]
 
Mtu ana ACCA tangu mwaka 1977, wewe unaanza kumtengenezea kashfa kwa kutumia MBA ya mwaka 2005!!! Labda kama huelewi maana ya ACCA. Ukiangalia utaona hiyo MBA alifanya wakati kashakuwa kiongozi katika nafasi mbalimbali za mashirika makubwa nchini. Na hakupata uwaziri kwa kigezo cha hiyo MBA unayoiita feki.
Jaribu kuangalia maana ya ACCA, unaweza kukuta Mkullo ndio mtanzania wa kwanza kuwa na ACCA.

Kuhusu uraia, hujasema kitu. Umeuliza maswali tu. Kama una majibu ya maswali yako yalete ili tuyachambue.
 
Msije kusikia hata JK si mtanzania ni Mzambia au mngazija kwa asili. Binadamu tunaishi kwa kuhama hama. Mbona nchi km USA Schwazenerger ni Governor.

Hata wewe tukifuatilia kwa makini tunaweza kukuta si mtanzania. Hawakujua kuwa si raia tangu walipompa ukurugenzi NSSF?

Wewe nji hii kuna kujua lolote? Shambani kwa bibi unaingia unachuma tu na unaondoka, Tanzania ndo iko hivyo! Kwa hiyo usishangae ndugu. Mfano wako wa USA hauna mashiko huko kuna taratibu za kufuata na unapata uraia kitu ambacho hapa kwetu hakipo. Maana hapa kwetu hata jamaa wa kutoka nchi nyingine akiwekwa kimada tu anaweza kuja kugombea hata Ubunge. Maskini Tanzania yetu imekosa mwenyewe wamemfanya Mkwere kama zezeta vile!!!!!!
 
Back
Top Bottom