Emerald hotel Zanzibari, kwa sasa ni The Mora Zanzibar hotel

Emanueli misalaba

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,113
1,659
Wana Jf habari za kutwa nzima ya leo wakuu!

Wadau kuna kitu hapa sielewi natamani wajuzi wanisaidie huenda hofu na mashaka vikaniondoka.

Wiki hii tangu ianze 04/03/2024, hadi siku ya leo 08/03/2024, imekuwa ni wiki ya u busy sana wa misafara ya kila mara ikitoka na kuingia si asubuhi, si mchana wala jioni na hata usiku misafara bandika bandua, huko Emerald hotel Zanzibari kwa sasa ikijulikana The Mora hotel iliyoko katika ufukwe wa Matemwe Muyuni kaskazini mwa Kisiwa cha Unguja.

Misafara hiyo inahusisha magari ya SMT na SMZ, katika kudadisi ni baadhi ya mawaziri wakifanya vikao na Wamarekani hapo hotelini kwa karibu siku 5 na kesho Wamarekani nimejuzwa wataondoka.

Maswali yangu ni.

1. Kwa misafara hii ya kila siku ikihusisha magari ya serikali ambayo huendeshwa na kodi za wananchi.

Nimejitahidi kutafuta kwenye Vyombo mbalimbali vya habari kuona vikao hivi labda vimeripotiwa na vyombo vyetu vya habari, lakini sijaona kabisa,
Kwa nini vikao hivi vimefanyika kwa siku zote hizi bila ya kuripotiwa na vyombo vya habari?

2. Je au mimi nimepitwa na taarifa za habari kuhusu hii mikutano?

3. Kama ni vikao vya viongozi wetu vya kibinafsi na hao Wamarekani, je wako sahihi kutumika misafara mikubwa ya kiserikali vile halafu bila kuripotiwa?

4. Si lazima waseme wamejadili nini bali ni vikao vinahusu nini.

5. Wanajidili nini ambacho hawataki kuujulisha umma?
Natanguliza shukurani.
 
mawaziri na viongozi mbalimbali wapo kazini, usiwe na wasi wasi, endelea na shughuli zako kwa bidii serikali iko kazini kuhudumia wananchi na kuwatumikia 🐒
mawaziri na viongozi mbalimbali wapo kazini, usiwe na wasi wasi, endelea na shughuli zako kwa bidii serikali iko kazini kuhudumia wananchi na kuwatumikia 🐒
Mkuu Tlaatlaah mawaziri wako kazini gizani?
 
Mkuu Tlaatlaah mawaziri wako kazini gizani?
gizani!🐒

kulikua na tatizo la umeme majuzi na bado sio stable sana kwa Zanzibar ila upo, but hiyo haiwezi kufanya vitu vifanyike gizani, umeme mbadala upo siku zote na hotel hiyo ni kubwa mno haiwezi kukosa standby generator....

lakini pia umwezaje kuona watu wanafanya kazi gizani hotel kubwa kama hiyo au unatamani waache pazi wazi 🐒

Kumbuka kuna wateja pia ambao hulala humo humo na wanalipa pesa ndefu kisha uwalaze kiza ya kweli hayo 🐒
 
Wewe ni mmoja wa hao Mawaziri?

Mh waziri mikutano yenu pale Matemwe Muyuni Zanzibar, mliofanya kwa siku 5 je kuna chombo chochote cha habari kimeripoti hiyo mikutano au mikutano imefanyika kimya kimya, huku umma wa Watanzania wengi wako gizani kwenye hili?

Mkutano wa mawaziri wa Jumuia ya madola pale Golden Tulip hotel Zanzibar, Mhe Rais Samia kwenye kufungua na Mhe Rais Mwinyi kwenye kufunga ilikuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari.

Huu wa baadhi ya mawaziri na Wamarekani hotel ya Matemwe kwa nini haijaripotiwi na media?
 
kama mwanahabari mkongwe unaefahamu misingi ya uandishi na weledi wake, unafahamu vizuri sana mahali pakupata ufahamu, uelewa au ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali serikalini 🐒

hii kubabaika na wasiwasi ambayo si muhimu umeibebea wap na umeanza lini ndrugu kutaka kuleta taharuki kwa Jamii EMANUEL misalaba
 
Back
Top Bottom