Hatimaye wazee wadai Mustapha Mkullo si mtanzania

malawi hakuna mtu anyeitwa mustapha,majina kama hayo utayakuta libya,somali au kidogo pemba lol
 
sasa wamempitisha anagombea kwenye jimbo lake kupitia sisiem
ingawa yeye kweli sio raia kama wazee wametoswa walikuwa wana
taka kumuharibia thru majungu tu tanzania ni nchi ya kipekee una
weza kuwa kiongozi wakati wewe sio raia.


Hii mbinu si mpya. Hao wazee wamejifunza kutoka CCM. Ni viongozi wangapi wa CCM waliowahi kuitumiikia nchi katika nafasi mbali mbali na kwa miaka lakini baadaye wakaambiwa si Watanzania?, wengine hata kubidi kuomba uraia upya? Nchi ina madudu hii!!!
 
nini cha kushangaza! mbona hata baba wa taifa anadaiwa kuwa ni mtusi ...na uwepo wake eneo la butiama linatokana na babu yake aliyekuwa mpagazi wa mdachi mmoja kuvinjari eneo hilo akitokea rwanda. mdachi huyo alipomaliza miadi yake katika koloni la tanganyika ambalo wakati huo lilijumuisha nchi za rwanda na burundi, akarudi kwao na babu ya baba wa taifa akaamua kuishi hapo butiama!!

we ni muongo wa kwanza duniani. Ungerelate Somalia tungechangia maana historia ya Babu wa mwalimu iko clear!
 
[/COLOR]Hii mbinu si mpya. Hao wazee wamejifunza kutoka CCM. Ni viongozi wangapi wa CCM waliowahi kuitumiikia nchi katika nafasi mbali mbali na kwa miaka lakini baadaye wakaambiwa si Watanzania?, wengine hata kubidi kuomba uraia upya? Nchi ina madudu hii!!!
Siku utasikia Ridhiwani si mtz
 
Nimesoma habari hii kwenye Nipashe. Wazee wa huko kwake Morogogoro wamemwandikia JK barua kudai Mkulo ni Mmalawi .Wana JF hii kweli.?

mtu wakupewa lawama ni Jk Nyerere yeye ndie aliyewapa wageni vyeo ktk nchi hii,kikwete kawakuta wameshaingia kwenye system afanyeje?
 
Hivi nchi hii ndo imeoza ivi! Hata jk nyerere walisema sio mtz, mkapa walisema sio mtz,jenerali ulimwengu wakasema sio mtz,bashe wakasema sio mtz, mkullo sio mtz!!! TUTIMUE VIONGOZ WOTE NINI?? INAWEZEKANA HATA MIJITU YA RITA SIO MITANZANIA! INAPEANA BIRTH CERT KAMA LAMBALAMBA!
 
Jamani mkitaka kuchambua kuhusu uraia inawezekana wengi wetu hatuna asili ya Tanzania......
 
Asilimia zaidi ya 90 ya viongozi wa nchi hii kuanzia boss wao mkuu pale juu wana vyeti feki. Kuna haja ya kuweka mfumo wa kuhakiki elimu za wananchi wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi.
 
Ulimi ni kiungo kidogo sana ila unaweza sababisha maafa kweli. Hivi haya yote yamekuja baada ya kutamka tutakula jasho letu!! asingesema wala kusingekuwa natatizo.

jamani tuombe Mungu, amani iendelee kuwepo.
 
In adding info to that kuna habari zinazodai pia Samuel Siita nae sio Mtanzania, ukitaka jua hili nenda Urambo ukatafute ndg zake kama utawapata, kule Urambo ana Tafuta jina Sitta kwa Wanyamwezi au Wasukuma huwezi lipata pia na hata wenye majina ya Sitta hawana undugu nae hata kidogo. Jamani hii ndio nchi yetu bana tunasubiri kuuzwa na sisi weneyewe

Si kweli, Sitta ni jina la wasukuma na wanyamwezi. Ninachojua, mkewe Samweli ndio mwenye asili ya Malawi huko, surname yake ni Simwanza!
 
Nimesoma habari hii kwenye Nipashe. Wazee wa huko kwake Morogogoro wamemwandikia JK barua kudai Mkulo ni Mmalawi .Wana JF hii kweli.?

Sio kama wana hoja yenye mashiko,kwa hiyo hata Obama kwa kua baba yake alikua ni Mkenya basi nae hakustahili kua rais wa America?sioni kama hiyo kitu ina tija!
 
Hapo sina Hoja, kwa sababu hakuna DNA ya uraia nani anaweza thibitisha. Ila nijuacho kwa maslahi ya watawala , wanapenda viongozi waandamizi wao wawe na utata hasa kwenye masuala ya uraia au kesi za mauaji na Uhaini ili watumie udhaifu huo Kama remote control kwa wasaidizi wao Hao.
 
Hata Abdallah Shaweji ambaye alikuwa mbunge wa huko Kilosa kabla ya Mkullo pia hakuwa raia. Huyu naye alikuja na wazazi wake katika mashamba ya mkonge na baadaye akapanda vyeo hadi kuwa meneja mkuu wa shamba la mkonge pale kimamba-kilosa ambapo pia mkullo anatokea maeneo hayo ya kimamba.

Lakini kwa Kilosa sishangai, kuna mtu anaitwa Omari Abdallah Makumulo naye alishawahi kuwa mbunge miaka ya 80 hadi 90. Kabla ya hapo alikuwa mchumi mkuu mwandamizi wa shirika la posta na simu, huyu naye ilisemekana kuwa hakuwa raia. lilipigwa zengwe hadi akawekwa kando na nafasi yake akachukua bw. Shaweji.
 
Kwa hali hii, Tz hata ipite miaka elfu kumi hatutapata maendeleo. Badala ya kujadili maendeleo mnajadili uraia wa mtu.
 
Sio kama wana hoja yenye mashiko,kwa hiyo hata Obama kwa kua baba yake alikua ni Mkenya basi nae hakustahili kua rais wa America?sioni kama hiyo kitu ina tija!

wamarekani karibu wote sio wenye nchi kwa mtazamo huu,wenyewe ni wahindi wekundu!
 
Mfamaji,
Sasa kama ana asili ya Malawi kuna tatizo gani?
Mkuu wangu hizi ni tuhuma za watu waliolewa mawazo ya bara ambao zamani tulikuwa tukiwaita Washamba. Ushamba ni pamoja na kutooona watu wa makabila mengine wakichanganyikana nanyi.. Hivyo kujichanganya kwao kumeletwa na Nyerere wakati huko pwani watu wa makabila walikuwepo karne na karne kabla hata ya kufikiria huo Uhuru.

Pili, Huwezi kuzungumzia asili wa mtu kama ndio Uraia wa mhusika. Kabila na Uraia, Vitu hivi havifanani na inaonyesha tena kwamba tunahitaji sana elimu ya Uraia kwani tunarudi katika Makabila kuzungumzia Uraia wa mtu. Na hakika tukifuata hivyo nchi zote duniani zitaingia ktk vita mpya ya Ukabila.
Umezungumzia ukabila,hoja ni UTAIFA,wewe vp?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom