Hatimaye Waraka umemtoa pangoni “mwenyewe”!

Hatimaye Waraka umemtoa pangoni “mwenyewe”!

Hapa hakuna swala la Udini .. Ni propaganda za kisiasa zinaendeshwa ili kufunga midomo watu.. Na wamekaribia kushinda.. Mana sasa hivi tunajibizana wenyewe kwa wenyewe..
 
Naam!

Sinema bado inaendelea kwa kasi huku vioja vikiendelea kujitokeza.leo kuna matukio mawili makubwa yaliyotokea.

Waraka wa baraza la maaskofu(Roman catholic)kupinga mkataba wa ubinafsishaji wa bandari za Tanganyika.
Ambao umesomwa nchi nzima katika kila kanisa na vigango vyake kote nchini.
Jambo hili limewachanganya sana!
Na hivyo kupelekea kuibuka kwa tukio la pili....

.....Tukio la pili ni lile la kuibuka Rais mstaafu awamu ya nne kutokea huko Rorya-Mara.

Yeye anaujibu waraka huo kwa kuigeuza hoja na kuwa "Udini" akiamini yeye kwamba hatuelewi kinachoendelea.

Kiujumla hawa wakuu wanazidi kujiumbua wao wenyewe,wameona wajaribu kutumia platforms za kidini ili ku-push DP-WORLD.

Kesho tunasubiri tumsikie huyo Kinara wa nchi kwenye Jubilei nyingine ya kanisa lingine kutimiza miaka 60 huko Arusha.

Hii ni kwa sababu mkuu wa sterling anajua kabisa nguvu ya TEC.

TEC inao uwezo wa kuongea na Dunia na ikaeleweka.View attachment 2723168View attachment 2723169
Maaskofu siyo watu wa michezo michezo. Kikwete bado hajajibu hoja ya msingi
 
Acheni kukuza vitu vidogo, kuna mambo mangapi magumu yamepita kiulakni tu
 
mwisho wa siku ukweli ni kwamba dini na siasa HAVITENGANI!
Wanasiasa ndio hao hao wanadini ama sivyo wakati wa uchaguzi wanasiasa wachaguliwe na wanasiasa wenzao na wanadini wabaki na imani zao!
Nchi ni yetu sote!
Acha ujinga wewe kwani hao maaskofu hawatapata tabu na matokeo ya hovyo ya mkataba kwamba wao watahama nchi kwani wao ni watu wa dini au
 
Viongozi wa serikali kuzidi kuiegemea hoja ya udini jamani wanazidi kuharibu. Si wajibu tu hoja za wananchi juu ya MKATABA. Kwa nini kimbilio lao ni udini?

Mbona yeye JK na watangulizi wake wote walikuwa challenged?! Hata Magu alikuwa challenged na watu wa dini zote. Kwa nini suala la dini lionekane leo kwa Samia. Sio sawa. Tutaingia kwenye shida kubwa kuliko hii ya bandari kwa ubinafsi wao.
 
HAIWEZEKANI KUWATENGA VIONGOZI WA KANISA NA SIASA ZA NCHI YAO!

Wapendwa Watanzania!
Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala au watu walio karibu na watawala wa Tanzania wakibanwa na viongozi wa dini hasa maaskofu huanza kutoa maneno ya propaganda dhidi ya viongozi wa dini wakiwaambia 'wasichanganye dini na siasa'. Msemo huu wanautumia kama kichaka cha kujifichia wasiguswe na viongozi wa dini!

Kauli hizo zimeibuka tena kwa kishindo zaidi kuanzia mwezi Juni 2023 baada ya maaskofu kuingilia sakata la Mkataba wa Bandari. Hivi karibuni tuliikemea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili hoja ya viongozi wa dini kuonekana wakiwa na viongozi wa vyama vya siasa.

Tumeona ni wajibu wetu ili kuwaelimisha watu kuhusu suala hili kusudi wasije wakapotoshwa na wanasiasa katika suala zima la kudai haki katika taifa lao. Wanasiasa ni wajanja sana na wanajua nafasi na nguvu ya viongozi wa dini katika jamii ndio maana wanatumia nguvu ili kupotosha ukweli kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika ukombozi wa kifikra katika taifa.

Tunapenda kukiri kuwa hili tunaloliandika ndilo eneo ambalo sisi tuna ubobezi nalo, kwa hiyo hatubahatishi bali tunakiandika tunachokijua, tulichokisomea na kukifundisha katika ngazi za Chuo Kikuu.

Kwa upande wa Wakristo, chimbuko la dini hiyo ni mji wa Yerusalemu, Israeli ya Kale. Lakini, ni vizuri watu wakaelewa kuwa Ukristo una mizizi yake miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hivyo, msingi mkubwa wa mafundisho ya Ukristo ni Biblia Takatifu yenye sehemu kuu mbili - Agano Jipya na Agano la Kale.

Dini haifanywi kwa wanyama na wala siasa pia haifanywi kwa ndege. Dini ni mfumo mzima wa maisha ambao ndani yake kuna mambo mengi. Tunaposoma au kufundisha kuhusu dini lazima tusome maisha ya jamii nzima ambayo kwanza dini ilifika kwayo. Kwa upande wa Wakristo, sisi tunasoma kuhusu jamii mbalimbali kama Misri, Syria, Ukaldayo (Babeli), Rumi, Wagiriki, Jordan, Waisraeli, Waajemi, Waarabu, Lebanon, nk.

Katika kusoma na kujifunza dini tunafundisha waumini kuishi kwa mifano ya jamii hizo ikiwa ni pamoja na kuiga mema na kuyaacha mabaya na hayo yanawezekana tu kwa kusoma kuhusu maisha yao kupitia viongozi au manabii wao.

Tunaposoma na kujifunza Biblia tunakutana na mambo yafuatayo:
1. Familia (family institutions): familia, ndoa, watoto, wajane, urithi, kifo, maziko, nafasi ya wanawake katika jamii, nk

2. Taasisi za Kiraia (Civili institutions): idadi ya watu, utumwa, taasisi ya kifalme, familia za kifalme, utawala, ajira na uchumi, kilimo, Afya na tiba, sheria na haki, mgawanyo wa muda, vipimo vya uzito, mahakama, nk.

3. Taasisi za Kijeshi (military institutions): majeshi ya Israeli, ngome za kijeshi, mbinu za kivita, siraha za kivita, vita, vita vitakatifu, nk

4. Taasisi za dini (Religious institutions): ibada, madhabahu, nyumba za ibada, uongozi wa taasisi za dini, Ofisi ya Ukuhani, Ofisi ya Walawi, sadaka, imani potofu, uchawi, utaratibu wa ibada, siku za ibada, sherehe na siku za sikukuu, nk.

Watu waliokuwa juu ya yote hayo ni viongozi wa dini na ndio waliopewa majukumu ya kuifundisha na kuionya jamii. Taasisi hizo ziliwekwa kwa ajili ya watu na kilichotofautisha ni ratiba. Wakati wa vita walipigana na wakati wa amani watu hao walifanya sherehe. Wakati wa mambo mazito ikiwemo kujua mustakabari wa nchi walikwenda kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini. Alipotokea kiongozi mkorofi au jeuri alikemewa na viongozi wa dini au hata kutangaziwa kuondolewa madarakani na hao viongozi wa dini.

Sisi Askofu Mwamakula tunaitoa kwenu elimu hii ili msiyumbishwe ili muelewe kuwa viongozi wa dini kuingilia kati mtafaruku wa kisiasa au kiutawala ni ishara kuwa jamii yenu iko na afya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023; 12:35 jioni.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Mh. Jk anapaswa kutambua mtu/nafsi Moja hii hii inahitajika kuhudumiwa na siasa na dini Kwa pamoja na wakati wote wa maisha ya duniani. So hakuna jinsi ambavyo binadamu kiongozi wa kisiasa/mtumishi wa umma/ majeshi/ mfanyabiashara au vyovyote vile ktk maisha yake ya duniani anaweza asihitaji siasa BORA na mafundisho ya DINI ya kweli. Muhimu hapa ni Kwa wanasiasa kuwa honesty Kwa jamii na Kila kitu kitaenda sawa. Wabunge tu wa ccm wote ni waumini wa dini ktk madhehebu Yao hii ni kukuonesha kwamba mambo haya mawili yanategemeana ktk maisha ya Kila siku.
 
kimya kileee kumbe mnajijua.
Hii safari tunakwenda perpendicular tukutane Ng’ambo ile.
Mmeichezea sana hii nchi
Alijisemea Mwalimu ( RIP) ‘ Hatujaja kutoa posa’
Mwalimu huku wenzio wale uliwakataa kata wametoa posa kwa waarabu tumeuza nchi kwa vipande vya fedha..
Lakini hatutakuangusha karibu kinaeleweka..
 
Naam!

Sinema bado inaendelea kwa kasi huku vioja vikiendelea kujitokeza.leo kuna matukio mawili makubwa yaliyotokea.

Waraka wa baraza la maaskofu(Roman catholic)kupinga mkataba wa ubinafsishaji wa bandari za Tanganyika.
Ambao umesomwa nchi nzima katika kila kanisa na vigango vyake kote nchini.
Jambo hili limewachanganya sana!
Na hivyo kupelekea kuibuka kwa tukio la pili....

.....Tukio la pili ni lile la kuibuka Rais mstaafu awamu ya nne kutokea huko Rorya-Mara.

Yeye anaujibu waraka huo kwa kuigeuza hoja na kuwa "Udini" akiamini yeye kwamba hatuelewi kinachoendelea.

Kiujumla hawa wakuu wanazidi kujiumbua wao wenyewe,wameona wajaribu kutumia platforms za kidini ili ku-push DP-WORLD.

Kesho tunasubiri tumsikie huyo Kinara wa nchi kwenye Jubilei nyingine ya kanisa lingine kutimiza miaka 60 huko Arusha.

Hii ni kwa sababu mkuu wa sterling anajua kabisa nguvu ya TEC.

TEC inao uwezo wa kuongea na Dunia na ikaeleweka.View attachment 2723168View attachment 2723169
Nyie mliomsikia kataja hata kifungu kimoja cha mkatana ule?
Kama hajafanya hivyo basi yeye ndiye analeta Choko choko za kidini na hazitamsaidia.

This time watanzania hatuburuzwi kwa migongo ya dini kwanza hiyo dini ameijulia wapi?
 
Na kikwete na kinana ni washika dau wa Waarabu wa dubai kuuziwa nchi

walidhani mipango yao ambayo wamekuwa wakipanga haijulikani

Kikwete nchi uliiharibu mwenyewe huu ni mwanzo tu

Nature itafanya kazi
Kikwete alifaidika kwa kiasi fulani na siasa za Udini wakati ule alipozidiwa hoja na Dr. Slaa. Hivyo anaamini akichomeka mambo ya dini yeye na wengine watatupoteza maboya. Suala la bandari halina mahusiano yoyote na dini. Kama anategemea wakitumia kete ya Udini watafanikiwa basi amechemka. TEC wamefanya kweli bila kujali hiyo propaganda mfu ya Udini.
 
Haswaaa..........wamezoa kudanganywa wananchi wanajificha eti Tunu za taifa.

Hizo tunu wangekuwa wanajali tungekuwa maskini?
Si ndio hapo, mtu anajifanya kuhubiri amani, kisha yeye na chama chake wanapora chaguzi za nchi bila kujali hiyo amani. Hawa ndio kuna ule wimbo unasema wanahubiri amani huku wameficha mapanga mifukoni.
 
Back
Top Bottom