Hatimaye Waraka umemtoa pangoni “mwenyewe”!

Hatimaye Waraka umemtoa pangoni “mwenyewe”!

Naam!

Sinema bado inaendelea kwa kasi huku vioja vikiendelea kujitokeza.leo kuna matukio mawili makubwa yaliyotokea.

Waraka wa baraza la maaskofu(Roman catholic)kupinga mkataba wa ubinafsishaji wa bandari za Tanganyika.
Ambao umesomwa nchi nzima katika kila kanisa na vigango vyake kote nchini.
Jambo hili limewachanganya sana!
Na hivyo kupelekea kuibuka kwa tukio la pili....

.....Tukio la pili ni lile la kuibuka Rais mstaafu awamu ya nne kutokea huko Rorya-Mara.

Yeye anaujibu waraka huo kwa kuigeuza hoja na kuwa "Udini" akiamini yeye kwamba hatuelewi kinachoendelea.

Kiujumla hawa wakuu wanazidi kujiumbua wao wenyewe,wameona wajaribu kutumia platforms za kidini ili ku-push DP-WORLD.

Kesho tunasubiri tumsikie huyo Kinara wa nchi kwenye Jubilei nyingine ya kanisa lingine kutimiza miaka 60 huko Arusha.

Hii ni kwa sababu mkuu wa sterling anajua kabisa nguvu ya TEC.

TEC inao uwezo wa kuongea na Dunia na ikaeleweka.View attachment 2723168View attachment 2723169
Kidogo kidogo tutaelewana baadae baada ya maji kujitenga na mafuta
 
Dini na siasa vinatengana sana tu. Ufalme wa mbinguni ni wa mbinguni na wa duniani ni wa duniani. Maslahi binafsi ndo huunganisha dini na siasa.
Wajinga nyie mnawafanya watu wa Mungu wawe maskini mnajificha kwenye dini na siasa.

Nenda Saudi arabia au Irani uwambie watenganishe dini na serikali uone kama utamka ukiwa mzima.

Mafisadi nyie
 
Nimekuwa nikipinga mkataba huu wa DP WORLD na serikali kwa sababu ya ubovu wake
Lakini
najiuliza kwa nini tec wanaupinga huu mkataba kwa nguvu zote?
Je? Wanapenda bandari kuendelea kuwa shamba la bibi au kuna maslahi yao au unafuu wanaupata hapo bandarini
Na wanajua mwarabu akikabidhiwa bandari ule unafuu hautakuwepo tena?.
 
Kazi ipo leo.
Yeye mwaka 2010 alimtumia Prof. Lipumba na misikiti kuendesha siasa.

Na Prof alikiri mwenyewe.

Leo kaenda kanisani, huko, ndiko kafanya siasa.

Alipotaka kushinda uchaguzi alitumia dini. Hii haikuwa shida.

Leo Dili lake linaonekana gumu, anasema viongozi wa dini wanyamaze.

Hili ni lake, shida niliwaambia tangu mwanzo, injinia halisi wa hili limkataba ni huyu.

Kuna style timu yake ya mkakati ilitumia, aonekane hayumo, tena wakaenda mbali zaidi kum set ili aonekane anapinga mkataba huu.

Sasa kamba imekazwa asipotarajia.

Ametoka nyuma kwenye kupiga kinanda, amekuja kuhutubia kabisa mbele.
Kabisa, na za chini ya pazia ni kuwa hii DP World iko mikononi mwa watanzania wenzetu, ila hao DP World wanatumika kinyemela. Ndio maana hata waliosaini huko upande wa DP World sio viongozi wa serikali, bali huku ndio serikali imesaini kuanzia viongozi.

Uzuri wezi wameshastukiwa, sasa wanatishia sijui amani, sijui Udini ili wafanikiwe kunyamazisha watu. TEC wamefanya kweli kuigomea huo mkataba hadharani, na kwenye makanisa yao maazimio hayo yanasomwa waziwazi.
 
Ndugu zangu tuombee Nchi yetu , Tumuombee sana Rais wetu kiongozi wetu. Tunaitaji maombi ya kuja pamoja na Kusimama pamoja Kumuombea hili awe imara kwa kuchukua maamzi sahihi. Naamini atatuvusha Salama kama March 2021.

Mi binafsi naona mbali na kuwa ni viongozi wa Kiimani (Dini), bado ni wananchi na viongozi wa kundi kubwa la wananchi. Kuzungumzia kwenye masuala makubwa ya kitaifa sioni kama ni kuchanganya Dini na Siasa. Nnachoamini ata wakati Bunge linaitisha maoni juu ya Mkataba huu naamini ilikuwa ni kwa wananchi wote viongozi wa dini inclusaive, Daftari la wapiga kura pia viongozi wa dini inclusaive, Kwenye Box la kura viongozi wa Dini inclusaive. Ikiitishwa mapendekezo ya Kuboresha Katiba bila shaka hao viongozi wa dini thy are absolutely inclussive.Binafsi sina ujuzi kwenye ground za siasa ila najaribu kuwaza tu. Kuna masuala mazito ya kitaifa ambayo 50/50 we Playing them politically but Social-life or social-economic in nature ( Eg. Milipuko ya Magonjwa kama Corona-ni sawa siasa pekee na wanasiasa kuwa solely player katika masuala ya nature hii?). Kuna plays za politicians battles (politicians wakiwa viwanjani) mara huyo kamsema vibaya yule au mara kundi moja kulalamikia kundi jingine kutoridhika kwenye uchaguzi...au kutuumiana kuibiana kura etc,etc( Not Necessary or important Dini kujiingiza kwenye sarakasi hizi za Siasa- Wapigane ngumi wafanyiane figisu wapigane mikwara May be iswhat i can solely regard as Church's Non of their ply business. Nnachojaribu kusema, tusitupiane lawama wala kupuuzana wala kutaftiza oja za wewe inakuhusu au wewe haikuhusu cha msingi kwa sabbu sote ni watanzania basi tujipe jukumu lakuhakikisha Tanzania iko salama. Ni jukumu la waislam, wakristo, wanasiasa na wasio na naupande wowote ule kuileta nchi yetu pamoja. Tumuombee Rais wetu na Viongozi wetu. Tusibezane kwa mlengo wa itikadi za vyama wala imani. So long as wewe ni mtanzania basi hili linakuhusu ata kama ni kiongozi wa Dini. Tanzania ni Mama yetu ni Maisha yetu.
 
Bandari ya Bagamoyo ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 
Naona mods wanajitahidi kufuta threads zinazohusu maoni ya udini na siasa. But mwisho wa siku ukweli ni kwamba dini na siasa HAVITENGANI!
Wanasiasa ndio hao hao wanadini ama sivyo wakati wa uchaguzi wanasiasa wachaguliwe na wanasiasa wenzao na wanadini wabaki na imani zao!
Nchi ni yetu sote!
Hawajui..

Hawa wanasiasa wanatunga sera za kodi, tozo nk na sheria zingine nyingi za hovyo zinazowaathiri wananchi wenye dini zao wakiwemo hawa viongozi wetu wa dini..

Cha ajabu sisi wananchi wenye dini zetu tukihoji maamuzi yao mabaya ya kutunga sheria zinazoleta athari hasi kwenye maisha yetu, eti wanasiasa hawa kina Kikwete, kina Samia Suluhu Hassan na chawa wao wanasema tusichanganye siasa na dini..!

This is absolutely very ridiculous and it doesn't make any sense at all......!!

Definitely, hii ni defensive mechanism ya hovyo na ya kipuuzi sana toka kwa viongozi hawa wanasiasa. Kwa kifupi wanatafunya wananchi ni wajinga sana...
 
Nimekuwa nikipinga mkataba huu wa DP WORLD na serikali kwa sababu ya ubovu wake
Lakini
najiuliza kwa nini tec wanaupinga huu mkataba kwa nguvu zote?
Je? Wanapenda bandari kuendelea kuwa shamba la bibi au kuna maslahi yao au unafuu wanaupata hapo bandarini
Na wanajua mwarabu akikabidhiwa bandari ule unafuu hautakuwepo tena?.
Ukimpa mtoto wako shamba alilime kisha likawa halitoi mavuno unayoyataka, suluhisho lake ni kuliuza?
 
Dini na siasa vinatengana sana tu. Ufalme wa mbinguni ni wa mbinguni na wa duniani ni wa duniani. Maslahi binafsi ndo huunganisha dini na siasa.
Kwa Waislamu Mtume Muhammad alipigana vita vingi 1.Badr, 2. Uhud,3. Khandak na Hunayn, je, alichanganya dini na siasa? Yesu alikemea maovu ya watawala hadharani mpaka akasulubiwa, alichanganya dini na siasa? Dini na siasa unazitenga vipi?
 
mcezo ndo kwanza umeanza, kwa nguvu ya TEC lazima panya wote waanze kutoka mashimoni mmoja badala ya mwingine. na Sasa hivi kila tunapokutana kwenye jumuia ndogondogo tunajisomea kwanza walaka wetu . TEC ndo tumaini pekee lililobaki.
 
Nimekuwa nikipinga mkataba huu wa DP WORLD na serikali kwa sababu ya ubovu wake
Lakini
najiuliza kwa nini tec wanaupinga huu mkataba kwa nguvu zote?
Je? Wanapenda bandari kuendelea kuwa shamba la bibi au kuna maslahi yao au unafuu wanaupata hapo bandarini
Na wanajua mwarabu akikabidhiwa bandari ule unafuu hautakuwepo tena?.
Yani ww unaupinga halafu unashagaa wengine wanaoupinga? uko wapi kwani msomi wa std 7?
 
DP W ndio chanzo Cha anguko la CCM.
Just imagine, mkataba huu umekwenda mbali mpaka watu wasio maaskari na wasio miliki silaha wakafunguliwa kesi za uhaini kitu ambacho si sahihi kwa mwananchi wa kawaida.
Walipoona watu wanataka kifungua kesi kushinikiza Dr Slaa apelekwe mahakamani wakagundua wameingia Cha kike, fasta wakapewa dhamana.
Tunasubiri Madeleka naye afikishwe mahakamani wakubwa waumbuke.
DP W ndio anguko la CCM . Wahenga walisema. Adui mwenyewe ndiye anayekupa fursa ya kumshinda.
CCM wamewapa upinzani fursa.
 
Back
Top Bottom