Hatimaye Waraka umemtoa pangoni “mwenyewe”!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Naam!

Sinema bado inaendelea kwa kasi huku vioja vikiendelea kujitokeza. Leo kuna matukio mawili makubwa yaliyotokea.

Waraka wa Baraza la Maaskofu (Roman Catholic) kupinga mkataba wa ubinafsishaji wa bandari za Tanganyika, ambao umesomwa nchi nzima katika kila kanisa na vigango vyake kote nchini. Jambo hili limewachanganya sana!

Na hivyo kupelekea kuibuka kwa tukio la pili...

Tukio la pili ni lile la kuibuka Rais Mstaafu Awamu ya Nne kutokea huko Rorya-Mara. Yeye anaujibu waraka huo kwa kuigeuza hoja na kuwa "Udini," akiamini yeye kwamba hatuelewi kinachoendelea.

Kiujumla, hawa wakuu wanazidi kujiumbua wao wenyewe, wameona wajaribu kutumia majukwaa ya kidini ili na ku-push DP-WORLD.
Sasa wamesambaa nchi nzima kwenye Mimbari ya kidini.
Kisa ni "DEEP- WORLD"

Kesho tunasubiri tumsikie Kinara wa nchi kwenye Jubilei nyingine ya kanisa lingine la "Anglican" kutimiza miaka 60 huko Arusha.ambako wamemualika.
Hii ni kwa kwa sababu "Starling" wa movie anaijua kabisa nguvu ya TEC.

Anajua kwamba TEC inao uwezo wa kuongea na dunia na ikaeleweka.
Na sio kueleweka tu,bali pia kuaminika kwa 100%.

JamiiForums507454731.jpg
JamiiForums-1424352711.jpg

View attachment 2723668
 
Kazi ipo leo.
Yeye mwaka 2010 alimtumia Prof. Lipumba na misikiti kuendesha siasa.

Na Prof alikiri mwenyewe.

Leo kaenda kanisani, huko, ndiko kafanya siasa.

Alipotaka kushinda uchaguzi alitumia dini. Hii haikuwa shida.

Leo Dili lake linaonekana gumu, anasema viongozi wa dini wanyamaze.

Hili ni lake, shida niliwaambia tangu mwanzo, injinia halisi wa hili limkataba ni huyu.

Kuna style timu yake ya mkakati ilitumia, aonekane hayumo, tena wakaenda mbali zaidi kum set ili aonekane anapinga mkataba huu.

Sasa kamba imekazwa asipotarajia.

Ametoka nyuma kwenye kupiga kinanda, amekuja kuhutubia kabisa mbele.
 
Mwisho wa siku ukweli ni kwamba dini na siasa HAVITENGANI!
Wanasiasa ndio hao hao wanadini ama sivyo wakati wa uchaguzi wanasiasa wachaguliwe na wanasiasa wenzao na wanadini wabaki na imani zao!
Nchi ni yetu sote!
Dini na siasa vinatengana sana tu. Ufalme wa mbinguni ni wa mbinguni na wa duniani ni wa duniani. Maslahi binafsi ndo huunganisha dini na siasa.
 
Naam!

Sinema bado inaendelea kwa kasi huku vioja vikiendelea kujitokeza.leo kuna matukio mawili makubwa yaliyotokea.

Waraka wa baraza la maaskofu(Roman catholic)kupinga mkataba wa ubinafsishaji wa bandari za Tanganyika.
Ambao umesomwa nchi nzima katika kila kanisa na vigango vyake kote nchini.
Jambo hili limewachanganya sana!
Na hivyo kupelekea kuibuka kwa tukio la pili....

.....Tukio la pili ni lile la kuibuka Rais mstaafu awamu awamu ya nne kutokea huko Rorya-Mara.

Yeye anaujibu waraka huo kwa kuigeuza hoja na kuwa "Udini" akiamini yeye kwamba hatuelewi kinachoendelea.

Kiujumla hawa wakuu wanazidi kujiumbua wao wenyewe,wameona wajaribu kutumia platforms za kidini ili ku-push DP-WORLD.

Kesho tunasubiri tumsikie huyo Kinara wa nchi kwenye Jubilei nyingine ya kanisa lingine kutimiza miaka 60 huko Arusha.

Hii ni kwa sababu mkuu wa sterling anajua kabisa nguvu ya TEC.

TEC inao uwezo wa kuongea na Dunia na ikaeleweka.View attachment 2723168View attachment 2723169
Katika nchi makini huyu alitakiwa awe gerezani, mwizi na fisadi wa kutisha
 
Mwisho wa siku ukweli ni kwamba dini na siasa HAVITENGANI!
Wanasiasa ndio hao hao wanadini ama sivyo wakati wa uchaguzi wanasiasa wachaguliwe na wanasiasa wenzao na wanadini wabaki na imani zao!
Nchi ni yetu sote!
Uko sahihi,kama dini na siasa visiingiliane...kilikoni kila mikutano na hafla za kisiasa wao ndio wa kwanza kualikwa seat za mbele?
DP-WORLD imewachanganya akili kabisa.
 
Dini na siasa vinatengana sana tu. Ufalme wa mbinguni ni wa mbinguni na wa duniani ni wa duniani. Maslahi binafsi ndo huunganisha dini na siasa.
Ahaa! Kumbee???
Basi kama ndivyo ilivyo wanadini waache kabisa kuombea taifa na viongozi wao. Na wanasiasa waache kuapa kwa kutumia vitabu vya dini zao!

Siasa ni jamii. Na jamii ni watu. Na watu ndio hao wenye dini na wasio na dini! Nchi ni yetu sote!
 
Kazi ipo leo.
Yeye mwaka 2010 alimtumia Prof. Lipumba na misikiti kuendesha siasa.

Na Prof alikiri mwenyewe.

Leo kaenda kanisani, huko, ndiko kafanya siasa.

Alipotaka kushinda uchaguzi alitumia dini. Hii haikuwa shida.

Leo Dili lake linaonekana gumu, anasema viongozi wa dini wanyamaze.

Hili ni lake, shida niliwaambia tangu mwanzo, injinia halisi wa hili limkataba ni huyu.

Kuna style timu yake ya mkakati ilitumia, aonekane hayumo, tena wakaenda mbali zaidi kum set ili aonekane anapinga mkataba huu.

Sasa kamba imekazwa asipotarajia.

Ametoka nyuma kwenye kupiga kinanda, amekuja kuhutubia kabisa mbele.
Tatizo ni kwamba haelewi kwamba dunia imebadilika,mawasiliano baina ya raia na raia sasa yako juu kwa kiwango kikubwa na sio kile kipindi cha kutegemea habari za magazeti.
 
Naam!

Sinema bado inaendelea kwa kasi huku vioja vikiendelea kujitokeza.leo kuna matukio mawili makubwa yaliyotokea.

Waraka wa baraza la maaskofu(Roman catholic)kupinga mkataba wa ubinafsishaji wa bandari za Tanganyika.
Ambao umesomwa nchi nzima katika kila kanisa na vigango vyake kote nchini.
Jambo hili limewachanganya sana!
Na hivyo kupelekea kuibuka kwa tukio la pili....

.....Tukio la pili ni lile la kuibuka Rais mstaafu awamu awamu ya nne kutokea huko Rorya-Mara.

Yeye anaujibu waraka huo kwa kuigeuza hoja na kuwa "Udini" akiamini yeye kwamba hatuelewi kinachoendelea.

Kiujumla hawa wakuu wanazidi kujiumbua wao wenyewe,wameona wajaribu kutumia platforms za kidini ili ku-push DP-WORLD.

Kesho tunasubiri tumsikie huyo Kinara wa nchi kwenye Jubilei nyingine ya kanisa lingine kutimiza miaka 60 huko Arusha.

Hii ni kwa sababu mkuu wa sterling anajua kabisa nguvu ya TEC.

TEC inao uwezo wa kuongea na Dunia na ikaeleweka.View attachment 2723168View attachment 2723169

View: https://youtu.be/cTmfQqT1jGY
 
Back
Top Bottom