Hatimaye waliomkata mkono Mwigulu wakamatwa

Hatimaye waliomkata mkono Mwigulu wakamatwa

Daaaah nimekuja fasta kweli nikijua ni Mwigulu Nchemba

Nilianza kushangilia kumbe sie!

Masikipo pole sana huyo mtoto!

Sheria ifuate mkondo wake na haki itendeke

Duuuh! Ulishaanza kushangilia! Kaaazi kweli kweli.
 
yani hi post ndo nimeamka nayo leo, hivi mleta mada ulitaka kuvutia watu kusoma mada yako? Si ungemalizia tu majina yote. Ila angekuwa mwigulu huyu ningesikitika sana, tungepoteza mkono wa mwenezi wa cdm.
 
Jina limemponza dogo. Majina kama Mwigulu kwa matendo ya Mwigulu Chemba inaonesha jina hilo lina mkosi...

Kama mzazi sishauri mzazi mwenzangu kumpa mwanao jina la Mwigulu


Mwigulu maana yake ni Mbingu
 
Hatua kali za fundisho zichukuliwe kwa hao magaidi na pia mungu awanyime rizki hawa wanaofanya mzaha ktk hii thred
 
dah!hizi imani potofu zinachefua. Halafu jina la victim nikajua ni yuleee wa scarf shingoni
in my
view the death penalty must be applied to these individuals for what
they have done. please kwa wale
mnaojua mwigulu(the good one) anaendeleaje please mtufahamishe mara ya
mwisho nilipomuona kwy luninga alikuwa akiogopa kurudi shuleni akiofia
kuuliwa na majangili hawa nilijisikia vibaya sana chozi kudondoka.
hongereni sana polisi mkoa wa Rukwa.


Polisi mkoani Rukwa kwa kushirikiana na wadau limewakamata watu tisa
wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumkata mkono mtoto mwenye ulemavu wa
ngozi (albino) Mwigulu Matonange (9).

Mkono wa mtoto huyo ulikuwa ukiuzwa kwa shilingi milioni mia sita
(600,000,000).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na mteja wa mkono huo kutotimiza
masharti ya makubaliano yao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema kukamatwa kwa
watuhumiwa hao kumefuatia taarifa za siri toka kwa wasamaria wema na
kikosi maalumu cha kitaifa kilichoundwa kwa ajili ya kushughulikia
matukio hayo ya ukatili wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu (27), James Paschal (24)
na Ibrahimu Tella (27).

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Tabora wakiwa wanatafuta soko
la kuuza viungo vya albino katika mikoa ya Shinyanga na Tabora na ndipo
mtego wa mawasiliano ulipowekwa na kufanikiwa kuwakamatwa watuhumiwa hao
watatu ambao walikuwa katika harakati za kutafuta soko.

Watuhumiwa hao walipohojiwa walikiri kuhusika na tukio hilo na
kufanikisha kukamatwa pia kwa Nickson Ngalimika kwa jina maarufu Kadogoo
(25) mjini Mpanda akiwa na mkono wa albino katika harakati za
kuusafirisha kwenda mkoani Tabora.

Kamanda Mangate alisema kuwa mara baada ya polisi kufanikiwa kuwakamata
watuhumiwa hao, waliwataja wenzao wanne walioshirikiana nao katika
unyama huo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Peter Said maarufu kwa jina la simon
Msabato (32), Ignas Sungura (27), Faraja Jairos (31) maarufu kwa jina la
Mwezi mpya na Kurwa Mashilimu (29)marufu Khamis.

Mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao waliweza kumtaja mganga wa jadi,
Hamis Mnywanywa (65) mkazi wa kijiji cha Kalemela B wilayani Urambo
mkoani Tabora ambaye ndiye aliwatuma kufanya unyama huo kwa ujira wa
shilingi milioni mia sita kila mmoja lakini baadaye akashindwa kupata
kiasi hicho na kusababisha waanze kuhaha kutafuta wateja wa mkono huo.

Kamanda Mwaruanda amesema mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na njama hizo
zilizosababisha kukatwa mkono mtoto huyo na kuwa alikusudia kuutumia kwa
kutengenezea unga maalum wanaoutumia wachawi kusafiri toka sehemu moja
hadi nyingine nyakati za usiku kwa kupaa angani.

Mtoto huyo alikatwa mkono Februari 15, mwaka huu majira ya saa 11 jioni
katika kijiji cha Msia tarafa ya Mtowisa zikiwa zimepita siku tano tu
baada ya mlemavu mwingine wa ngozi Maria Chambanenje (38) kukatwa mkono
na watuhumiwa kunaswa siku nne baada ya tukio hilo.
source nipashe.
 
Daaa!hyo heading imenikumbusha enz za dar leo na alasiri news papers.
 
aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah.
nilianza kufurahi kumbe siye.
pole sana mtoto usiye na hatia.
 
Ila mil.600 parefu mazee hv ndugu zangu mnajua km kuna wabongo wanalala njaa?ht mm naweza kushawishika kupeleka mkono wangu nikauze km kuna mteja ajitokeze nimpe mkono wangu mm ni albino.
 
Hatua kali za fundisho zichukuliwe kwa hao magaidi na pia mungu awanyime rizki hawa wanaofanya mzaha ktk hii thred
Dont argue with mentally handicapped people, they are terrorists after all.
 
Back
Top Bottom