Hatimaye waliomkata mkono Mwigulu wakamatwa

Hatimaye waliomkata mkono Mwigulu wakamatwa

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Posts
2,376
Reaction score
1,519
in my view the death penalty must be applied to these individuals for what they have done. please kwa wale
mnaojua mwigulu(the good one) anaendeleaje please mtufahamishe mara ya mwisho nilipomuona kwy luninga alikuwa akiogopa kurudi shuleni akiofia kuuliwa na majangili hawa nilijisikia vibaya sana chozi kudondoka. hongereni sana polisi mkoa wa Rukwa.


Polisi mkoani Rukwa kwa kushirikiana na wadau limewakamata watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumkata mkono mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Mwigulu Matonange (9).

Mkono wa mtoto huyo ulikuwa ukiuzwa kwa shilingi milioni mia sita (600,000,000).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na mteja wa mkono huo kutotimiza masharti ya makubaliano yao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumefuatia taarifa za siri toka kwa wasamaria wema na kikosi maalumu cha kitaifa kilichoundwa kwa ajili ya kushughulikia matukio hayo ya ukatili wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu (27), James Paschal (24) na Ibrahimu Tella (27).

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Tabora wakiwa wanatafuta soko la kuuza viungo vya albino katika mikoa ya Shinyanga na Tabora na ndipo mtego wa mawasiliano ulipowekwa na kufanikiwa kuwakamatwa watuhumiwa hao watatu ambao walikuwa katika harakati za kutafuta soko.

Watuhumiwa hao walipohojiwa walikiri kuhusika na tukio hilo na kufanikisha kukamatwa pia kwa Nickson Ngalimika kwa jina maarufu Kadogoo (25) mjini Mpanda akiwa na mkono wa albino katika harakati za kuusafirisha kwenda mkoani Tabora.

Kamanda Mangate alisema kuwa mara baada ya polisi kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, waliwataja wenzao wanne walioshirikiana nao katika unyama huo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Peter Said maarufu kwa jina la simon Msabato (32), Ignas Sungura (27), Faraja Jairos (31) maarufu kwa jina la Mwezi mpya na Kurwa Mashilimu (29)marufu Khamis.

Mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao waliweza kumtaja mganga wa jadi, Hamis Mnywanywa (65) mkazi wa kijiji cha Kalemela B wilayani Urambo mkoani Tabora ambaye ndiye aliwatuma kufanya unyama huo kwa ujira wa shilingi milioni mia sita kila mmoja lakini baadaye akashindwa kupata kiasi hicho na kusababisha waanze kuhaha kutafuta wateja wa mkono huo.

Kamanda Mwaruanda amesema mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na njama hizo zilizosababisha kukatwa mkono mtoto huyo na kuwa alikusudia kuutumia kwa kutengenezea unga maalum wanaoutumia wachawi kusafiri toka sehemu moja hadi nyingine nyakati za usiku kwa kupaa angani.

Mtoto huyo alikatwa mkono Februari 15, mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Msia tarafa ya Mtowisa zikiwa zimepita siku tano tu baada ya mlemavu mwingine wa ngozi Maria Chambanenje (38) kukatwa mkono na watuhumiwa kunaswa siku nne baada ya tukio hilo.
source nipashe.
 
Bullshit! Kwa haraka haraka unaweza fikiri kuwa ni Mwigulu huyu wa sisiemu. Thread nyingine bwana!
 
Dah. I wish wangemkata mkono huyu mwingulu mchemba wa maccm..kumbe ni mtoto ddah
 
Dah. I wish wangemkata mkono huyu mwingulu mchemba wa maccm..kumbe ni mtoto ddah

Lupe kuwa na chembe hata ya huruma kwa binadamu mwenzio

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Pole sana mtoto mzuri, kwa hili naungana na Pinda hawa watu wauawawe tu ! Mtu mzima unaenda kufyeka kiungo cha mtoto mdogo

Pongezi polisi
 
Hivi ni kwa nini? Haya masuala ya mauaji, na ukataji wa viungo vya Albino yako commonly katika jamii za kisukuma? Nimefuatilia kidogo Mara Nyingi wahanga ni Wasukuma na inatokea Mara Nyingi Mikoa ya Kanda ya Ziwa na ikitokea kwingine Wasukuma wanahusika, na bado kuna unreported issue... Ukienda Buhangija Ukiwaona hawa vijana wenye Albinism waliokimbia makazi Yao utawaonea Imani
 
mil 600 si nampeleka ndugu yangu wakamkate mkono tu tutafuta wa bandia
 
Åaaah!! Nilijua Nchemba mie,any way pole yake sana bwana mdogo ulieumizwa na hawa wahuni
 
Jina limemponza dogo. Majina kama Mwigulu kwa matendo ya Mwigulu Chemba inaonesha jina hilo lina mkosi...

Kama mzazi sishauri mzazi mwenzangu kumpa mwanao jina la Mwigulu
 
Yaani we mleta Mada hufai kabisa. Nilifurahi nikijua ni Yule Mzinzi MWIGULU NCHEMBA ndio Kafumaniwa na kukatwa Mkono!!

Nilianza kuwalaumu walio Mkata Mkono kwani nilitamani kusikia Wamemkata UUME kabisa!!
Kumbe masikini ni mtoto na sio huyo Mwigulu Mzinzi.

Nawapa pole ndugu wote wa Mtoto aliekatwa Mkono.Nawapongeza sana pia polisi kwa kazi nzuri walioifanya kumbe polisi Ccm wakiamua wanaweza.?

Mwisho natamani sana ingekua MWIGULU MZINZI ni Mlemavu wa Ngozi ili Wamkate Sehemu za Ndoa.
 
Daaaah nimekuja fasta kweli nikijua ni Mwigulu Nchemba

Nilianza kushangilia kumbe sie!

Masikipo pole sana huyo mtoto!

Sheria ifuate mkondo wake na haki itendeke
 
Nilianza kufurahi nkahisi ni yule mzinzi mwigulu wa iramba,ghafla furaha yangu imekata na kuwa huzuni...
Wazazi nao inabd waangalie majina ya kuwapa watoto wao maana jina la mwigulu limelaaniwa na ndiyo maana mtoto mwigulu akakutana na yaliyomkuta.
Pole mtoto mwigulu
 
Dah! Nilijua ni Nchemba wamemlamba mkono...

Ha ha haa... ma pro chadema mume patikana mumeingia kwa vurugu mumerudi kichwa chini nimeamini huyu jamaa ni mwiba wa koo dah povu limewatokaa poleni kwa kununua bundle harakaharaka...
 
Back
Top Bottom