Hatimaye uhusiano wangu umefikia mwisho...

Hatimaye uhusiano wangu umefikia mwisho...

Habari Za humu ndani wakuu?

Natumaini wote ni wazima wa afya ukiachilia mbali changamoto za kijamii zinazotukabili, kama vile Mgao wa umeme na maji, binadamu tuache ukaidi wa kuharibu vyanzo vya maji ili kuepukana na hili janga la ukame,in Chief Hangaya’s voice.

Jamaa yako ni mhuni ndio maana anahisi wewe pia ni mhuni.
 
Kuna namna nyingi ya kuomba hela ambapo si lazima utaje neno hela kwenye maelezo yako

Ushazoea kuwa mcheshi kwenye simu mkiwasiliana, siku anakupigia unajibu kinyonge anauliza nini shida?

Unamjibu kodi ya nyumba imeisha afu mwenye nyumba kamaindi anataka kunipa notes alikua ananifokea hapa na ndio maana nimepokea simu yako nikiwa katika mode hiyo

Umeona pesa ilivyo ombwa hapo, kuna neno hela hapo?
Hahaha sawa kabisa mkuu,bibie anajaribu kutuaminisha haombi pesa lakini hata ukijaribu ku read between lines unaona hio kazi ya mwamba (urubani) ni moja ya vitu binti kavutiwa navyo akijua atakua akivuna chochote ndo maana hadi sasa kwa kiasi yuko njia panda.
 
Kudate na mwanamke mzuri sana was sura na umbo ni kujitakia maradhi ya moyo na pressure. Toto limejaa vizuri, sura nzuri, rangi yenyewe, mguu na nyonga, huko nyuma limekaa ndivyo halafu uwe na amani mda wote kweli!!!

Utapata sonona kisa mtoto wa mwanaume mwenzako.
 
Natamani niwe najua kupenda na kubembeleza kama huyo jamaa yako lakini wapi nashindwa.Kuwa makini usije angukia mikononi mwa watu kama mimi u will cry forever
 
Ukifikisha miaka 30 njoo una mathread ya kutafuta mume nitakukumbusha ujuaji, na kiburi chako cha leo. Na liko wazi kwa uandishi wako na mazingira unayosimulia wewe ni **** nje nje type. Kula ujana au sio !!
Habari Za humu ndani wakuu?

Natumaini wote ni wazima wa afya ukiachilia mbali changamoto za kijamii zinazotukabili, kama vile Mgao wa umeme na maji, binadamu tuache ukaidi wa kuharibu vyanzo vya maji ili kuepukana na hili janga la ukame,in Chief Hangaya’s voice.

Niende moja kwa moja kwenye mada nisiwachoshe sana, naandika nikiwa nimenyong’onyea sana ila najikaza tu kwa sababu maisha lazima yaendelee ila kimsingi ni kwamba mahusiano yangu yamefikia tamati na hii haina budi kutokea sababu mambo yamekua mengi kiasi kwamba unaona haina tena haja ya kuigiza upo na furaha kumbe kiuhalisia sio kweli.

I was dating a guy, siwezi kusema handsome guy nitakua nadanganya kwa sababu mimi sipendi wanaume wenye muonekano mzuri saana, yaani hicho sio kipaumbele kwangu kabisa. Basi bwana mahusiano yalianza mwaka mmoja uliyopita na tulikutana kule mjini Instagram.

Kama utani mambo ya DM haya mtoto wa kike nikaingia kingi baada ya kupigwa saundi za kufa mtu nikaona isiwe shida ukizingatia nilikua single kwa muda kidogo. Basi bwana baada ya kuwa na urafiki na huyu jamaa kwa muda wa kama mwaka hivi hatimaye nikakubali DM yake na tukaanza kuhamia WhatsApp, tukakubaliana kuonana na kweli tukaonana na tukaanza kujenga Chemitry na hatimaye tukaanza kuwa wapenzi.

Nachelea kusema mwanzo sikumpenda sana jamaa yaani nilikua nachukulia kawaida mno lakini kadri siku zilivyokwenda nilijikuta nampenda kwa sababu alinionyesha upendo wa hali ya juu, here am not talking about money no, just ile caring yake yaani he was there for me.

Asikwambie mtu huyu ndiye alikua mwanaume wa kwanza mnene kudate naye, nilikua sijawahi kabisa kudate mtu mwenye mwili wa kijayanti lakini kusema kweli nimegundua wanaume wanene warefu wenye muonekano wa kawaida wanajua kupenda nyie . Jamaa anampunga kiasi maana ni rubani katika shirika fulani la ndege hapa nchini lakini kwangu mm hiyo haikua issue sana kwangu kilichonivutia kwakwe ni kwamba ananipenda sana na yuko romantic kinoma.

Shida sasa ni kwamba ana wivu ule ambao haupimiki, yaaani nikisema mtu ambaye ana wivu alafu very insecure sijui kama mnanielewa? Kwanza alianza kufatilia sana cm yangu anasoma text na kuangalia call logs kila tunapoonana, ole wako sasa apige cm yako inatumika hiyo kesi sio ya nchi hii.

Kwakua nilishaanza kumpenda nikaona acha nimvumilie na kuanza kumuelewesha taratibu kwa kua kila mtu ana namna yake ya kupenda nikaona sio tatizo kubwa, lakini kabla ya hapo kuna siku alishika cm yangu kwa mara ya kwanza tangia tumeanza mahusiano so akakutana na text za nyuma nachat marafiki wa kiume tunaitana baby lkn sio wapenzi siunajua ile kichuochuo yaan kama utani tu weeee basi akanichukulia kama mdada mwenye mambo mengi kumbe wala ni ile kutaniana tu ukizingatia nilikua singo.

Basi bwana maisha yakaendelea akaanza ku block watu kwenye cm yangu, yaaan tukionana baada ya salamu tu anakagua cm nilikua sipendi kwa sababu hamna kitu kibaya nafanya kwaiyo nikawa najiuliza huyu kwa nn haniamini kiasi hiki? Mm mbona nimejifunza kumuamini na wala simu yake siigusi? Basi nikawa naanza kukosa furaha kidogo kidogo lakini napotezea kwa sababu nampenda. Kuna siku aligonga gari kwa nyuma kwa sababu ya kugombania simu ikawa kesi akamlipa mwenye IST yake laki mbili ya kunyoosha bampa nikasema huyu kaka sio mzima Wallah.

Nikiri kwamba kimuonekano mm na yy ni sawa na mbingu na ardhi ndio maana anakuwa very insecure lakini nilijitahidi kumuonyesha upendo wa hali ya juu cz kuna vitu amazing ambayo yupo navyo na sio rahisi kuvijua kama hauna ukaribu naye.

Siku za nyuma tukigombana namwambia tuachane na sijali basi huwa ananibembeleza tunarudiana alivyofanikiwa kuteka hisia zangu sikuwahi hata sikumoja kumtamkia neno kuachana sababu mm kama nikimpenda mtu basi kumuacha ni ngum sana kwaiyo sitaki kuropoka kitu ambacho naona kitaniumiza na siko tayari kubreakup.

Basi kama miezi mitatu iliyopita nimeshaachwa kama mara tano hivi, tukikosana kidogo utaskia huniheshimu kama vipi tuachane, mtoto wa watu naomba msamaha yanaisha. Kuna kipindi nilikua field Kwenye moja ya media kubwa hapa nchini weee hapo ndio tulikua tunagombana almost everyday. Siku hiyo akanambia tuachane maana huniheshim unapiga picha na wakaka, mara kwa nn mnawasiliana yaaan hata kama ni mambo ya kazini, nikasema huu sasa ni upuuzi nikamwambia poa tuachane, siku haijaisha anaanza kuteseka yy na mm najishusha yanaisha.

Sasa jana tarehe 17.11.2021 nimeona isiweshida, bora haya mahusiano yafikie mwisho. Mpaka mtu anakwambia tuachane kila mki mess up basi huyo atakua anamaanisha anachokiongea nikasema leo afe kipa afe beki tunaachana kweli na haijalishi nampenda kiasi gani bora nife nimechoka sasa.

Sababu ni ya kipuuzi sana, haina mashiko kabisa yaaan eti kisa kanipigia cm saa tano ucku anasema nikitua Dar nakuja kukuchua twende nyumbani nikamwambia nina Assignment Kama tatu hivi na moja ni research proposal kwaiyo nakuomba nivumilie nitakuja kesho jioni. Povu likaanza kumwagika oooh hunipendi unaniavoid umebadilika sana kama vipi nikupe space maana unanidharau sana now days, baada ya kusoma magazeti yake nikawa natetemeka kwa hasira, yaaan naandika text nafuta naandika tena nafuta mpaka nilijihisi nimedata.

Nilichokifanya nilisubiria amalizie magezi yake alafu nikajibu text moja tu kama ifuatavyo 17.11.2021 alafu nikatulia. Akaanza kunipigia cm unstoppable, meseji Kama zote, mara oooh yaaan “ndio umeamua tuachane kweli? “ i still love you plz dont do this...kimoyomoyo nikasema what the fu**ck yaaan unanifanya kama mjinga kwamba muda wote ukijiskia kuniacha unafanya hivyo maana unajua nitakubembeleza turudiane nikasema hapana imetosha.

Kweli bwana leo siku ya pili natumiwa magazeti kama yote kwa ajili ya text moja tu ya tarehe na nimeshaamua nakaza hii wiki nzima nikishindwa kumove on nitarudi ila nikiweza basi imetoka hiyo. Imagine umeacha upuuzi wote kwakua unamuheshim mpenzi wako lkn haisadii kitu, ni stress mwanzo mwisho mpaka nikahisi au huyu kuna vitu vibaya anafanya kwaiyo anahisi na mm nikama yeye au hizi insecurities zimezidi kiwango? Huwezi amini naumia kinoma ila najikaza tu maana ukiwa ulishamzoea mtu ni ngumu sana kuishi mbali naye lakini hamna namna.Nipeni pole wakuu maana nahisi Huyu mwanaume hanifai kwa ajili ya future life, wivu ukizidi unaboa sana aisee.

NB wanaume vibonge mjiamini jamani sisi tunawapenda hivyo hivyo maana mnaroho nzuri sana, na mnajua kupenda,hawa walamba lips hamna kitu ni show off tu, kwa hivyo mkipendwa mshikamane muache mahangaiko na mawivu yasiyo na kichwa wala miguuu. Niwatakie kila la kheri wanafamilia wa JF katika ujenzi wa Taifa letu.
 
Pole Dear, Though Nimependa mtiririko wa uandishi wako.

Kifupi Unaonekana upo vizuri kiakili na Hata kimwili.

Ushauri wangu Naomba uendelee kumkazia uyo jamaa Hadi achoke na akusahau kabisa.

Nimekupenda bure.
 
Kusema ukweli nilikuwa kama your guy mwanzoni mwa mahusiano yangu na huyu baby mama wangu. Nilikuwa na sababu zangu either zilikuwa za kijinga but they mattered to me. Niamini mimi kuna kitu ulikifanya kikabuild hiyo insecurity sisemi ulicheat hapana sio kila insecurity inakuwa because you cheated Hapana. Kuna stuffs kwako vinaweza kuonekana very minor issues but huwezi jua the other side unachukulia vipi. Bila honesty talk mje kwenye common understanding. Ununda kwenye relationship hakuna kombe. That's it. You need to fix your shits together as one.
 
I can relate Your story ,Happened to me This year, I pushed this girl too far to love me and she just quit . 😂😂 that was the most childish thing I ever done . She even told me . She loves the other guy who practically I was above him in every thing . And she left me . I learnt so much from that situation . Am now so open on learning how to love . I tend to take new great ideas from Every relationship I know and add them in my files . I got say she was my great indirect teacher . Despite being better , to hell she left me .😑
 
Wapi nimesema nimemaliza chuo mkuu? Nimesema nilikua field now ndio namalizia third year
Akuache mkuu. By the way Una mwandiko mzuri. Mshikaji anakuelewa and he is a good guy kama ulivyosema anasumbuliwa na insecurities kutokana na wewe kuwa kisu sana na it seems bado mbichi. Kama uko Chuo na huko hivyo no wonder umelelewa vyema. Huyo mshikaji ni mtu pouwa kama anageushinda udhaifu wake wa insecurities.

Anyway kama hakufunzwa hilo na mamayee basi na afunzwe na ulimwengu.
 
Back
Top Bottom