Hatimaye uhusiano wangu umefikia mwisho...

Miss Cherry

Member
Oct 2, 2020
36
249
Habari Za humu ndani wakuu?

Natumaini wote ni wazima wa afya ukiachilia mbali changamoto za kijamii zinazotukabili, kama vile Mgao wa umeme na maji, binadamu tuache ukaidi wa kuharibu vyanzo vya maji ili kuepukana na hili janga la ukame,in Chief Hangaya’s voice.

Niende moja kwa moja kwenye mada nisiwachoshe sana, naandika nikiwa nimenyong’onyea sana ila najikaza tu kwa sababu maisha lazima yaendelee ila kimsingi ni kwamba mahusiano yangu yamefikia tamati na hii haina budi kutokea sababu mambo yamekua mengi kiasi kwamba unaona haina tena haja ya kuigiza upo na furaha kumbe kiuhalisia sio kweli.

I was dating a guy, siwezi kusema handsome guy nitakua nadanganya kwa sababu mimi sipendi wanaume wenye muonekano mzuri saana, yaani hicho sio kipaumbele kwangu kabisa. Basi bwana mahusiano yalianza mwaka mmoja uliyopita na tulikutana kule mjini Instagram.

Kama utani mambo ya DM haya mtoto wa kike nikaingia kingi baada ya kupigwa saundi za kufa mtu nikaona isiwe shida ukizingatia nilikua single kwa muda kidogo. Basi bwana baada ya kuwa na urafiki na huyu jamaa kwa muda wa kama mwaka hivi hatimaye nikakubali DM yake na tukaanza kuhamia WhatsApp, tukakubaliana kuonana na kweli tukaonana na tukaanza kujenga Chemitry na hatimaye tukaanza kuwa wapenzi.

Nachelea kusema mwanzo sikumpenda sana jamaa yaani nilikua nachukulia kawaida mno lakini kadri siku zilivyokwenda nilijikuta nampenda kwa sababu alinionyesha upendo wa hali ya juu, here am not talking about money no, just ile caring yake yaani he was there for me.

Asikwambie mtu huyu ndiye alikua mwanaume wa kwanza mnene kudate naye, nilikua sijawahi kabisa kudate mtu mwenye mwili wa kijayanti lakini kusema kweli nimegundua wanaume wanene warefu wenye muonekano wa kawaida wanajua kupenda nyie . Jamaa anampunga kiasi maana ni rubani katika shirika fulani la ndege hapa nchini lakini kwangu mm hiyo haikua issue sana kwangu kilichonivutia kwakwe ni kwamba ananipenda sana na yuko romantic kinoma.

Shida sasa ni kwamba ana wivu ule ambao haupimiki, yaaani nikisema mtu ambaye ana wivu alafu very insecure sijui kama mnanielewa? Kwanza alianza kufatilia sana cm yangu anasoma text na kuangalia call logs kila tunapoonana, ole wako sasa apige cm yako inatumika hiyo kesi sio ya nchi hii.

Kwakua nilishaanza kumpenda nikaona acha nimvumilie na kuanza kumuelewesha taratibu kwa kua kila mtu ana namna yake ya kupenda nikaona sio tatizo kubwa, lakini kabla ya hapo kuna siku alishika cm yangu kwa mara ya kwanza tangia tumeanza mahusiano so akakutana na text za nyuma nachat marafiki wa kiume tunaitana baby lkn sio wapenzi siunajua ile kichuochuo yaan kama utani tu weeee basi akanichukulia kama mdada mwenye mambo mengi kumbe wala ni ile kutaniana tu ukizingatia nilikua singo.

Basi bwana maisha yakaendelea akaanza ku block watu kwenye cm yangu, yaaan tukionana baada ya salamu tu anakagua cm nilikua sipendi kwa sababu hamna kitu kibaya nafanya kwaiyo nikawa najiuliza huyu kwa nn haniamini kiasi hiki? Mm mbona nimejifunza kumuamini na wala simu yake siigusi? Basi nikawa naanza kukosa furaha kidogo kidogo lakini napotezea kwa sababu nampenda. Kuna siku aligonga gari kwa nyuma kwa sababu ya kugombania simu ikawa kesi akamlipa mwenye IST yake laki mbili ya kunyoosha bampa nikasema huyu kaka sio mzima Wallah.

Nikiri kwamba kimuonekano mm na yy ni sawa na mbingu na ardhi ndio maana anakuwa very insecure lakini nilijitahidi kumuonyesha upendo wa hali ya juu cz kuna vitu amazing ambayo yupo navyo na sio rahisi kuvijua kama hauna ukaribu naye.

Siku za nyuma tukigombana namwambia tuachane na sijali basi huwa ananibembeleza tunarudiana alivyofanikiwa kuteka hisia zangu sikuwahi hata sikumoja kumtamkia neno kuachana sababu mm kama nikimpenda mtu basi kumuacha ni ngum sana kwaiyo sitaki kuropoka kitu ambacho naona kitaniumiza na siko tayari kubreakup.

Basi kama miezi mitatu iliyopita nimeshaachwa kama mara tano hivi, tukikosana kidogo utaskia huniheshimu kama vipi tuachane, mtoto wa watu naomba msamaha yanaisha. Kuna kipindi nilikua field Kwenye moja ya media kubwa hapa nchini weee hapo ndio tulikua tunagombana almost everyday. Siku hiyo akanambia tuachane maana huniheshim unapiga picha na wakaka, mara kwa nn mnawasiliana yaaan hata kama ni mambo ya kazini, nikasema huu sasa ni upuuzi nikamwambia poa tuachane, siku haijaisha anaanza kuteseka yy na mm najishusha yanaisha.

Sasa jana tarehe 17.11.2021 nimeona isiweshida, bora haya mahusiano yafikie mwisho. Mpaka mtu anakwambia tuachane kila mki mess up basi huyo atakua anamaanisha anachokiongea nikasema leo afe kipa afe beki tunaachana kweli na haijalishi nampenda kiasi gani bora nife nimechoka sasa.

Sababu ni ya kipuuzi sana, haina mashiko kabisa yaaan eti kisa kanipigia cm saa tano ucku anasema nikitua Dar nakuja kukuchua twende nyumbani nikamwambia nina Assignment Kama tatu hivi na moja ni research proposal kwaiyo nakuomba nivumilie nitakuja kesho jioni. Povu likaanza kumwagika oooh hunipendi unaniavoid umebadilika sana kama vipi nikupe space maana unanidharau sana now days, baada ya kusoma magazeti yake nikawa natetemeka kwa hasira, yaaan naandika text nafuta naandika tena nafuta mpaka nilijihisi nimedata.

Nilichokifanya nilisubiria amalizie magezi yake alafu nikajibu text moja tu kama ifuatavyo 17.11.2021 alafu nikatulia. Akaanza kunipigia cm unstoppable, meseji Kama zote, mara oooh yaaan “ndio umeamua tuachane kweli? “ i still love you plz dont do this...kimoyomoyo nikasema what the fu**ck yaaan unanifanya kama mjinga kwamba muda wote ukijiskia kuniacha unafanya hivyo maana unajua nitakubembeleza turudiane nikasema hapana imetosha.

Kweli bwana leo siku ya pili natumiwa magazeti kama yote kwa ajili ya text moja tu ya tarehe na nimeshaamua nakaza hii wiki nzima nikishindwa kumove on nitarudi ila nikiweza basi imetoka hiyo. Imagine umeacha upuuzi wote kwakua unamuheshim mpenzi wako lkn haisadii kitu, ni stress mwanzo mwisho mpaka nikahisi au huyu kuna vitu vibaya anafanya kwaiyo anahisi na mm nikama yeye au hizi insecurities zimezidi kiwango? Huwezi amini naumia kinoma ila najikaza tu maana ukiwa ulishamzoea mtu ni ngumu sana kuishi mbali naye lakini hamna namna.Nipeni pole wakuu maana nahisi Huyu mwanaume hanifai kwa ajili ya future life, wivu ukizidi unaboa sana aisee.

NB wanaume vibonge mjiamini jamani sisi tunawapenda hivyo hivyo maana mnaroho nzuri sana, na mnajua kupenda,hawa walamba lips hamna kitu ni show off tu, kwa hivyo mkipendwa mshikamane muache mahangaiko na mawivu yasiyo na kichwa wala miguuu. Niwatakie kila la kheri wanafamilia wa JF katika ujenzi wa Taifa letu.
 
Daaaaaaaaaaaaaaaah kuna wanaume wanachezea chance ......................imagine nina pesa ndefu sana (mwaka huu ntawekwa kwenye list ya 21 ya forbes as kijana tajir chin ya miaka 30) ................lakn cjawahi kubaliwa na demu af kuna msenge anachezea chance adimu hizo
 
Habari Za humu ndani wakuu? Natumaini wote ni wazima wa afya ukiachilia mbali changamoto za kijamii zinazotukabili, kama vile Mgao wa umeme na maji, binadamu tuache ukaidi wa kuharibu vyanzo vya maji ili kuepukana na hili janga la ukame,in Chief Hangaya’s voice.
Kipindi cha kuwa na mahusiano imara ndio hiki unakipoteza, mtu anakukula wee mpaka utamu unakwisha na mimba juu ndio unajuwa kama ulikuwa unachezewa.

Nipe namba yako nikutumie msg ya uchumba nataka kukuowa naleta mshenga kwa wazazi wako halafu muoneshe huyo boya wako ndio utaujuwa ukweli wake.
 
Njoo kwangu acha kuteseka
20210927_140745.jpg
 
Hehehehehe acha nicheke tu...

Umenikumbusha ex bf wangu wa kwanza, alikuwa na tabia za kindenzi kama hizo! Ila hili la kwangu lilikuwa linapenda kitonga mteremko na halijui nini maana ya mwanamke asee, halijui kucare,lenyewe linajua kuomba uch..tu...nikaliambia kafie mbele mwanaume kama mwanamke asee full kujiliza
 
Pole ila ukweli mchungu unaenda kupoteza mwanaume anayekupenda kwa sababu ya kuendekeza usister duu, kwani huwezi kuishi bila picha na hao masharobaro? Huwezi kuacha nyendo za mashaka kama kuchat na wanaume? So you are going to be a single mama.
Kuwa single kuna tatizo gani? Uchumba sugu na kuwa single bora nini?

Uko na jitu limekuganda tu watu serious wanakupotezea wanajuwa mzigo una booking huu kumbe unawapotezea muda watoto wa watu halafu baadaye unaowa mwingine, hii siyo sawa.

Ni bora kuwa single zikimbana anamtunuku mtu utamu maisha yanasonga tu.
 
Habari Za humu ndani wakuu? Natumaini wote ni wazima wa afya ukiachilia mbali changamoto za kijamii zinazotukabili, kama vile Mgao wa umeme na maji, binadamu tuache ukaidi wa kuharibu vyanzo vya maji ili kuepukana na hili janga la ukame,in Chief Hangaya’s voice.
Wewe una wanaume wengi, jamaa yuko sahihi!! Meseji za nyuma na wanaume wako ukiwa chuo kwann huzifuti mpaka bwanaajo anazikuta? 😂😂

Ulipokataa kutoka na jamaa kisa Research proposal na assignments za nini wakati ulishasema wewe ulishamaliza chuo zamani??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom