hjayhals
JF-Expert Member
- Feb 13, 2013
- 768
- 558
Serikali au dola kwa ujumla ina mkono mrefu sana, na kwa muundo wake haijawahi kushindwa, huwa ni suala la muda tu.
Hivyo ni vyema unapotaka kuitunushia misuli lazima utafakari kwa kina sana, kwa maana ya madhara utakayoyapata wewe binafsi, familia yako na jamaa zako kwa ujumla.
Unaweza pata umaarufu wa muda mfupi lakini madhara yake ni ya muda mrefu.
Na kwa kawaida ukiona serikali ina deal na wewe ujue imejiridhisha kwa asilimia zote toka vyanzo vyake ya kua unaikosea.
Ni vigumu sana serikali kuonea raia wake wema, nasema haiwezekani. Nashauri wale mnaojiita wapambanaji dhidi ya dola mtafakari kwa kina sana kabla ya kutenda.
Mwisho kosoeni kwa staha mkiweka hadharani njia au mawazo mbadala, yatafanyiwa kazi ,hii ni imani yangu.
Kutusi, kudhihaki, kukejeli, kuonyesha dharau kwa mamlaka kwa kisingizio cha kukosoa haikubaliki hata kidogo, mtaumia kwani kila zama na kitabu chake, someni alama za nyakati.
Dua la kuku halimpati mwewe. Tulilia mpendwa wetu apelekwe mahakamani, ona sasa.
Tukutane tarehe 07/01/2020, safari ndio kwanza imeanza.
Narudia tena serikali haishindwi, ni suala la muda tu, ukiona mwenzako ananyolewa tia maji.
Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali haijawahi kushindwa?? Endelea kulala ukiamka utuambie kama serikali haijashindwa jambo dogo tu la kuwalipa watu pesa zao za korosho, utuambie pia haijashindwa kutoa tamko juu ya watu kuuawa na kutekwa. Badala ya kufanya maendeleo mko bize kugharamia kunyamazisha watu bila kufikiria kuwa kwa kufanya hivyo tu idadi ya wakosoaji inaongezeka kwa kasi mbaya. Mwisho wa siku serikali hushindwa! Nitafutie ilipo serikali ya omar al bashir.