Hatimaye Pengo la Mzee Mengi lazibwa, Hongera Waziri Makamba

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,785
218,411
Kabla ya kukutwa na Umauti , Mzee Reginald Mengi alikuwa na mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza Simu za Kisasa zinazoitwa Smartphone .

Mpango huo ulipotea baada ya Mzee huyo kufariki Dunia .

Sasa leo Waziri wa mambo ya kigeni January Makamba amewaleta Wahindi ili kuziba Pengo hilo.
---
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema Tanzania inauza zaidi mazao ya kilimo nchini India huku wao wakiuza zaidi nchini dawa na vifaa vya viwandani.



 
Jamaa kaanzia upigaji mwingine🤣
Nchi hii uwezi kuwekeza kama ukwepi kodi, hizo kampuni zote zinakwepa kodi balaa, uwezi kuwekeza kwenye nchi ambayo mtu anaendesha gari umbali mrefu kutoka Rwanda au Uganda kufuata bidhaa Bandari ya Dar halafu kitu chenyewe bado bei iwe rahisi kuliko Tanzania.

Bila ya kuangalia namna ya kufanya kugawanya hizi kodi kwa kila raia, tutaendelea kuangalia namna ya kukwepa kodi tu.
 
Nchi hii uwezi kuwekeza kama ukwepi kodi, hizo kampuni zote zinakwepa kodi balaa, uwezi kuwekeza kwenye nchi ambayo mtu anaendesha gari umbali mrefu kutoka Rwanda au Uganda kufuata bidhaa Bandari ya Dar alafu kitu chenyewe bado bei iwe rahisi kuliko Tanzania.
Bila ya kuangalia namna ya kufanya kugawanya hizi kodi kwa kila raia, tutaendelea kuangalia namna ya kukwepa kodi tu.
Ni aibu tupu
 
Kabla ya kukutwa na Umauti , Mzee Reginald Mengi alikuwa na mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza Simu za Kisasa zinazoitwa Smartphone...
Sijaona mantiki ya kumtaja mzee Mengi kuwa pengo lake limezibwa, kwenye story hii! Mengi alikuwa ni msaada kwenye nyanja nyingi.

Baadhi ya walemavu wanalia mpaka leo. Kuna familia za wamasai, wanalia mpaka leo, kutokana na alivyokuwa anawasaidia ma binti zao, kielimu.

Pengo lake HALIZIBIKI!
 
Sijaona mantiki ya kumtaja mzee Mengi kuwa pengo lake limezibwa, kwenye story hii! Mengi alikuwa ni msaada kwenye nyanja nyingi. Baadhi ya walemavu wanalia mpaka leo. Kuna familia za wamasai, wanalia mpaka leo, kutokana na alivyokuwa anawasaidia ma binti zao, kielimu.
Pengo lake HALIZIBIKI!
Mengi alitangaza kuanzisha kiwanda cha simu hizo kabla umauti haujamkuta , ndio chanzo cha kutajwa kwake hapa
 
Mengi ni mtanzania, kama ndoto yake ingetimia inamaanisha, mtaji ungekuwa wa ndani na faida ingebakia ndani. Ila muwekezaji anaweka mtaji (capital inflow) Ila faida inarudi kwao (profit outflow). Kwa hiyo hakuna gap lililozibwa

By the way, top ten ya matajiri Tanzania imejaaa watanzania wenye asili ya Asia na bado sioni black enterprises zikishamiri maana sioni jitihada zozote za kulifanya hilo liwezekane. Wacha viwanda vije ili tupate mshahara wa 8,000 per day maana ndipo furaha yetu ilipo "ajira za hand to mouth"
 
Back
Top Bottom