Habari
wapenzi.
Hakika nimeamini kwamba wanaume ni wabinafsi sana, simaanishi wote ila
asilimia kubwa ni wabinafsi. Akicheat yeye kwenye mapenzi wala ila
akicheat mwanamke inakuwa shuguli pevu. Nisimulie kidogo, Hope
mnakumbuka nishawahi kuja hapa nikilalamika kwamba mpenzi wangu ananunua
malaya, mbali na kuwa alikuwa ananunua malaya alikuwa na wapenzi
wengine wanne ambao niliwafahamu.
Alikiri kwamba ni kweli anafanya hivyo na kwamba yuko tayari kuacha na
kubadilika kabisa, ila sasa tatizo likaja kwa hawa wapenzi wanne
namuambia aniweke clear kama kweli kaachana nao wala hafanyi hivyo ndo
kwaanza unakuta anachati nao.Kweli niliumia sana maana kila nikimwambia
aniweke clear utasikia "Cherry mama kama huwezi kuvumilia ondoka. maana
kama huamini kama nimeachana nao sina namna ya kukuaminisha".
Nikaona kuacha na moyo wangu hautaki nikawaza cha kufanya ni kucheat tu
ili nipate relief, Kweli baada ya kucheat nilijisikia mwepesi na mwenye
Amani kupita maelezo. Basi last week akagundua kwamba nacheat, akawa
mkali utadhania sio yule aliyekuwa ananunua malaya na kunitumia picha za
wanawake wake wakiwa kwenye kitanda tunacholala.
Kweli nilikiri makosa na kumueleza kuwa chanzo ni yeye. jana akaniambia
eti nichart na mchepuko whatsap then nimtukane halafu ni screenshort
hiyo conversation nimtumie. Nikaona huu ni Ujinga, nikamwambia busara
hapa ni kuoa kwa vile umesema March unanipeleka home basi endelea na
process uoe kama nitakataa.
Nikaona haelewi anakomalia tu screenshort, ni prove kama kweli nampenda
yeye or mchepuko, nikamwambia siwezi, so akasema tusijuane nikasema poa.
tukaachana jana rasmi.
Sasa ninachojiuliza hivi ni sawa kulalamika screenshort wakati nishampa
go ahead ya kuniona? hii kukubali yeye anioe na sio mchepuko si ndo
upendo, screenshort ndo upendo wakati nina simu mbili naweza weka
privacy nikasave picha ya mchepuko nikajichatisha pale nikamfool.
Nikaona wacha aende maana mpenzi mwenyewe Dishi tu, ana salary nzuri but
hana maendeleo, ukimshauri tufanye hivi hataki, basi fanya maendeleo
yako kama mwanaume hataki, yaani mtu salary nzuri but maisha ya
shidashida tu. haambiliki hashauriki.