Dondoo za yaliyojiri kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Charles Magesa Arusha leo:
- Hakimu Magesa alisema ni kweli mahakama iliruhusu washitakiwa wabunge wahudhurie kikao cha bunge la bajeti na hivyo hawana tatizo na Mh. Mbowe, ila kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri ya kukamatwa kwake.
- Hakimu amesema mahakama inaendelea kuwapa ruhusa washitakiwa wote ambao ni wabunge kutohudhuria mahakamani hapo hadi pale ambapo kikoa cha bunge kitamalizika ila aliwasisitiza wadhamini wa washitakiwa kuhudhuria mahakamani kila siku ambapo tarehe ya kesi imepangwa
- Wakili upande wa Utetezi, Method Kimomogoro, aliiomba Mahakama kuondoa amri ya kukamatwa kwa Mbowe na kutaka apewe dhamana yake ya awali, ili aweze kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti ambalo yeye ni kiongozi wa kambi ya Upinzani na kwamba mdhamini wa Mbowe hakufika mahakamani kwa kuwa alisahau, na hiyo ipo kwa kila mtu na hata wao kama mawakili wanasahahu tarehe za mahakamani.
- Mdhamini wa Mbowe bwana Julius Margwe alizitaja sababu za kutofika mahakamani Mei 27, 2011 ni kutokana na kuwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso. Pia, hakufika Mahakamani Mei 30, 2011 kwa sababu mahakama haikumpa nafasi kusema lolote.
- Wakili wa Serikali Juma Ramadhani, aliiomba mahakama hiyo itoe onyo kali kwa mshitakiwa kwa kutofika mahakamani hapo na pia kumtaka mshitakiwa huyo na wenzake wawe na mawasiliano ya karibu na wadhamini wao, ili wasikosekane wanapotakiwa mahakamani hapo, pia, mdhamini wa Mbowe hana uhakika na hajui nini anafanya, hivyo hafai kuwa amdhamini.
- Hakimu Magesa akasema Julius ana makosa mengine yanayomkabili na hata hawezi kujieleza, hivyo Mahakama haina sababu kuwa naye sababu tayari ana kesi ya jinai ambayo hatma yake haifahamiki.
- Mahakama imemkubali mdhamini mwingine ambaye ni John Bayo, Diwani wa kata ya Elerai (CHADEMA).
- Baada ya Freeman Mbowe, kuachiwa huru na aliwashukuru wananchi na kusema anasikitishwa sana na kutumia nguvu kubwa kumlinda yeye na kumsafirisha usiku akiwa chini ya ulinzi mkubwa kama kwamba yeye alikuwa ni gaidi ambaye alikuwa na silaha, Mimi nilijipeleka mwenyewe polisi sasa kama kweli ningekuwa wa kukimbia ningejipeleka? Sasa wao hawajaona hayo yote haitoshi wameamua kutumia nguvu kubwa sana maana wakati wakinipeleka uwanja wa ndege walikuwa na polisi wengi sana zaidi ya 50 yaani utadhani ni gaidi anapelekwa alafu ndege ya kubeba watu mia ndo wameniweka mimi, wakati hayo mafuta wangeyaweka ata kwenye kutengeneza vitanda vya hospitali. Wanatumia vibaya kodi za wananchi alisema Mbowe. Alisema kuwa Serikali ilitumia ndege ya jeshi, ambayo ina uwezo wa kubeba watu 100, ambayo ilichukua watu watatu yaani yeye, Kamishina wa Polisi kanda kanda ya Ilala na Kamishna wa Polisi wa kikosi cha kuzuia ghasia wa Tanzania hadi KIA usiku wa majira ya saa 9.00. Pia alisema mbali na kusafirishwa kwa ndege hiyo kubwa, pia kulikuwa na magari nane ya FFU ambao walikuwa na mabomu na silaha kama wanasindikiza mhalifu. Akashukuru Polisi kutomfanyia unyama wowote, walikaa naye vizuri, isipokuwa alinyimwa haki yake ya msingi ya kuwa na uhuru wa kuwasiliana na watu. Mara baada ya kesi hiyo kumalizika wananchi walimbeba kiongozi waho kwa juu huku wakiimba.
Kesi ilihudhuriwa na wabunge 13 wa CHADEMA ambao ni Zitto Kabwe, Halima Mdee, Godbless Lema, Suzan Kiwanga, Ezekia Wenje, Christina Lissu, Paulina Gekulu, Israel Natse, Suzana Lyimo, Joseph Mbilinyi, Rahya Ibrahimu ( Mbunge toka Pemba), Joyce Mukya na Joseph Selasini.
SOURCE:
Wavuti - Home