Hatimaye, leo mimi ndio nahitaji ushauri kwenu wanajamii

Sonko Bibo

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2019
Posts
1,182
Reaction score
1,823
Iko hivi,
1. Leo nimegundua kuwa mwanamke ninaempenda sana ana ugonjwa ambao ni mtihani kwa watu wengi sana.

2. Ndugu zake wamekuwa wakiniharakisha nimuoe huyu binti tangu mwezi ule wa kwanza wa kukutana kwetu.
Hiki ni kitu kilinitisha sana nikachagua kuvuta subira kwanza mpaka nijue ni nini kinasababisha ndugu zake kutaka nifanye hiyo hatua kwa uharaka kiasi hicho?
Jibu limekuja leo hii

3. Ugonjwa huu ni janga kwenye jamii nyingi sana za nchi masikini na uchumi wa kati,
Ugonjwa uliogubikwa na unyanyapaa na hatari kubwa ya kumpoteza umpendae muda wowote.

4.Nimeelewa sasa kuwa ndugu wanahitaji binti yao apate mtu wa kudumu na ambae atalazimika kujitwisha haya majukumu mazito maadam atakuwa ameshajifunga kwenye minyororo ya maisha.

5. Binti sio mkweli juu ya ugonjwa unaomsumbua, anaisingizia presha na majini kwa mwanaume ambae anakutana nae.
Yaani mpaka sasa tunaenda mwaka amenificha na nishajua tayari ni ugonjwa gani unaomtafuna.

6. Madaktari wengi sio wote lakini ni watu wanaotoa taarifa kwa mwanaume zenye kificho ndani yake.
Yaani wanaweza kukuficha kiini cha tatizo mpaka pale mpendwa wako atakapofariki ndipo watathubutu kufungua midomo yao kukueleza.

7. Najua sina uwezo wa kumlinda mpenzi wangu na inaweza kuja siku nikampoteza ghafla. Itaniuma mno na nitasakamwa na ndugu zake maana sijamtolea chochote.
Na ugonjwa alionao sio kwamba hawaujui, wanaujua sana na wanamuonea huruma sana mwanaume atakaejikomiti kuishi na binti yao, ila ndio hivyo hawawezi kumuambia ukweli kuwa utateseka, utalia na kusaga meno huku kamasi zikikutoka puani na kuchanganyika na mate na machozi, kifupi utalia kilio kikuu cha kutojitambua hata ukipigiwa simu muda huo akili yako haitakuwa hapa duniani.

8. Nawaza tunaachana vipi? Maana kuachana ni lazima tu nikaze au nisikaze fuvu kuachana ni given.
Naachana nae vipi ili nisilete jeraha kwenye ubongo na moyo wa huyu mpenzi wangu?
Kumbuka kuachana kwetu ni kwaajili ya usalama wangu na si vinginevyo.

9. Nampenda mno na nimepokea hizi taarifa za ugonjwa kwa unyonge na mshituko mkubwa mno, moyo wangu una simanzi nzito. Maybe she was never meant for me.
Nina mfadhaiko wa nafsi mkubwa sana mimi SONKO.
Kuna uzi niliuleta hapa kipindi mtoto alipofariki tumboni na baadae mpenzi wangu akapata upofu wa ghafla.
Upofu nilipambania sana na hatimaye kwasasa shemeji yenu anaona.
Na tatizo la kupata upofu chimbuko lake liko kwenye huu ugonjwa.

10. Tangu mwanzo nasikika nikitaja ugonjwa, ugonjwa ila sitanabaishi ni ugonjwa gani kiasi cha kukupa maswali wewe msomaji.

Shemeji yenu ana kifafa.

Vijana kwa mabinti pia chukueni tahadhari mapema msiishie kutamaniana njiani na kukimbilia kuoana haraka haraka,,
Vuteni subira kwanza mchunguzane vyema kabla ya kuja kuleta migogoro kwenye jamii hapo baadae.

Nipo mwishoni nipeni ushauri kwanza juu ya hili la kwangu.
 
lazima uwe na 1st draft yaa uamuzi na sababu zake.Labda hapo unataka kupata kufahamu namna utakavyo muacha mtu uliyempenda bila kumuumiza moyo

Ila kumbuka maumivu yakiwa na sababu ya msingi huwa yanapona pia.Sijapenda pia trick waliyotaka kukuchezea wazazi wake.Wangekufahamisha mapema msingefika kote huko mbali.Ni wazazi matapeli naweza waita.

Nakumbuka kisa cha dogo mmoja ambaye aliozwa mke kumbe msichana ana kansa ya titi.Ila ndugu wa mke hawaku disclose.Miezi michache sana baada ya ndoa dogo akaanza kuuguza mke kwa takribani miaka miwili. Nadhani hata uchumi wake uliyumba na mwishowe binti akafariki.

sijajua,ila inaonekana hali ilibadilika haraka mara baada ya kuingia kwenye ndoa.siijajua labda ni kutokana na majukumu ya kwenye ndoa.labda kama asingeingia kwenye ndoa hali isingebadirika haraka kiasi hicho
 
Daah mkuu pole sana. Nakuelewa vizuri tu, miezi miwili imepita toka nimzike mdogo wangu (mtoto wa baba mdogo) kwa ugonjwa huu huu. Yeye ulimuanza akiwa darasa la 3, ikabidi aache shule awe mtu wa kukaa nyumbani tu kwa matibabu na uangalizi zaidi... Baada ya purukushani za miaka kadhaa hatimae Mungu aliamua kumpumzisha akiwa na miaka 24. Inauma sana mkuu asikwambie mtu, mateso aliyokuwa anapitia hayaelezeki. Chukua tahadhari mapema mkuu, huu ugonjwa kifo kiko mkononi muda wowote.
 
Back
Top Bottom