Hatimaye Lazaro Nyalandu aoa; kaoa miss Tanzania

Status
Not open for further replies.

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,945
Hatimaye moja ya wabunge wetu wa Singida na ambaye amekuwa akilalamikiwa sana kwa kuendekeza ubachela na usela, ameoa. Kama ilivyotarajiwa, amemuoa Miss Tanzania Faraja Kota. Kwa muda mrefu sasa mheshemiwa huyu amekuwa akiwanyatia sana hawa mamiss. Naambiwa jana kulikuwa na nderemo na vifijo vya kukata na shoka. Harusi ilifana sana na kila mkubwa wa bunge letu alikuwepo kuanzia na Six mwenyewe. Harusi ilipambwa na ngoma maridadi za kinyaturu.

Kudos Mheshimiwa Nyalandu. Utulie sasa.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Heshima kwako Mkumbo, ila tuchombeze na picha mbili tatu kama unazo pls!
Ni ombi tu.
Nawasilisha!
 
Heshima kwako Mkumbo, ila tuchombeze na picha mbili tatu kama unazo pls!
Ni ombi tu.
Nawasilisha!

yeah nyama na halua baba yake kama kuna vipicha tubandikie mambo yazidi kupendeza

mola awajaalie mapenzi na wadumu kwa afya na raha tele.

sio baada ya muda kuchokana
 
Bahati mbaya picha sijapata, lakini Michuzi ataweka (au ameshaweka) kule kwenye vitu vyake.
 
yeah nyama na halua baba yake kama kuna vipicha tubandikie mambo yazidi kupendeza

mola awajaalie mapenzi na wadumu kwa afya na raha tele.

sio baada ya muda kuchokana
mie picha ninazo..nitazidondosha hapo kesho..ila watu wa photo point wlaikuwapo,nashangaa kwanini hawajaweka picha katika blog yao..haya ndio mambo ya #rushwa ,inawezekana lazaro kakataza picha zake zisiwekwe katika mtandao kama ilivyokuwa katika harusi ya kinje.

Lazaro-38
Faraja-22
 
NDOA YA FARAJA KOTTA AIBU TUPU risasi mchanganyiko

Tukio hilo ambalo ni nadra sana kutokea katika sherehe za watu maarufu liliwashangaza waaalikwa na kuwafanya washindwe kuamini macho yao.

Vinywaji vilivyokuwepo katika sherehe hiyo ni maji, ‘wine', na soda pekee.

"Huwezi kuamini kilichotokea katika hafla hii ya mheshimiwa kwani vinywaji vilivyokuwa vikigawiwa, vilikwisha katikati ya sherehe hali iliyosababisha ndugu wa bwana harusi kumtonja MC Godwin Gondwe kukatisha baadhi ya vitu vilivyo kwenye ratiba ili mambo yasije yakaharibika zaidi," kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kwa kuhofia aibu zaidi ambayo ingeweza kuwapata waandaaji wa sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na vigogo mbalimbali wa serikali, Gondwe aliamua kukata mambo mengine yaliyoainishwa kwenye ratiba ambayo yangelazimu sherehe hiyo kuchukua muda mrefu huku hali vinywaji vikiwa vimeisha, jambo ambalo lingeleta fedheha.

Katika fufunika funika ya mambo ukumbini hapo Gondwe alijikuta akilazimika kurukia kipengele cha mwisho cha ratiba ambacho kilikuwa kinamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samuel Sitta kwenda mbele ya ukumbi kuongea machache kwa wanandoa hao.

Akiwa amelamba suti ya nguvu, Spika aliitakia maisha mazuri ndoa hiyo na kumuagiza mbunge Nyalandu kwenda naye bungeni mkewe ili kumtambulisha rasmi kama kanuni ya bunge inavyoagiza.

Kwa mujibu wa Spika Bunge, mbunge yeyote anapooa au kuolewa anatakiwa kumpeleka mkewe au mumewe kwenye vikao vya bunge viwili mfululizo ili kumtambulisha kwa wabunge.

Baada ya Spika wa bunge kumaliza kutanabaisha wasaa wake kwa wanandoa hao, alirudisha kipaza sauti kwa Gondwe ambaye naye bila kufanya ajizi alitangaza kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa sherehe hiyo, ndipo wageni waalikwa walipoanza kuinuka na kuondoka ukumbini hapo.

Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam
siku hiyo hiyo ya sherehe.
SOURCE;RISASI ...SHIGONGO
 
mmh shigongo, bado hujakoma kuandika habari ambazo si kuwa hazinufaishi jamii bali ni za kuwachafua watu na kusababisha madhara mkubwa ndani ya jamii

ushindwe na ulegeee
 
mie picha ninazo..nitazidondosha hapo kesho..Lazaro-38 Faraja-22

Nitazidondosha hapo kesho!!!! nadhani ulikuwa unaimanisha mwaka kesho teh teh teh mambo mengine bwana watu hujipa sifa hata wasizostahili....kaa kimya uonekane una busara!!
 
Nyalandu na Faraja.jpg

Jamaa kachukua jumla
Walimeremeta sana lakini nina wasiwasi hii angalia yake inaelekea kaona mwingine pembeni. Ndoa bado changa macho pembeni(Joke).
Hata hivyo nawatakia kila la heri Mh Nyalandu na Faraja ndoa njema
Both of you take care!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Enheeee! Hapo sawa kabisa, naona ombi langu la kutaka picha za wanandoa hao limekubaliwa.
Binafsi nawatakia maisha mema "Nyota" hao wa Tanzania, Mungu awabariki sana!
 
Hatimaye moja ya wabunge wetu wa Singida na ambaye amekuwa akilalamikiwa sana kwa kuendekeza ubachela na usela, ameoa. Kama ilivyotarajiwa, amemuoa Miss Tanzania Faraja Kota. Kwa muda mrefu sasa mheshemiwa huyu amekuwa akiwanyatia sana hawa mamiss. Naambiwa jana kulikuwa na nderemo na vifijo vya kukata na shoka. Harusi ilifana sana na kila mkubwa wa bunge letu alikuwepo kuanzia na Six mwenyewe. Harusi ilipambwa na ngoma maridadi za kinyaturu.

Kudos Mheshimiwa Nyalandu. Utulie sasa.

Hongera zake kwa kuachana na ukapera, bado mbunge mwingine kija Mh. Zitto.
 
Hongera zake kwa kuachana na ukapera, bado mbunge mwingine kija Mh. Zitto.

Icadon,
Zitto- naye achukue kati ya hawa mamiss wengine waliobaki! Kwani wote walishachukuliwa?
Kwanza Zitto ana kipaji cha kushawishi sana- sijui kwa nini hajapata jiko! Au ushawishi ni wa siasa tu?
Hebu kama mnamjua mschana mrembo- basi mskae kimya- mkonyezee Zitto!
 
Lidaka mahojiana ya Zitto kwenye Channel 10 kitambo kidogo alisema ana mchumba tayari kama sikosei yuko mlimani pale. Nadhani naye anasubiria wakati muafaka.
 
yani staki kuamini kuwa mkumbo nawe kama jina lako lilivyo ushajiingiza katika mkumbo wa kujadili maisha ya watu binafsi,mlikuwa mnapiga sana mikelele wakati slaa kweli alipora mke wa mtu aliposemwa mkaja juu ooh,maisha binafsi,vipi kwa nylandu? mkuki kwa nguruwe
Hatimaye moja ya wabunge wetu wa Singida na ambaye amekuwa akilalamikiwa sana kwa kuendekeza ubachela na usela, ameoa. Kama ilivyotarajiwa, amemuoa Miss Tanzania Faraja Kota. Kwa muda mrefu sasa mheshemiwa huyu amekuwa akiwanyatia sana hawa mamiss. Naambiwa jana kulikuwa na nderemo na vifijo vya kukata na shoka. Harusi ilifana sana na kila mkubwa wa bunge letu alikuwepo kuanzia na Six mwenyewe. Harusi ilipambwa na ngoma maridadi za kinyaturu.

Kudos Mheshimiwa Nyalandu. Utulie sasa.
 
wengi wa hao wabunge na viongozi wanaochelewa kuoa, wamepeleka kizazi kwa mganga wa kienyeji, kinakuwa ndo kafara ya cheo chao cha ubunge...mfano zitto alisema yeye ni mchawi, aliaga kwao kwa wazee alipokuwa anakuja dar, ndo maana hakufa kwenye ile sumu waliyokuwa wanataka afe...unaona?....mtu mzima kama zitto anaishi bila mke..kizazi kapeleka wapi?
 
mbona mwaweka mambo yaliyopitwa na wakati? watu wan watoto saizi !
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom