Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

Nadhani msikose baadhi ya magazeti kesho... kuna mambo mazito ambayo mheshimiwa Zitto aliyasema hapa kijijini.. na kama alivyosema kuna mambo ambayo hayawezi kuyasema kiundani hadi ripoti itoke.
 
Naona hiyo ripoti hawataki itoke au inafanyiwa 'mchakato' kama ilivyofanyiwa ile ya EPA. Sasa hivi jambo hili la wananchi kutoridhika na kutokuwepo kwa maslahi yoyote tunayopata kama nchi kutokana na dhahabu yetu lingetakiwa lichukue kipaumbele ndani ya chama na sirikali.

Ripoti imeshakamilika zaidi ya mwezi sasa na wahusika walioandika ripoti hiyo wameshasema kwamba wanasubiri kumkabidhi ripoti hiyo JK, lakini inaelekea JK hana haraka nayo!! anatafuta safari ambazo hazina kichwa wala miguu ili mradi tu apate kisingizio cha kutotafuta muda wa kukabidhiwa ripoti hiyo. SHAME ON THEM!
 
Sijui unawaza nini? Sikuelewi. Ila tu ujue kuwa sijawahi kuwa msaliti na mimi ni mtu mwenye misimamo isiyoyumba. Safari hii kuna wengi tu ambao wamewahi kuja. Mnyika alikuja mwaka 2006, kabla yangu, sasa sijui yeye ilitumika vigezo gani. Nadhani tuache utabiri

Mkuu Zitto,
Nachukua maneno yako kama ahadi kwetu. Lakini kama ujuavyo tushang'atwa na nyoka baada ya Kaborou kuishia mitini na wengineo. Kwa hiyo tunapokuwa na wasiwasi ni kutokana na historia ya wanasiasa wetu. Ila unapojitokeza na kututhibitishia msimamo wako, hilo linatia moyo. Safari na kazi njema.
 
Ndugu wana jf naomba tuelezane kama mimi binafsi niko out of touch ama la!

Ni wazi kuwa tunaendelea kulilia na kubembeleza kuhusu ripoti ya kamati ya madini!

Narudia tena tunabembeleza(sisi wananchi)
Kutokana na hilo basi nemejikuta nikijiuliza maswali nisiyoweza kupata majibu

Taarifa za awali zilikuwa ni kwamba Ripoti ishakabidhiwa kwa Mkuu.

Then Zitto akasema bado hawajafanya hivyo!

Tuna jua kuwa ishakamilika! Na kama sivyo...

Je bado wanaifanyia kazi ama hawajapata nafasi ya kumpa Mh Rais?

Mh Zitto sijui kama yuko hapa marekani ama keshaondoka!

Lakini haonyeshi tena ule moyo aliokuwa nao mwanzoni wa kuwa upande wa wananchi!

Na ndio maana tumetoa muda ambao tunaona kuwa unatosha la sivyo tuta muinclude Mh Zitto kweye propaganda za Rais kama hataki kutueleza kuwa ripoti iko wapi!

Akumbuke kuwa tulijadili hapa kama kweli hiyo kamati ni ya kumyamazisha ama ni ya kuwasaidia wananchi!

Tumeshuhudia Muungwana akishindwa kudeal na masuala ya kitaifa kwa sababu ya safari za kila kukicha!

Tunajua Mh Zitto yuko kwenye safari ama ziara yenye manufaa kama vile Mh Rais anavyodai pale akitetea safari zake!

Hatujali hizo safari! Je vilio vya wananchi vinafanyiwa kazi?

NAULIZA TENA RIPOTI IKO WAPI?
 
Ndugu wana jf naomba tuelezane kama mimi binafsi niko out of touch ama la!

Ni wazi kuwa tunaendelea kulilia na kubembeleza kuhusu ripoti ya kamati ya madini!

Narudia tena tunabembeleza(sisi wananchi)
Kutokana na hilo basi nemejikuta nikijiuliza maswali nisiyoweza kupata majibu

Taarifa za awali zilikuwa ni kwamba Ripoti ishakabidhiwa kwa Mkuu.

Then Zitto akasema bado hawajafanya hivyo!

Tuna jua kuwa ishakamilika! Na kama sivyo...

Je bado wanaifanyia kazi ama hawajapata nafasi ya kumpa Mh Rais?

Mh Zitto sijui kama yuko hapa marekani ama keshaondoka!

Lakini haonyeshi ten ule moyo aliokuwa nao mwanzoni wa kuwa upande wa wananchi!

Na ndio maana tumetoa muda ambao tunaona kuwa unatosha la sivyo tuta muinclude Mh Zitto kweye propaganda za Rais kama hataki kutueleza kuwa ripoti iko wapi!
Tumeshuhudia Muungwana akishindwa kudeal na masuala ya kitaifa kwa sababu ya safari za kila kukicha!

Tunajua Mh Zitto yuko kwenye safari ama ziara yenye manufaa kama vile Mh Rais anavyodai pale akitetea safari zake!

Hatujali hizo safari! Je vilio vya wananchi vinafanyiwa kazi?

NAULIZA TENA RIPOTI IKO WAPI?

Jmushi,

Kama kina Zitto wameshakabidhi report kwa Jakaya Kikwete naye ameamuaa kuikalia kama vile alivyofanya kwenye EPA, je kuna haja ya kumlaumu Zitto katika hili?

Mimi bado ninampa Kikwete siku 30 za bashing free posts ili nione kama kweli anaipenda hii nchi kama anavyodai au ni usanii tu kama ambavyo imekuwa inaonekana so far!
 
Nipo na wananchi na nitaendelea kuwa na wananchi. Siwezi kutoa taarifa za kamati kabala ripoti haijakabidhiwa. Vuta subira. Inabidi nitumie busara na hekima. Tusubiri ripoti. Tuemjibu maswali mengi zaidi ya hayo maana hatukuangalia Buzwagi tu, bali mikataba yote na kutoa mapendekezo ili nchi ifaidike na madini yetu.

Hapo juu ni kauli ya Mh Zitto!

Kipi ni kipi Mwafrika wa Kike?

Zitto si yuko huku na wala hata hazungumzii tena mambo ya madini ambayo ndo yaliyompa umaarufu alionao?

Is this man still our own?
 
Where should i stand Mwafrika wa Kike?
 
Isitoshe Mh. Zitto hakuwa mwenyekiti wa kamati ile, alikuwa ni mjumbe tu.. Hapa anaiachia democrasia ifanye kazi kwa kutofanya kazi isiyokuwa yake.

jmushi1, unataka upewe information ambayo bado ni classified?? Subir kama mtanzani mwingine.
 
zitto hawezi kuja hapa na kuropokwa yaliyomo ndani ya ripoti kabla haijatoka kwa Rais.

hayo maneno ya zitto ya kuwa ripoti "haijakabidhiwa" ndio yanayotia mushkel kwenye nyoyo za watu. hivi ulikusudia neno hili au ...?
 
Hapo juu ni kauli ya Mh Zitto!

Kipi ni kipi Mwafrika wa Kike?

Zitto si yuko huku na wala hata hazungumzii tena mambo ya madini ambayo ndo yaliyompa umaarufu alionao?

Is this man still our own?

Amesema kuwa Report haijakabidhiwa kwa nani? Na alisema hayo lini? Sijaribu kumtetea Zitto hapa kwani yeye mwenyewe huwa yuko hapa kujieleza. Ninaelewa kitu kimoja though, ni vigumu sana kwa Zitto kuongelewa hii report kama Kikwete hajaamua kuitoa kwa wananchi.

Kuhusu Zitto kuwa hapa US, nadhani inajulikana kabisa kuwa Zitto yupo hapa kufanya nini na kwa mwaliko wa nani. Hata hivyo kwa yale anayoweza kusema, Zitto ameongelea mengi kwa kiasi kikubwa katika settings kidogo alizopata kukutana na watanzania hapa kuhusu mambo ya madini.

Kuhusu Zitto kuwa your own, hilo nitakuacha mkuu ufanye your own call!
 
Isitoshe Mh. Zitto hakuwa mwenyekiti wa kamati ile, alikuwa ni mjumbe tu.. Hapa anaiachia democrasia ifanye kazi kwa kutofanya kazi isiyokuwa yake.

jmushi1, unataka upewe information ambayo bado ni classified?? Subir kama mtanzani mwingine.

Jibu hizo posting hapo juu whether imeshakabidhiwa or not?
Zitto kasema hivi and then the reality inasema vingine!
Huoni kuna
kauli kanganyifu hapo juu?

Nasema wiki ilishapita na sasa we're on it!
 
Amesema kuwa Report haijakabidhiwa kwa nani? Na alisema hayo lini? Sijaribu kumtetea Zitto hapa kwani yeye mwenyewe huwa yuko hapa kujieleza. Ninaelewa kitu kimoja though, ni vigumu sana kwa Zitto kuongelewa hii report kama Kikwete hajaamua kuitoa kwa wananchi.

Kuhusu Zitto kuwa hapa US, nadhani inajulikana kabisa kuwa Zitto yupo hapa kufanya nini na kwa mwaliko wa nani. Hata hivyo kwa yale anayoweza kusema, Zitto ameongelea mengi kwa kiasi kikubwa katika settings kidogo alizopata kukutana na watanzania hapa kuhusu mambo ya madini.

Kuhusu Zitto kuwa your own, hilo nitakuacha mkuu ufanye your own call!

Sijazungumza on behalf of Zitto!
Whats this?

Quote:
Zitto

Nipo na wananchi na nitaendelea kuwa na wananchi. Siwezi kutoa taarifa za kamati kabala ripoti haijakabidhiwa. Vuta subira. Inabidi nitumie busara na hekima. Tusubiri ripoti. Tuemjibu maswali mengi zaidi ya hayo maana hatukuangalia Buzwagi tu, bali mikataba yote na kutoa mapendekezo ili nchi ifaidike na madini yetu.
 
Isitoshe Mh. Zitto hakuwa mwenyekiti wa kamati ile, alikuwa ni mjumbe tu.. Hapa anaiachia democrasia ifanye kazi kwa kutofanya kazi isiyokuwa yake.

jmushi1, unataka upewe information ambayo bado ni classified?? Subir kama mtanzani mwingine.

If thats the case then kwanini kamati ya bunge haikupewa nafasi?

Hii issue ni ya Zitto na Rais ama ni ya everybody?(Taifa)
 
Sijazungumza on behalf of Zitto!
Whats this?

Quote:
Zitto

Nipo na wananchi na nitaendelea kuwa na wananchi. Siwezi kutoa taarifa za kamati kabala ripoti haijakabidhiwa. Vuta subira. Inabidi nitumie busara na hekima. Tusubiri ripoti. Tuemjibu maswali mengi zaidi ya hayo maana hatukuangalia Buzwagi tu, bali mikataba yote na kutoa mapendekezo ili nchi ifaidike na madini yetu.

Mkulu Jmushi,

Nadhani inafahamika hapa for a while kuwa report ilishakabidhiwa kwa JK. Ndio maana nimekuuliza swali kuwa Zitto alimaanisha kuwa report haijakabidhiwa kwa nani? - kwa wananchi au kwa JK?

Kama alimaanisha kuwa haijakabidhiwa kwa JK basi hiyo inazua utata mkubwa sana. Kama alimaanisha kuwa haijakabidhiwa kwa watanzania (haijatolewa?) basi huo ni ukweli kuwa hii report haijatolewa hadharani kwa watanzania ingawa sources za JF zinayo hii report in full.
 
If thats the case then kwanini kamati ya bunge haikupewa nafasi?

Hii issue ni ya Zitto na Rais ama ni ya everybody?(Taifa)

Hii issue ni ya taifa na ndio maana taifa zima la watanzania linamsubiria Kikwete atoe hadharani yote yaliyomo kwenye hii report.

Kama unataka Zitto atoe hii report kwa upande wake bila kumsubiria Kikwete, basi unaweza tu kusema hilo pia mkuu na Zitto akatoa majibu kwenye hilo.
 
Mkulu Jmushi,

Nadhani inafahamika hapa for a while kuwa report ilishakabidhiwa kwa JK. Ndio maana nimekuuliza swali kuwa Zitto alimaanisha kuwa report haijakabidhiwa kwa nani? - kwa wananchi au kwa JK?

Kama alimaanisha kuwa haijakabidhiwa kwa JK basi hiyo inazua utata mkubwa sana. Kama alimaanisha kuwa haijakabidhiwa kwa watanzania (haijatolewa?) basi huo ni ukweli kuwa hii report haijatolewa hadharani kwa watanzania ingawa sources za JF zinayo hii report in full.

Hapo inabidi awe specific na hatuhitaji politics hapo!

Naomba nieleweshwe!

Na ndio maana nikasema kuwa kauli ni kanganyifu!
 
Back
Top Bottom