Mama Killango Jitoe Ccm Kama Wewe Ni Mkweli!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,705
21,907
Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!

Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.

Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!

Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!

Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.

Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.

Ni hayo tu kwasasa...
 
J1Mushi unaona Mrema alifanya uamuzi wa busara alipotoka CCM???!!! Sidhani kama ukitoa mfano wa Mrema utaweza kumconvice mama Malecela kutoka CCM!
 
J1Mushi unaona Mrema alifanya uamuzi wa busara alipotoka CCM???!!! Sidhani kama ukitoa mfano wa Mrema utaweza kumconvice mama Malecela kutoka CCM!

Wananchi sasa hivi hawaitaki tena ccm..Si kama wakati ule wa zamani walileta UKABILA!

UKABILA HAUTATUFIKISHA MAHALI NA SERIKALI INAUKUMBATIA TOKA ENZI ZA MWALIMU!

Hawezi kubaki ccm na kufanya chochote kwasababu hata Mwenyekiti wao keshasema hakuna mafisadi humo...Jambo ambalo ni kinyume na mitizamo yenye mwelekeo wa kizalendo halisi.

NB:Naomba pia u concentrate kwenye sababu nilizozitoa za ni kwanini ajitoe
 
Atoke CCM ili aende chama gani?
Hilo ni swali la kuniuliza mimi?
Je anasapoti mgombea binafsi?
Data ziko na tutawachambua wote..Yeye aweke wazi,ama kuwe na kura ya maoni uone kama wananchi hawatasema atoke uko!
Na hivyo vyama vya siasa vinajulikana..So kabla hajaamua kujiunga na chama chochote kama akiamua kufanya hivyo..Then avifanyie uchunguzi.
 
Wananchi sasa hivi hawaitaki tena ccm..Si kama wakati ule wa zamani walileta UKABILA!
UKABILA HAUTATUFIKISHA MAHALI NA SERIKALI INAUKUMBATIA TOKA ENZI ZA MWALIMU!
Hawezi kubaki ccm na kufanya chochote kwasababu hata Mwenyekiti wao keshasema hakuna mafisadi humo...Jambo ambalo ni kinyume na mitizamo yenye mwelekeo wa kizalendo halisi.

Hoja yako inaweza kuwa sahihi au la kutokana na mwongozo utakaoutoa Jmushi1. Tunapomshauri mtu atoke mahala pamoja ni vyema tukampa ushauri wa pa kuelekea.

Halafu hiyo sentensi kwamba wananchi hawataki CCM nadhani haiko factually correct, kwanza huna uwezo wa kujua wanachotaka wananchi na pili wananchi wenyewe wameshaprove hiyo kauli wrong several times na soon itakufa fursa nyingine kwa wananchi kutoa sauti yao(uchaguzi 2010) tungoje kusikia sauti watakayoitoa. Naomba nikukumbushe kitu ambacho nilishakwambia awali : KILA MTANZANIA ANA KURA MOJA.
 
respect mkuu

nashkuru kwa no. ya simu nilipata bahati ya kumpigia mama k, kumpa moyo na kumuunga mkono.

kama kawaida alipokea simu yangu kama mtumishi yeyote wa umma, kwa unyenyekevu na usikivu mkubwa bila ya kuwa na kujisikia km baadhi yetu wakishaupata uheshimiwa na kuona hawawezi kuzungumza na watu wadogowadogo.

long live the struggle 4 fighting against 'mafisadi'.
 
Tunataka kumwamini lakini chama ndiyo shida!
Atapigana vipi na majambazi ya EPA AMBAO NI ccm yake?
 
Hopefully ulimpa huu ushauri mkuu kwasababu sioni ni kivipi ccm ni chama cha wazalendo wakati wameshindwa kuwakamata baadhi ya wanachama wao MAFISADI waliozikwapua pesa za watanzania na kuzifuja kwa KUFRU!
 
Tunataka kumwamini lakini chama ndiyo shida!
Atapigana vipi na majambazi ya EPA AMBAO NI ccm yake?

Recall mazungumzo yake na Mwanakijiji, yeye haamini kuwa chama ni tatizo. Mimi pia siamini kuwa chama ni tatizo kama jinsi asivyoamini mh. Zitto Kabwe pia.belief tunayoshare mimi, mama Malecela na Zitto katika hili ni kwamba tatizo ni tabia za watu.Hivyo basi mabadiliko yatapatikana iwapo kutakuwa na checks and control on the missuse of power by individuals.
 
Huoni kuwa kufanya majadiliano ya mustakabali wa TAIFA hakuitaji kuwashirikisha MAFISADI?
Huoni kuwa ccm wameshatoa kauli kuwa hakuna mafisadi ccm na wala hakuna atakayekamatwa kwasababu eti inasemekana ballali kafa?
Mambo makuu muhimu tufanye sasa hivi watanzania...Tudai ripoti ya EPA na tusimamie mijadala ya mahojiano dhidi ya mafisadi na huku tukifanya comparison na ripoti zote za uchunguzi!
Pia naomba tena urudi kwenye posting yangu ya kwanza hapo juu nilipofungua hii thread na kusema ni kwanini ccm haiwezi kumpatia mtanzania haki dhidi yake yenyewe!
Tatizo ni kwamba anajua mipesa iliyoko humo ccm na anaogopa hilo..Yaliyomkumba MREMA Ndio kujitolea kwenyewe huko!
 
Mafisadi hawafai kushirikishwa katika kujadili mustakabali wa taifa and they belong in prisons lakini ni muhimu kupata jibu la swali hili: who is fisadi? the notion that being out of CCM is being non-fisadi is something I just cant agree.
 
Tusisahahu haya maneno ya wenye uchungu na TAIFA LAO!

Na Dunstan Bahai

``...Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni, na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. Tumekuwa yatima waliofiwa na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.

Tunakunywa maji yetu kwa fedha, kuni zetu twauziwa.

Watufuatao wako juu ya shingo zetu, tumechoka tusipate raha yoyote Baba zetu walitenda dhambi hata hawako, na sisi tumeyachukuwa maovu yao. Watumwa wanatutawala, hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.

``Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu, kwa sababu ya upanga wa nyikani. Ngozi zetu ni nyeusi kama tanuu, kwa sababu ya hali ya njaa ituteketezayo Wakuu hutungikwa kwa mikono yao, nyuso za wazee hazipewi heshima.

``... Wazee wameacha kwenda langoni, na vijana kwenda ngomani. Furaha ya mioyo yetu imekoma, michezo yetu imegeuka maombolezo.

``Mbona watusahau siku zote, na kutuacha muda huu mwingi. We Bwana, utugeuze kwako nasi tutageuka, zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. Isipokuwa wewe umetukataa kabisa, nawe una hasira nyingi sana juu yetu,`` hayo ni baadhi maneno ya Bibilia yanayopatikana kwenye kitabu cha Maombolezo sura ya 5:1-22.

Nimelazimika kunukuu sehemu hiyo ya Biblia kama kitabu kitakatifu, kuonyesha maonyo yaliyotolewa wakati wa zamani na dhuluma iliyopo sasa duniani, hasa katika nchi maskini na zile zinazoendelea, dhuluma zinazofanywa na baadhi ya watawala wake.

Katika kipindi cha takribani miaka miwili na miezi minne hivi, Watanzania na Walimwengu kwa ujumla, wameshuhudia viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya nne wanavyoachia nyadhifa zao.

Hatua hiyo ya viongozi kuachia nyadhifa zao haimaanishi wamehusika na tuhuma zinazoenezwa juu yao, bali ni ishara ya heshima na uwajibikaji.

Hatuwezi kuwahukumu viongozi hao kuwa `walivaa ngozi ya kondoo`, huku wakijijua ni `mbwa mwitu` bali walionyesha mfano mzuri wa kuwajibika ingawa wapo wengi wa aina hiyo wanaotakiwa kufuata nyayo zao.

Kuwajibika si dhambi, wala kuwajibika si aibu bali kama kiongozi, anazidi kujijengea heshima.

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, anatanabaisha kwamba baada ya Tanzania kupata Uhuru, uongozi wa wakati huo ulikuwa ukitegemea Rais zaidi.

Hata hivyo, alikiri kuwa viongozi wa wakati huo walikuwa na maadili makubwa ikilinganishwa na wa sasa.

Alisema mtu mbadhirifu au aliyepatikana na rushwa, alikuwa hana nafasi wala sifa ya kuendelea kuwa kiongozi, kwani Rais, wakati huo hayati Mwalimu Julius Nyerere, hakusita kumchukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kumfukuza kazi moja kwa moja.

``Wakati huo ilikuwa amri moja tu kwa kiongozi asiye na maadili. Zamani kiongozi akiitwa Ikulu anatetemeka, anajua akirudi hana kazi, ni kiama kwake, lakini sasa hivi mambo tofauti.`` alisema.

Alisema kipindi cha awamu ya kwanza, kulikuwa na matukio mengi ya viongozi kujiuzulu, kufukuzwa na kustaafishwa kazi.

Miongoni mwa tukio la kujiuzulu kwa kuwajibika ni la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kutokana na makosa yaliyotokea katika wizara yake.

Katika serikali ya sasa viongozi wengine walioachia ngazi zao kwa uwajibikaji mapema mwaka huu ni aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge.

Hata hivyo, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Daud Balali, alifukuzwa kazi ingawa ni baada ya kumuandikia Rais kuwa ameamua kujiuzulu.

Uwajibikaji ni sehemu ya uadilifu, nidhamu na kujijengea heshima ndani ya familia ya anayewajibika, lakini zaidi nje ya familia yake na nje ya mipaka ya nchi, kwani kiongozi anaonyesha kujutia kilichotokea akiwa kiongozi katika eneo lake, lakini kujiuzulu kwa shinikizo la umma, hilo halimletei heshima kiongozi.

Kwa mujibu wa Profesa Baregu, kumekuwa na matukio mengi ya ubadhirifu, hali ambayo imewaudhi wananchi hadi kufikia umma huo kuchukia kudanganywa huku mali zao wakishuhudia zikiporwa.

Profesa Baregu alisema shinikizo la nguvu ya umma limechangia kuibuka kwa mambo mengi maovu.

Pia alivipongeza vyama vya upinzani hasa ushirika wa vyama vinne vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

Alisema vyama hivyo kwa kushirikiana na umma wa Watanzania, waliweza kufanikiwa kuufikisha ujumbe, kilio chao cha kuporwa mali zao, na matokeo yalijidhihirisha na kwa upande mwingine serikali imeonyesha nia ya kushughulikia malalamiko hayo.

Hatua iliyofikiwa na serikali ya kuanika uozo uliojitokeza, ni hatua muhimu sana na ya kuungwa mkono na wananchi wengi, hicho ndicho kilichokuwa kikisubiriwa na umma wa Watanzania.

Aidha, hatua hiyo itairejesha heshima na imani ya Watanzania kwa uongozi wa Taifa na mihimili yote ya nchi.
Naye Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katholiki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methedius Kilaini, ameonyesha kukerwa na watu wanaohusika na ufisadi.

``Mimi simjui fisadi, lakini ninachukia sana hali hiyo. lakini nimeridhika jinsi suala hili lilivyoibuliwa, kwani haya mambo yalikuwepo tangu enzi za mababu, lakini, nani awe wa kwanza kumfunga paka kengele,`` alisema.

Aliwashauri Wabunge, kutokana na ujasiri wao kuliibua suala hili na kulizungumzia kwa kina, waendeleze jitihada hizo hadi mafisadi watakapojulikana na kufikishwa mahakamani, kwani huko wananchi watakapowajua na kupata haki yao.

Askofu Kilaini alikuwa akimaanisha, huwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni fisadi, kwani wengi wanaamini viongozi wote waliojiuzulu ni mafisadi, la hasha, hao walifanya hivyo kama sehemu ya uwajibikaji, kwani tuhuma hizo zimeibuka wakati wao wakiwa ni viongozi wa maeneo yanayotuhumiwa.

Kwa maana hiyo, uchunguzi unaofanywa na serikali katika maeneo hayo wananchi wanaamini utawaibua mafisadi, pengine ni wale waliojiuzulu kwa heshima au wengine.

Inawezekana kabisa, Rais Kikwete ana dhamira ya kweli ya kuwaondolea umaskini na kero zote zinazowakabili wananchi, lakini wapo wanaokwenda kinyume na dhamira hiyo.

Hata hivyo kuna dalili yawezekana Rais Kikwete ameonyesha kukerwa na ufisadi pamoja na rushwa, ndiyo maana alishindwa kulitolea maamuzi suala hilo na badala yake ameviachia vyombo vya dola kulishughulikia, na Watanzania wanasubiri kwa hamu sana matokeo ya uchunguzi huo.

Kumekuwa na maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi na viongozi wa dini, juu ya nini kifanyike kwa wale wote watakaobainika kuhusika na kupora mali za Watanzania.

Pia yapo maoni yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuchunguza tuhuma za Richmond.

Baadhi ya maoni ya wananchi na viongozi wa dini ni serikali kuwachukulia hatua haraka wale wote wanaodhani ni mafisadi ikiwa ni pamoja na kufilisi mali zao.

Maoni hayo ni ya haraka sana, tunaamini hakuna mtu anayemfahamu fisadi, cha msingi ni wananchi kuwa na subira, kusubiri uchunguzi unaoendelea wa vyombo vya dola.

Cha msingi ni vyombo hivyo kufanyakazi yake kwa umakini na ukweli na uwazi ili Watanzania waendelee kujenga heshima kwa serikali yao ya awamu ya nne na hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili suala hili lisiendelee kuwa mjadala, tena mjadala wa kutoaminiani, dhamana ya ukweli wa mambo yenyewe iko mikononi mwa vyombo vilivyoteuliwa na serikali katika kuchunguza masuala hayo.

Vyombo hivyo visipofanyakazi yake kwa makini na ukweli, viongozi waliojiuzulu nyadhifa zao hawatakwepa hasira za wananchi, na maisha yao yatakuwa juu ya mikono ya Watanzania.

Watanzania kama kawaida yao ni wapole, hivyo upole wao usichukuliwe kama ni mazuzu.

Tanzania ni yetu, hakuna mgeni atakayetutengenezea amani na utulivu, kwani suala hili likichukuliwa kwa jazba, urithi wa amani yetu utabakia kama historia, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
 
Pesa za EPA zilizoibiwa na ccm ni kosa la jinai na waache siasa mara moja!

Hakuna haja ya Said Mwema kuingiliwa kazi za uchunguzi wa jinai!
Alidai ameogopa kuwakamata mafisadi na wakati Rais alishamwambia afanye hivyo!

Siasa iwekwe kando kwenye kesi za jinai!

Kauli za kina Mkullo,Makamba na wengineo zinatuchanganya tu!

Licha ya kwamba ballali alipotea ama kufa..Haina maana kuwa na kesi nayo imekufa...Watanzania daini ripoti muone jinsi ilivyo wazi kuwa ni nani wa kukamatwa..MSIKUBALI WATANZANIA!

BODI YA WAKURUGENZI YA BOT NAO NI WATUHUMIWA TU!
KUDAI BALLALI KUFA NI KUFA KWA KESI NI KAULI ZA KISIASA KWANI RIPOTI HAIONYESHI KWA THATS THE CASE!

KESI YA KUJIBU BADO IPO,NA WATUHUMIWA PIA WAPO!

HATA HATUTAKUWA NA HAJA YA BALLALI..KWASABABU UTARATIBU WA KUSAINI DOCUMENT UNAWAFANYA WASAIDIZI WAKE AMBAO WENGINE BADO WAKO BOT..KWA WATUHUMIWA!

DDD,DEP NA DF WANA UMUHIMU KAMA WA BALLALI TU NA KUFA KWA BALLALI HAKUNA MATATIZO YA KISHERIA BALI YA KISIASA NA NDIO MAANA ccm WANAIFANYA ISSUE YA EPA KUWA YA KISIASA BADALA YA KUWA YA KISHERIA KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA NI UJAMBAZI ULIFANYIKA!

Mama ajiunge upande wa haki mara moja ili tuache kubishana mambo yaliyoko wazi!

Nawashauri ndugu zangu mukasome ile ripoti ya EPA na mtaujua ukweli..Nilijaribu kuitafsiri lakini sijaimalizia yote..Nimeisoma yote na nimeamua kudeal na issue hii ili haki yetu iapatikane!

Balali hana ujanja!

2008-05-09 19:21:02
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Licha ya Serikali kutoa taarifa inayodai kuwa hivi sasa haimtafuti aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Dokta Daudi Balali ambaye inasemekana amejichimbia Marekani, baadhi ya wanasiasa nchini wanasema, msomi huyo hana ujanja na kinachotakiwa ni kumrejeshwa nchini fasta fasta ili aeleze ni vipi mabilioni ya Watanzania yalichotwa na kuliwa hivihivi.

Imeelezwa kuwa kinachotakiwa kufanyika ni uchunguzi kuendelea kufanywa huku mtuhumiwa akiwa tayari ametiwa mikononi mwa dola kama inavyofanyika kwa watuhumiwa wengine wa makosa mbalimbali.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha,CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, amesema sheria ya Tanzania kuhusu makosa ya jinai iko wazi na kamwe haichagui mtu na wala haiangalii hali yake kuwa ni tajiri au maskini.

Akasema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtuhumiwa wa makosa ya jinai anapaswa kukamatwa, kufunguliwa jalada polisi na kisha uchunguzi wake kufanywa wakati mtuhumiwa akiwa nyumbani kwa dhamana au rumande.

Dk. Slaa amesema sheria inasema kesi ambayo hairuhusu mtu kukamatwa au kufungwa ni ya madai pekee.

\"Tuhuma zinazomkabili Dk. Balali ni za wizi wa mabilioni ya fedha... hilo ni kosa la jinai.

Sasa kwanini asitafutwe na kukamatwa? Sasa wanaposema wanachunguza, watafanya hivyo kwa RB ipi?\" akahoji Dk. Slaa.

Amesema kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria ni kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi, kuwafungulia RB polisi na kisha uchunguzi kufanyika wakati watuhumiwa wakiwa rumande au wakiwa nje kwa dhamana.

Jana Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Bw. Balali ametoweka na hajulikani alipo.

Hata hivyo, taarifa zilizotolewa jana kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu Bw. Salva Rweyemamu, zimedai kuwa hivi sasa, Serikali haina shida na Dk. Balali na kwamba itamtafuta wakati utakapowadia baada ya uchunguzi wa sakata lake kukamilika.

Dk. Balali alipigwa chini na Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete baada ya ripoti ya mkaguzi wa hesabu za BOT, kampuni ya ukaguzi ya kimataifa ya Ernst & Young, kubaini kuwa kuna mapesa mengi yametumika visivyo wakati akiiongoza taasisi hiyo.
Kashfa kubwa iliyotikisa nchi na kumfanya Balali apigwe chini na Rais ni ile ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh. Bilioni 133 za BOT, ambazo zililipwa isivyo halali kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje, EPA.
  • SOURCE: Alasiri
 
Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!

Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.

Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!

Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!

Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.

Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.

Ni hayo tu kwasasa...

Huyu mama namshukuru kwa kutusemea wananchi huko bungeni. Ana uchungu na wananchi, lakini akakubali kupitisha bajeti ambayo ilikuwa na mapungufu kibao. Kama ni mkweli ahame sisiemu, kuna vyama vingi tu ambavyo anaweza jiunga navyo kuithibitisha dhamira yake kwa watanzania.
 
Mimi nadhani huyu mama ana ajenda yake. Just give her sometimes na mtaona ukweli wake. She is very ambitious, she is vying for a seniour post! Hivi unapigia kelele EPA kila siku hata pale ambapo unajua kuwa muda wa Timu ya Rais unakariia kuisha? Kwanini asiangalie bajeti ina mapungufu gani na asubiri ripoti ili aseme hili. Alichotaka ni publicity, and believe me amepata wa kutosha.
 
Mushi,

Walikuwepo kina Njelu Kasaka, Lumuli Kasyupa, Augustino Mrema, Sefu Hammad na wengine wengi ambao walitoka CCM wakaenda Upinzani na tangu wahamie huko, hawajawa na uwezo wa kuleta mtikisiko wowote wa kubadilisha mawazo ya Watanzania kuwa wao Upinzani ni bora kuliko CCM.

Sasa kama Mama Kilango Malecela atajitoa, ajitoe aende wapi? aanzishe chama kipya au akagombane na kina Lipumba, Mrema, Cheyo, Mbowe na Mtikila kutoaka kugombea madaraka na kuuza njozi kama sera?

Unasema Mama Kilango Malecela atetee Mgombea Huru. Huyu Mgombea huru ana sera gani na wafuasi gani kwa Itikadi gani ambayo itaweza kusaidia kubadilisha sura ya nchi yetu na kuanza kuleta tumaini?

Mimi nafikiri alichokifanya sasa hivi kwa kuwa mkweli ndani ya CCM ni jambo la kupongezwa sana na tungetaka aendelee kubakia ndani ya CCM awe mwiba mkali ambao utawazindua CCM na kuhakikisha kuwa wale CCM ambao ni CCM Utaifa, wanakuwa na nguvu na hata kushika hatamu za Uongozi wa Chama chao na kisha kuleta mabadiliko ndani ya CCM ambayo yataumaliza ufisadi.

Akifanya kosa kama la Mrema kukurupuka na kuondoka na kuelekea Upinzani bila kuwa na mwelekeo, ataishia kuwa mvuke kama Mrema na kuishiwa nguvu.

Kitu kimoja ambacho sijui kama unakielewa vizuri kuhusu Siasa za Tanzania na historia yake, CCM ni Chapa iliyokomaa mawazoni mwa Wananchi (Brand Name). Ni Taasisi iliyojijenga kwa uimara mkubwa sana kuliko wengi mnavyofikiri. Kazi ya kuingoa CCM ni kubwa. Tatizo la CCM si Chama kama Taasisi, bali ni wanachama wachache ambao wana nguvu za ushawishi, wana fedha na wana madaraka ambayo wanayatumia vibaya kwa manufaa binafsi na washiriki wao Mafisadi.

Kama upinzani na uwezo wa kusema kweli ndani ya CCM umeanza na Mama Kilango Malecela, halafu kina Aloyce Kimaro, Lazaro Nyalandu, Harrison Mwakyembe, Lucas Seleli, Stella Manyanya, William na Beatrice Shelukindo, Ole Sendeka na wengine wataanza kujiamini na kujitutumua kuzidi zile nguvu za jeuri ya Chama, basi hapo kuna matumaini.

Kuhama CCM mtu mmoja mmoja bila kuwa na dira au sera kisa msimamo wangu ni tofauti au sikubaliani nao, kutakuwa sawa na kutaka kuwasha mshumaa kando ya bahari yenye tufani la Tsunami.
 
Halafu hawa ccm kweli wanafikiri sisi hatuna akili kabisa...Ebu cheki hii kauli ya huyo mkullo...Walidhamiria kabisa kuigeuza kesi ya jinai kuwa siasa!
UCHUNGUZI WA NINI NA WAKATI KWENYE RIPOTI ZA UKAGUZI KUNA MAJINA NA SAINI ZA MAJAMBAZI?
Eti sirikali haijui alipo kwani katoweka..Tulipowauliza wamarekani huyu mtu atatoweka vipi..Wakadai kikwete hamtaki arudi TZ,Hatukuweza kumwuliza ballali kuhusu hilo lakini ni wazi walidili na bado wanadili na hii issue kisiasa siasa!
Sasa ghafla wakaona ballali hana ujanja...MARA AKAFA/KUPOTEA MOJA KWA MOJA!
Huku taarifa za yeye kufa HURU zikisambaa kwa kasi!
WAKATI WA MUNGU NI HUU...MAMA TOKA HUMO ccm!
Hata hivyo, taarifa zilizotolewa jana kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu Bw. Salva Rweyemamu, zimedai kuwa hivi sasa, Serikali haina shida na Dk. Balali na kwamba itamtafuta wakati utakapowadia baada ya uchunguzi wa sakata lake kukamilika.
 
Mama Kilango ingekuwa vyema kama pia ungepigia kelele ufisadi unaotokea katika mahospitali yetu, kuna watu wanakufa kwa kukosa elfu tano ya kumpa nesi ili aongezewe damu, kuna watu wanafia hospitali kisa hawana vifaa vya kujifungulia, wananchi wanashindwa kusafirisha mazao yao kwa ajili ya kukosa miundombinu bora itakayowaunganisha na masoko ya mazao yao mijini, Je hili sio la kulipigia kelele kuliko hilo suala la EPA? Je hii ni nguvu ya soda kutuzuga wadanganyika tunyamaze kusema kuhusu mengine?

Nilidhani hapatakalika pale ambapo bajeti ilionekana ina mapungufu mengi sana na waziri wa fedha kuonekana incompetent hadi asaidiwe? Je mama hili kwake lilikuwa halina haja ya kupigiwa kelele?
 
Mushi,

Walikuwepo kina Njelu Kasaka, Lumuli Kasyupa, Augustino Mrema, Sefu Hammad na wengine wengi ambao walitoka CCM wakaenda Upinzani na tangu wahamie huko, hawajawa na uwezo wa kuleta mtikisiko wowote wa kubadilisha mawazo ya Watanzania kuwa wao Upinzani ni bora kuliko CCM.

Sasa kama Mama Kilango Malecela atajitoa, ajitoe aende wapi? aanzishe chama kipya au akagombane na kina Lipumba, Mrema, Cheyo, Mbowe na Mtikila kutoaka kugombea madaraka na kuuza njozi kama sera?

Unasema Mama Kilango Malecela atetee Mgombea Huru. Huyu Mgombea huru ana sera gani na wafuasi gani kwa Itikadi gani ambayo itaweza kusaidia kubadilisha sura ya nchi yetu na kuanza kuleta tumaini?

Mimi nafikiri alichokifanya sasa hivi kwa kuwa mkweli ndani ya CCM ni jambo la kupongezwa sana na tungetaka aendelee kubakia ndani ya CCM awe mwiba mkali ambao utawazindua CCM na kuhakikisha kuwa wale CCM ambao ni CCM Utaifa, wanakuwa na nguvu na hata kushika hatamu za Uongozi wa Chama chao na kisha kuleta mabadiliko ndani ya CCM ambayo yataumaliza ufisadi.

Akifanya kosa kama la Mrema kukurupuka na kuondoka na kuelekea Upinzani bila kuwa na mwelekeo, ataishia kuwa mvuke kama Mrema na kuishiwa nguvu.

Kitu kimoja ambacho sijui kama unakielewa vizuri kuhusu Siasa za Tanzania na historia yake, CCM ni Chapa iliyokomaa mawazoni mwa Wananchi (Brand Name). Ni Taasisi iliyojijenga kwa uimara mkubwa sana kuliko wengi mnavyofikiri. Kazi ya kuingoa CCM ni kubwa. Tatizo la CCM si Chama kama Taasisi, bali ni wanachama wachache ambao wana nguvu za ushawishi, wana fedha na wana madaraka ambayo wanayatumia vibaya kwa manufaa binafsi na washiriki wao Mafisadi.

Kama upinzani na uwezo wa kusema kweli ndani ya CCM umeanza na Mama Kilango Malecela, halafu kina Aloyce Kimaro, Lazaro Nyalandu, Harrison Mwakyembe, Lucas Seleli, Stella Manyanya, William na Beatrice Shelukindo, Ole Sendeka na wengine wataanza kujiamini na kujitutumua kuzidi zile nguvu za jeuri ya Chama, basi hapo kuna matumaini.

Kuhama CCM mtu mmoja mmoja bila kuwa na dira au sera kisa msimamo wangu ni tofauti au sikubaliani nao, kutakuwa sawa na kutaka kuwasha mshumaa kando ya bahari yenye tufani la Tsunami.

Nashukuru kwa maoni yako lakini this time around there is an EXTREMELY DIFFERENT SITUATION HENCE DEFINING MOMENT IN THE HISTORY OF OUR COUNTRY AND MAYBE THE WORLD!
Kuna mwamko wa tofauti miongoni mwa wananchi mchungaji fanya uchunguzi utajua hilo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom