Sidhani kuwa kuna ukweli kwani TTCL hawahusiki kabisa na hilo! Wanaohusika ni TCRA! Kama CDM wameingia mkataba na TTCL wametapeliwa!!
Mkuu hapo kwenye red huitwa boiling strategy. Serikali inaweza kweli kufanya mchezo wa namna hiyo?? Sidhani....swali siyo kuwa nayo; swali ni je wasikilizaji/watazamaji wataunga mkono wadhamini na kuwa tayari kulipia gharama ya kuendesha? Maana kama mashirika makubwa yatajikuta hayawezi kutangaza biashara zao humo media ya aina hiyo inaweza kujikuta inakufa kifo cha kutegewa.
Kwaiyo busara zimekutuma kudhani kuwa CDM wameingia mkataba na TTCL bila kupita TCRA?Ninahusika na na taaluma na idara hiyo kwa hiyo nasema kitu nilicho na hakika nacho 100%
sijui walikuwa wapi muda wote huu
kwani vyombo ulivyovitaja hapo juu vimefanya nini?au ndo kale kautaratibu ka kupinga serikali na vyombo vyake bila sababu za msingi na kutaka kuwaaminisha watu wasiojielewa kwamba serikali ni chombo cha kuwanyonya na kuwakandamiza?Kama ni propaganda hawa ndio wakongwe...TBC, Habarileo, Uhuru n.k mbona hukutoa angalizo?
ccm wameleta danadana gani?Tunawatakia kila la heri cdm, tunataka usawa katika demokrasia tanzania kama ccm wana redio uhuru, nao cdm wawe nayo ya kwao ili watanzania waamue siku ya mwisho nani wa kumpa uongozi wa taifa letu! Ila katika hili watimize wasilete danadana kama ccm!
hivi kumbe vinavyofungiwa ni vile vinavyoandika habari za ukweli ee! kama lile gazeti lililoandika "waziri anaswa akiwanga" Au lile lililoandika "Njama za kumpindua kikwete zagundulika;mpango kuongozwa na ridhiwani". hakika yeyote atakayekuwa anatoa taarifa za kipuuzi kama hizi serikali isipomfungia itakuwa imefanya dhambi kubwa mno!Kwa hili ni sawa lakini sijui wamejipanga vipi na ukiritimba wa serikali ya CCM dhidi ya kufungia vyombo vya habari vinavyojaribu kutoa na kuandika habari za ukweli na uwazi? Bado kazi ipo inabidi wajipange kisawasawa wasijekaa hewani kwa sekunde.
Mkuu wewe upo dunia ipi?kwani vyombo ulivyovitaja hapo juu vimefanya nini?au ndo kale kautaratibu ka kupinga serikali na vyombo vyake bila sababu za msingi na kutaka kuwaaminisha watu wasiojielewa kwamba serikali ni chombo cha kuwanyonya na kuwakandamiza?
ukikichukia kitu hatimae utakuwa ukifanya unfair judgement.hebu toa mfano tukio ambalo TBC walieneza propaganda chafu.Mkuu wewe upo dunia ipi?
Ugolo mchafu uliooza umekuwa ukitapikwa sana na hivyo vyombo vya CCM na Serikali.
*Vyombo hivyo vimekuwa mstari wa mbele kutotangaza habari muhimu mbaya kwa CCM na serikali, kutoa Coverage ya juu kwa CCM, kuchakachua habari na kueneza propaganda chafu.
*Infact ninaichukia sana CCM na serikali yake kwa namna ilivyowaharibu watanzania katika kufikiri kupitia media hizo.
Mkuu mbona unajihami sana????!!!,ningetoaje angalizo kama hoja hiyo ilikuwa haijatolewa????!!!
Sijui itakuwaje kwa sababu ninachokiona kama kila chama kitaanzisha chombo chake cha habri maana yake ni kwamba propaganda zitakuwa ni za kuwamga badala ya ukweli halisi,hapa lazima kuna kuhamasishana kuvunja amani.Wizara ya habari angalieni hili vinginevyo>>>>>>>>>>>>..........
Sidhani kuwa Gamba ni tatizo,kipendacho roho ni Dawa,naangalia mwelekeo wa siasa namna ulivyo kwa sababu wewe ni mmoja wapo ambaye unashdidia mambo kwa sababu tu eti wewe ni CDM!!!!!!!!!kwa taarifa yako kuna watu ni cdm lakini siku zote wanasimamia ukweli na si ushbiki.
Seikali ya kichwa chako ndo kimekutuma hivyo mimi siko huko!!!!!!!!!!!!!!!!1
Sipendi kuendelea kubishania hilo kwa kuwa utaratibu wa nani ni nani na hatua zipi za kufanya ili mtu amiliki radio au tv ni moja ya kazi zangu za kila siku. Nina hakika na ninachosema 100%. Tusubiri tutaona matokeo ya kupata umiliki wa electronic media kupitia TTCL. Hao wanaomiliki hakuna hata mmoja aliyepitia njia hiyo!!Kirumo usidanganye umma hapa
TCRA ni licence provider
TTCL ni access/network provider kwenye facility yao to mean telecommunication network.
kwa Tanzania na duniani kwa ujumla huwa vyombo vya habari na mawasiliano wanashea network ambayo
mara nyingi inakuwa owned na state hapa namaanisha TTCL kwa Tanzania.Its not easy kwa kila kampuni kujenga
network yao sheria za ushindani haziko hivo.