Hatimaye CCJ chasajiliwa

Sidhani kama hiko ni kigezo cha kuwakataa wanachama kwani ninavyojua mimi muda wa kujiandikisha bado upo, so wangejiandikisha hata baada ya kuwa wanachama.

Labda kama kuna sababu nyingine ya msingi.


Mkuu, labda wanaogopa yasije kuwakuta yaliyomkuta Mrema 1995. Unakumbuka alikuwa anabebwa na watu lukuki ambao hawakuwa wapiga kura!!!

Nawashauri wawe wazi na criteria za scunity ya wanachama ili kuchuja chenga na mchele!!
 
Issue siyo kuanzisha chama kimya, ila ni kujiondoa CCM na kujiunga vyama vilivyopo na kuviimarisha. Hivi hatuoni kwa watani wetu Kenya.
 
Mkuu, labda wanaogopa yasije kuwakuta yaliyomkuta Mrema 1995. Unakumbuka alikuwa anabebwa na watu lukuki ambao hawakuwa wapiga kura!!!

Nawashauri wawe wazi na criteria za scunity ya wanachama ili kuchuja chenga na mchele!!

Ni kweli mkuu,
Lakini pia wangeongeza nguvu na mikoani kwani huko ndo kunako'wacost wapinzani.
Kuna watu huko (mikoani) huwaelezi kitu mbele ya CCM, wamekariri tu kuwa chama ni CCM tu.
 
Mkuu avatar imebadilika tena!!
Ni maneno gani hii kwa Mkuu wetu(Mwanakijiji) kukosa msimamo hivi tena?...Juzi umetupigisha kura wee..leo unaleta maneno mpyaa, ambayo haipo hata kwenye ile mambo ya juzi...Mbona unakuwa double standard Mkuu?..Angalia unatemper na credibility yako Mkuu!
 
Ni maneno gani hii kwa Mkuu wetu(Mwanakijiji) kukosa msimamo hivi tena?...Juzi umetupigisha kura wee..leo unaleta maneno mpyaa, ambayo haipo hata kwenye ile mambo ya juzi...Mbona unakuwa double standard Mkuu?..Angalia unatemper na credibility yako Mkuu!

Kweli mkulu, maana juzi tumepiga kura... nikasema inawezekana kwa kuwa 2010 kuna kazi nzito, ni vizuri kubadili sura na kupambana!!! MMKJ mkuu wetu angalia hili.
 
Jamaa wanatafuta mshiko tu kipindi hiki cha uchaguzi, mbona wasianzishe mapema ili wajipange uzuri kama nia yao ya dhati ni kujipanga kumkomboa Mtanzania?

Ndio wale wale tu kama jina lao linavyojieleza CCJ (sisi je). Baada ya kuona wenzao chama cha mananihii wanakula kiulaini, wakajiuliza 'na sisi je?

Usiwakatishe tamaa wananchi wenzio. Ni haki yao ya kidemokrasia kuanzisha chama na hakuna muda maalum wakati wowote ni ruksa kuanzisha chama. You've said it "mbona wasianzishe mapema ili wajipange uzuri kama nia yao ya dhati ni kujipanga kumkomboa Mtanzania?" Nia ya dhati ya kumkomboa Mtanzania haina muda maalum, watu huamua na kuanza kujipanga wakati wowote wanapoona kufanya hivyo kunahitajika kwa manufaa ya Taifa. CCJ kwa maana yako ya "sisi je?" can mean sisi je kwani hatuwezi kuikomboa nchi yetu; sisi je tunangoja nini kufanya hivyo - wakati ndio huu!
 
Ni maneno gani hii kwa Mkuu wetu(Mwanakijiji) kukosa msimamo hivi tena?...Juzi umetupigisha kura wee..leo unaleta maneno mpyaa, ambayo haipo hata kwenye ile mambo ya juzi...Mbona unakuwa double standard Mkuu?..Angalia unatemper na credibility yako Mkuu!

Mkuu Nilimuomba Mwanakijiji aiweke hii japo kwa Siku moja! This is Mwanakijiji Orijino kaka
 
I smell ukombozi tokana na chama hiki.
Kama kuna mtu alitazama TBC1 LEO katika kipindi cha JAMBO, yule mtangazaji Marina H.Marin anajaribu kukikandia sana chama hiki, wakati msajili Tendwa anajibu very fairly!...Sijui TBC wana hila gani na chama hiki...I HATE THEM!

Watangazaji wanawake wa TBC naweza kusema ni bogus. Jana ama juzi I just happened kusikiliza kipindi sijui ndio kinaitwa 'Mambo Bado' huyo mdada mtangazaji akawa ana-argue kuhusu vyandarua vya hati punguzo vinavyouzwa madukani kwa bei kubwa. Akadai kwamba wapo baadhi ya watu wanalalamikia bei ya vyandarua hivyo madukani bila kujua kwamba haviwahusu vinahusu wajawazito na watoto. She is forgetting that ni haki ya Mtanzania yoyote kutoa mawazo yake pale anapoona jambo haliendi sawa na hili la vyandarua likiwemo regardless mtu ana mimba au ana mtoto mchanga.

Haingii akilini kuambiwa kwamba kuna vyandarua vya hati-punguzo kwa akina mama wajawazito na watoto lakini vyandarua hivyo haviwafikii walengwa tangu wanapoanza kwenda clinic mpaka wanajifungua. Badala yake unavikuta vinauzwa holela madukani bila maelezo wala maelekezo yoyote vikiwa na nembo ya FREE NET by USAID! That bogus mtangazaji said something like 'Wazee mnaolalamikia vyandarua hivyo yanawahusu nini wakati nyie si wajawazito!?'
 
Najaribu kuwa shekhe ubwabwa kwa muda: Kwa mwendo huu wa kudanganyika kirahisi, CCM itatutawala kwa muda mrefu ujao.
 
Najaribu kuwa shekhe ubwabwa kwa muda: Kwa mwendo huu wa kudanganyika kirahisi, CCM itatutawala kwa muda mrefu ujao.

Kudanganyika huku kirahisi kunadhihirisha jambo moja lililo wazi .... kuna mambo yamewachosha hao wadanganyika na wanatafuta afueni, wasipoipata hilo ni jambo jingine!
 
Najaribu kuwa shekhe ubwabwa kwa muda: Kwa mwendo huu wa kudanganyika kirahisi, CCM itatutawala kwa muda mrefu ujao.
Huu uchangamkiaji wa kadi za CCJ unadhihirisha jambo moja tu ambalo watu hawataki kulitilia maanani "Wananchi wa tanzania ni kama kondoo wasio na mchungaji, wamekatishwa tamaa na CCM lakini bado hawajaona option nje ya CCM"; wanabakia kumsubiri masiha atakayekuja....

Vyama vya upinzani visipojirekebisha ili kubeba matarajio ya wananchi hawa wanaotangatanga, CCM itatawala milele unless imeguka yenyewe katika makundi na kuondolewa madaraka na watu walio ndani ya CCM yenyewe.
 
Najaribu kuwa shekhe ubwabwa kwa muda: Kwa mwendo huu wa kudanganyika kirahisi, CCM itatutawala kwa muda mrefu ujao.
I buy your idea nimejifunza mengi tangu NCCR ya 1994 kwa nini watanzania tunakuwa wepesi kukubali jambo! jibu linakuja wengi wamechoshwa na utawala uliopo watanzania ni kama tupo jangwani tunapoona mtu yeyote tunadhani ni masihi inawezekana kweli akawa masihi lakini inawezekana pia likawa dudu mtu lililotumwa kuwaangamiza kumbuka wakati wa NCCR ya Mrema mambo yalikuwa hivi hivi watu kwa mamia tulikimbilia kadi tukidhani mkombozi katelemshwa lakini tusikate tamaa tuchukue kadi ila tuwapime kabla ya kuwapa kura zetu
 
CCK nacho chaja.....Chama Cha Kula....kupata kadi mpaka uwe na msosi mkononi.
 
CCJ yaigusa Marekani

• Balozi nchini akana kuisaidia kifedha, kimkakati

na Waandishi Wetu

KUANZISHWA kwa Chama Cha Jamii (CCJ) kumeendelea kuchochea hali ya mikanganyiko inayotokana na kuwapo kwa taarifa mbalimbali zinazokinzana kuhusu ustawi na mfumo wa uendashaji wake; Tanzania Daima imebaini.

Siku tatu baada ya chama hicho kukabidhiwa cheti cha usajili wa muda kumeibuka taarifa zinazokihusisha chama hicho na misaada kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa mtandao wa kompyuta katika kusaka wanachama 200 kutoka mikoa minane ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar.

Hata hivyo saa chache tu baada ya taarifa hizo kuifikia Tanzania Daima, Marekani, moja ya nchi ambazo zimekuwa zikitajwa chinichini kukisaidia chama hicho, ilitoa tamko la kukanusha kufanya hivyo kwa CCJ na kwa chama kingine chochote cha siasa hapa nchini.

Tamko hilo la Serikali ya Marekani lilitolewa jana na Balozi wa taifa hilo kubwa hapa nchini, Alfonso Lenhardt, wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao kuzungumzia uzoefu alioupata wa kuishi hapa nchini kwa siku 100 za kwanza, tangu alipowasili nchini Novemba 10, mwaka jana.

Balozi Lenhardt ambaye alikuwa akijibu swali, alisema sera ya Marekani ya kuchochea ustawi wa demokrasia duniani na Tanzania hailengi katika kuvisaidia kifedha au kimikakati vyama vya siasa na wala haitekelezwi katika misingi ya kutaka matokeo fulani kupitia katika sanduku la kura.

"Hatusaidii vyama vya siasa katika uchaguzi, tangu nimefika nimekutana na viongozi au wawakilishi wa vyama vitatu vyenye nguvu vya CCM, CUF na CHADEMA, ambavyo nadhani ndivyo vikubwa hapa...ndiyo nimekisikia hiki chama cha CCJ kupitia katika vyombo vya habari, sijakutana na viongozi wake na hata hawajulikani ni kina nani. Jambo la msingi, hatusaidii chama chochote cha siasa, tupo hapa kuwasaidia wananchi wa Tanzania," alisema balozi huyo.

Alipoulizwa alikuwa ana maoni gani kuhusu kauli iliyopata kutolewa hivi karibuni na kwa nyakati tofauti na Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ya kuyataka mataifa ya nje kutoingilia masuala ya ndani ya Tanzania, balozi huyo kwanza alisema anaamini matamshi hayo hayakuilenga nchi yake.

Akifafanua alisema alikuwa akiunga mkono kauli hizo kutokana na yeye mwenyewe kuwa na imani kwamba, Watanzania wenyewe ndio walio na wajibu wa kuamua hatima ya masuala yanayohusu nchi yao na si mataifa ya nje kama Marekani.

Balozi Lenhardt alisifia hatua mbalimbali za kukabiliana na masuala yanayohusu rushwa na utawala bora hapa nchini na akasema ni vyema viongozi wanaojiuzulu uongozi kutokana na kukabiliwa na tuhuma za rushwa wakafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

"Tunaona hatua zikipigwa katika mapambano dhidi ya rushwa na kuimarisha misingi ya utawala bora. Kuna viongozi wamejiuzulu kutokana na mambo hayo, nadhani ni jambo jema baada ya kujiuzulu uchunguzi ukafuata na watuhumiwa wakafikishwa mbele ya vyombo vya sheria," alisisitiza balozi huyo na kuongeza kuwa hatua za namna hiyo zinaonyesha namna serikali inavyopambana na rushwa ipasavyo.

Alipoulizwa ni kwa nini anaona ni vyema kwa Tanzania viongozi waliojiuzulu kwa tuhuma za rushwa wakashitakiwa ilhali nchini Marekani miaka ya 1970 wakati rais wa nchi hiyo, Richard Nixon, alijiuzulu kwa rushwa na hakushitakiwa, Balozi Lenhardt alisema kutoshitakiwa kwa rais huyo kulitokana na msamaha aliopewa na rais aliyefuata baada yake, Gerald Ford.

Wakati Balozi wa Marekani akitoa kauli hiyo, uongozi wa muda wa CCJ nao kwa upande wake uliihakikishia Tanzania Daima kwamba chama hicho kilikuwa hakijawahi hata siku moja kuwasiliana na kupata msaada wa aina yoyote kutoka nje ya nchi, kwani kinaendeshwa kwa kutumia rasilimali za wanachama na wananchi.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa muda wa CCJ, Richard Kiyabo, alisema; "Hatujawahi kuomba fedha kutoka nchi yoyote, kwani uendeshaji wa chama chetu unatokana na vyanzo vyetu binafsi. Hatutarajii kufanya hivyo hata siku zijazo kutokana na sheria mpya ya fedha iliyopitishwa hivi karibuni."

Katika hatua nyingine, uongozi huo wa muda wa CCJ, umemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kuacha kutengeneza mazingira magumu ya kuwazuia kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Akizungumza na Tanzania Daima, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muhabi, alisema kauli za msajili huyo zinatengeneza mazingira ya kuwazorotesha katika juhudi za kupita mikoani kwa ajili ya kuwapata wanachama.

Alisema wanatarajia kuwasilisha majina ya wanachama 200 kila mkoa kwa mikoa 10 mwanzoni mwa Aprili mwaka huu, hivyo kauli za msajili huyo kwamba atafuata sheria ya miezi sita, atawanyima haki wananchi wengi wenye matumaini na chama hicho.

"Kwa kauli zake, Tendwa anatengeneza mazingira ya kutunyima usajili wa kudumu mapema ili tusishiriki kwenye uchaguzi, sasa hili si jambo jema…asitafute sababu ili baadaye apate kitu cha kusema. Mategemeo yetu ni kushiriki Uchaguzi Mkuu.

"Sisi hadi mwanzoni mwa mwezi ujao (yaani Aprili), tutakuwa tayari tumekamilisha idadi ya wanachama wanaotakiwa kwa mujibu wa sheria… hatujawahi kufanya kazi za chama kabla ya kupata usajili wa muda," alisisitiza Muhabi.

Aidha, katibu huyo aliitaja mikoa minane ya Tanzania Bara watakayoitembelea kuwa ni Mara, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani, ambapo kwa Zanzibar watafika Unguja na Pemba.

Alisema wakati wanatengeneza chama walifanya utafiti wa kutosha hivyo haitawawia vigumu kwao kuwapata wanachama 200 kwa mikoa watakayoitembelea huku akiahidi kuzunguka nchi nzima baada ya kupata usajili wa kudumu.

Akitolea mfano kwa Dar es Salaam, Muhabi alisema baada ya kupata usajili wa muda, wamejizolea wanachama rasmi wenye kadi za CCJ zaidi ya 4,000 na kubainisha kwamba hiyo ni dalili njema kwao.

Kuhusu uvumi kwamba wanatumia teknolojia ya mtandao kuwapata wanachama wanaotakiwa, katibu huyo alikanusha maneno hayo na kusisitiza kuwa wameshaanza kwenda mikoani kutafuta wanachama na ofisi za chama chao.

"Hatuna teknolojia hiyo, ingawa tunafikiria kuwa nayo ila kwa sasa bado… tukitafuta wanachama kwa njia hiyo itakuwa kazi ngumu kwa msajili kuhakiki majina ya wanachama na kujiridhisha kama kweli wanatoka kwenye mikoa tajwa," alisema katibu huyo akiwa na Mwenyekiti wake, Richard Kiyabo. Juzi, CCJ ilikabidhiwa cheti cha usajili wa muda kwenye ofisi za msajili wa vyama vya siasa huku msajili wake akionyesha wasiwasi wake kwa chama hicho kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kutokana na muda wa kutimiza matakwa ya sheria.

Tendwa, alisema ili chama kipate usajili wa muda kuna sheria ya miezi sita ili kutafuta wanachama 200 kila mkoa kwa mikoa 10 nchini, ambayo kwa mujibu wake anazingatia zaidi sheria zilizopo.
 
Ukiona hivyo CCM wameanza kuitafutia vijisababu kionekane kinavyunja sheria wameshamaliza mbinu zote walianza na udini kwa CUF wakachoka kinapeta tu wakaja na ukabila kwa Chadema wananchi wamewadharau sasa wamekuja na mbinu hii sijui kama itasaidia wanasema eti CCJ ilianza miaka miwili kabla sasa walitaka sijui mtu na mke wake waamuke asubuhi kwenda moja kwa moja kwa msajili kuomba usajili bila kukutana au kufanya utafiti kwa kuogopa wataonekana chama kimeanza mapema mawazo finyu kweli
 
Back
Top Bottom