Hatimaye CCJ chasajiliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye CCJ chasajiliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 24, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tanzania Daima

  HATIMAYE Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imeridhia kukipa usajili wa muda Chama Cha Jamii (CCJ), baada ya kukikwepa kwa zaidi ya miezi miwili.

  Habari za uhakika zilizoifikia Tanzania Daima zinasema ofisi ya msajili jana ilimwandikia mwenyekiti wa muda wa CCJ, Richard Kiyabo yenye kumbukumbu namba RPP/CCJ/136/09, ikijibu maombi ya usajili wa muda.

  Barua hiyo iliyoandikwa na Ibrahim Mkwawa kwa niaba ya msajili, ilisema itakikabidhi chama hicho cheti cha usajili wa muda Machi 2 mwaka huu saa tano asubuhi katika ofisi za msajili.

  Ilieleza kuwa msajili ameridhika na maombi ya usajili wa muda wa chama hicho baada ya kukidhi matakwa ya sheria namba tano ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

  "Hivyo basi, Msajili wa Vyama vya Siasa atakabidhi cheti cha usajili wa muda kwenu siku ya tarehe 2/03/2010 saa tano asubuhi kwenye ofisi ya msajili," ilieleza sehemu ya barua hiyo ambayo Tanzania Daima ilipata nakala yake.

  Licha ya kupatikana kwa barua hiyo, ofisi ya msajili imetaka kuongezewa nakala tatu za katiba ya chama hicho kabla ya kukabidhiwa rasmi cheti cha usajili wa muda mapema juma lijalo.

  Jana, gazeti hili liliandika kuhusu ucheleweshwaji wa usajili wa muda hali iliyodaiwa kukwamisha utekelezaji wa baadhi ya mambo kwa lengo la kujiimarisha kama chama ili kukabiliana vilivyo kwenye uchaguzi mkuu ujao.

  Hata hivyo, ofisi ya msajili iliahidi kukutana na CCJ leo ili kuwapa maelekezo ya lini hasa watapata usajili wa muda, lakini katika hali ya kushtukiza, viongozi wa chama hicho walipokea simu zilizowataka kufika ofisini kwa msajili jana mchana.

  "Tumepokea simu kutoka kwa msajili mwenyewe akisema kwa nini tumeamua kumshitaki kwa jamii, sasa ametuita… sijui anakwenda kuzungumza nini, tukishakutana nae mchana wa leo (jana) tutajua cha kufanya," kilieleza chanzo cha habari chenye kuaminika kutoka CCJ na kuongeza kwamba, ahadi ya kukutana na msajili ilikuwa leo.

  Awali, viongozi wa juu wa chama hicho walisema tayari chama chao kimetengeneza katiba, kanuni za chama, bendera, kadi na kwamba inao zaidi ya wanachama 3,000 kwa Dar es Salaam pekee, hivyo walikuwa wakisubiri kupata usajili kabla ya kukizindua rasmi.

  Sehemu ya Katiba ya CCJ inaeleza: "Kwa kuwa Tanzania inao utajiri wa kutosha wa rasilimali unaoweza kuleta maendeleo ya haraka ya nchi kiuchumi na kuleta mabadiliko makubwa ya maisha kwa kila mwananchi ikiwa ombwe la uongozi litashughulikiwa."

  Sehemu nyingine ya katiba hiyo inaeleza kwamba itahakikisha utajiri wa rasilimali zilizopo unatumika kwa maendeleo ya wananchi kwa kuondoa umaskini, ujinga, na maradhi huku aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, uonevu, rushwa au ufisadi vinatokomezwa nchini.

  Ujio wa CCJ umeleta mtikisiko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea urais Oktoba mwaka huu.

  Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wanadai kuanzishwa kwa CCJ ni mkakati wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo ina lengo la kupotosha umma kuhusu hatima ya CCM na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Vile vile, wanadai CCJ imeanzishwa ili kuupotosha umma unaoikosoa CCM, na kuumaliza nguvu upinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kimekuwa mwiba mkali kwa CCM katika miaka ya hivi karibuni.

  Baadhi ya vigogo wa CCM wanaohusishwa na CCJ ni Spika wa Bunge Samuel Sitta, makundi ya wanachama na viongozi waliojiweka mbele kupambana na ufisadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba na John Malecela. Lakini wote wamekanusha jambo hilo.

  Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, hatua ya vigogo hao kuikana CCJ ni mwanzo mbaya na fursa iliyopotea ya kukikuza na kukijenga chama hicho. Wapo baadhi ya vigogo waliojitambulisha na chama hicho, lakini hawataki kutajwa majina magazetini kwa sasa.

  UPDATE:

  March 02, 2010

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  CCJ yapata usajili rasmi
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hii ni kama hatua moja tunawasubiri hao vigogo wajitangaze hadharani
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  So who was a hoax, Tendwa or CCJ? He said openly that there is no such a thing as CCJ and here comes the birth of CCJ.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  hamna kitu, kujificha ndio nini sasa? ukishapika nawa kula!

  CCJ siyo ya yeyote ni walewale wana seek employment,

  hao wanaojiita vigogo wanataka tuje kuwachezea ngoma? wamekuwa wanawali?
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Uslama wa Taifa unaweka maslahi ya CCM mbele kuliko maslahi ya Taifa, tunatakiwa kujiuliza vizuri kama usalama wa taifa umekuwa secirty department ya CCM, au department ya kutoa seciruty kwa baadhi ya watu walioko CCM. I wonder kama CCJ inaanzishwa kama walivyoanzisha NCCR mageuzi, kuua upinzani na kuipa CCM easy ride.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  labda wakati wa kufikiria kuchukua kadi..
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,517
  Likes Received: 7,271
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa UWT hipo hapo kwa maslahi ya CCM, lakini kwa mtazamo wa wahusika wakuu wa hiki chama nadhani nao watakuwa Maaduhi wakubwa wa UWT kwa sababu wtakuja na sera na upinzani wa kweli katika hii nchi, ukiwa na watu kama SALIM, WARIOBA, BUTIKU, QARES, MAKWETA ambao kwa upande mmoja wana influence zao ndani na nje ya nchi, mfano salimu almost Africa nzima walijua ndio atakuja kuwa raisi wa Tanzania, lakini kwa sababu siasa za Tanzania zinafata sura akakosa
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It is a pity kuona watu wanakazania kutaka kujua majina ya vigogo wa CCJ badala ya kuangalia Katiba ya CCJ na Sera zake zina mwelekeo gani. Tanzania haitaendeshwa wala kukombolewa kwa majina ya vigogo bali nia thabiti ya kizalendo kuhakikisha nchi inarudisha heshima yake na kuleta maendeleo ya haraka kwa walio wengi. Tanzania imepoteza heshima yake ndani na nje ya nchi kutokana na kunuka ufisadi. Enzi hizo Wanigeria ndio waliokuwa wananuka kwa utapeli na sisi sasa tunasifika kunuka ufisadi! Sakata la rada peke yake limeweza kuchafua jina la Tanzania katika medani ya kimataifa ukiacha ufisadi wa ndani unaovuma kutokana na kesi zilizo mahakamani na ambazo bado zinapigwa danadana hazijafikishwa huko. Ufisadi umetanda kila kona ya nchi kwa kiwango cha kutisha. Fedha za Umma zinamung'unywa tu badala ya kuwasaidia wananchi kupata huduma za jamii na kuwaletea maendeleo wanayostahili.

  Je CCJ ina mikakati gani itakayoirudishia nchi hii heshima yake na kuwaangalia asilimia 80 ya Watanzania wasiokuwa na uhakika wa maisha yao ya kila siku? Hayo ndiyo ya msingi na si kujua majina ya vigogo. Kukazania majina ya vigogo ni ku-underrate uwezo wa kuongoza wa Watanzania wengine ambao si vigogo. After all 'vigogo' ndio walioifikisha nchi hapa ilipo kwa kukaa kimya muda wote huu mpaka nchi inafika hapa.
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Let them come wenyewe tutachambua pumba na mchele kama wako serious watajulikana tu kina Marando Lwamwai Tambwe Kabourou walifika wapi mbona walikuwa peupe mapema sasa Cheyo na Mrema hakuna haja ya kutuambia kuwa CCJ ni UWT wananchi watawatambua tu
   
 10. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 718
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 80
  Ndugu wana jamvi, demokrasia ya kweli na makini si mlolongo wa vyama.

  Mlolongo wa mavyama mengi, ni dalili ya uroho wa madaraka, ubinafsi uliokithiri ukiambatana na u parpet. Kwa kuweka maslahi ya taifa nyuma na kutanguliza mbele maslahi binafsi.

  Kamwe serikali ya CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuwa na mlolongo wa mavyama mengi. Bali CCM itahakikishiwa nafasi yake ya kudumu kulitawala taifa hili kwa kuwa na mlolongo wa mavyama.
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Siasa za Bongo bwana eti Tendwa alisema bila aibu CCJ is a Hoax hakuna kitu kama hicho na baadhi ya wanaJF waka support kwa nguvu kama hawaijui Tanzania tukawaambia CCM watabana sana lakini mwisho wataachia mambo taratibu lakini tutafika
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Hivi nyie CCJ ni kina nani?? kwa nini hamtaki kujitoa mapema tuwatambue ?
  Wasi wasi wasngu 2010 hamtaruhusiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro..
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 5,071
  Likes Received: 915
  Trophy Points: 280
  Big Up Boramaisha. Hawa vigogo ni sawa na OLD WINE IN A NEW BOTTLE. Nchi hii haitaendelea kwa kutumia akili za watu walewale ambao waliotufikisha hapa. Hawa akina Warioba, Salim, Butiku, Mateo Qares etc. ni walewale hawana jipya.

  CCJ itafanikiwa kama kizazi kipya cha wanachama watajiunga na kuendeleza ajenda yake.
   
 14. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama demokrasia ni kuwa na vyama vingi basi Tanzania tujivunie...mi wenyewe nna mpango wa kusajili cha kwangu nianze kulamba ruzuku...
   
 15. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanks Tata but, personally nawaheshimu sana hao vigogo uliotaja majina yao na naheshimu mchango wao mkubwa kwa taifa letu. Kwanza hao vigogo wote hakuna hata mmoja ambaye ananuka ufisadi. Kwa hiyo hatutakuwa tunawatendea haki kwa kubeza akili zao hata kama tunahitaji kizazi kipya kiendeshe nchi yetu. Lakini inabidi pia tujiulize hicho kizazi kipya kina msimamo gani? Isije ikawa ndio yale yale wana aspire kuwa viongozi ili waweze kula nchi badala ya kuwasaidia wananchi waliowaweka madarakani.
   
 16. F

  Felister JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh kweli nimeamini...Si mwenyekiti na katibu wake wanajulikana sasa hao wengine unaowataka wewe akina nani? Nami naomba wasipewe usajili wakati huu if I am to strategise for them. Maana wakipewa usajili na kungombea term hii kuleta significant change ni ngumu labda kwa favour ya Mungu. Ila come next election wakajichunga na mapupet basi hiki ndicho kitakua kimbilio la wengi maana mwendo mdundo acha hasira za wananchi ziwe nyingi kiasi cha kutosha...
   
 17. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  CCJ,Chadema,CUF,TLP UDP tutakuwa na utitiri usio na chocchote.
  Kwa nini CCJ wajifiche?

  Ruzuku inaua demokrasi,no body cares maisha ya wenzetu huko vijijini.
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  you...........can............say...............that.............again!!!!!!!!!!!!
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  aliyekuambia siasa ni employment nani?
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,415
  Likes Received: 2,056
  Trophy Points: 280
  waje tu ilimradi wawe na kadi ya chama kimoja cha siasa sio kuwa na kadi zaidi ia mija na mwishowe kuwa vibaraka wa vyama vingine. Nadhani wakiwa serious tunaweza kupata pa kuanzia!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...