Hatimaye CCJ chasajiliwa

Ni nani aliye na CVs za akina Mwenyekiti wa Muda, Richard Kiyabo, na Katibu Mkuu wake, Renatus Muabhi?

Au "backgrounds" zao?

 
Watangazaji wanawake wa TBC naweza kusema ni bogus. Jana ama juzi I just happened kusikiliza kipindi sijui ndio kinaitwa 'Mambo Bado' huyo mdada mtangazaji akawa ana-argue kuhusu vyandarua vya hati punguzo vinavyouzwa madukani kwa bei kubwa. Akadai kwamba wapo baadhi ya watu wanalalamikia bei ya vyandarua hivyo madukani bila kujua kwamba haviwahusu vinahusu wajawazito na watoto. She is forgetting that ni haki ya Mtanzania yoyote kutoa mawazo yake pale anapoona jambo haliendi sawa na hili la vyandarua likiwemo regardless mtu ana mimba au ana mtoto mchanga.

Haingii akilini kuambiwa kwamba kuna vyandarua vya hati-punguzo kwa akina mama wajawazito na watoto lakini vyandarua hivyo haviwafikii walengwa tangu wanapoanza kwenda clinic mpaka wanajifungua. Badala yake unavikuta vinauzwa holela madukani bila maelezo wala maelekezo yoyote vikiwa na nembo ya FREE NET by USAID! That bogus mtangazaji said something like 'Wazee mnaolalamikia vyandarua hivyo yanawahusu nini wakati nyie si wajawazito!?'

Bora Maisha,huyo dada kweli hamnazo,anajua vipi kwamba wazee hao hawawanunulii watoto ama wake zao ambao ni wajawazito?Ama anadhani ni watoto wote na wajawazito wote wenye kuweza kujinunulia kila kitu?
Ni wazi watoto hawafanyi kazi,na kwahivyo issue hii inahusu familia kwa ujumla,sasa huyu dada hajisumbui hata kufikiri?
 
pix.gif
1267686078_alfonso_lenhardt.jpg

• Balozi nchini akana kuisaidia kifedha, kimkakati
KUANZISHWA kwa Chama Cha Jamii (CCJ) kumeendelea kuchochea hali ya mikanganyiko inayotokana na kuwapo kwa taarifa mbalimbali zinazokinzana kuhusu ustawi na mfumo wa uendashaji wake; Tanzania Daima imebaini..
Siku tatu baada ya chama hicho kukabidhiwa cheti cha usajili wa muda kumeibuka taarifa zinazokihusisha chama hicho na misaada kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa mtandao wa kompyuta katika kusaka wanachama 200 kutoka mikoa minane ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar.

Hata hivyo saa chache tu baada ya taarifa hizo kuifikia Tanzania Daima, Marekani, moja ya nchi ambazo zimekuwa zikitajwa chinichini kukisaidia chama hicho, ilitoa tamko la kukanusha kufanya hivyo kwa CCJ na kwa chama kingine chochote cha siasa hapa nchini.

Tamko hilo la Serikali ya Marekani lilitolewa jana na Balozi wa taifa hilo kubwa hapa nchini, Alfonso Lenhardt, wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao kuzungumzia uzoefu alioupata wa kuishi hapa nchini kwa siku 100 za kwanza, tangu alipowasili nchini Novemba 10, mwaka jana.

Balozi Lenhardt ambaye alikuwa akijibu swali, alisema sera ya Marekani ya kuchochea ustawi wa demokrasia duniani na Tanzania hailengi katika kuvisaidia kifedha au kimikakati vyama vya siasa na wala haitekelezwi katika misingi ya kutaka matokeo fulani kupitia katika sanduku la kura.

“Hatusaidii vyama vya siasa katika uchaguzi, tangu nimefika nimekutana na viongozi au wawakilishi wa vyama vitatu vyenye nguvu vya CCM, CUF na CHADEMA, ambavyo nadhani ndivyo vikubwa hapa...ndiyo nimekisikia hiki chama cha CCJ kupitia katika vyombo vya habari, sijakutana na viongozi wake na hata hawajulikani ni kina nani. Jambo la msingi, hatusaidii chama chochote cha siasa, tupo hapa kuwasaidia wananchi wa Tanzania,” alisema balozi huyo.

Alipoulizwa alikuwa ana maoni gani kuhusu kauli iliyopata kutolewa hivi karibuni na kwa nyakati tofauti na Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ya kuyataka mataifa ya nje kutoingilia masuala ya ndani ya Tanzania, balozi huyo kwanza alisema anaamini matamshi hayo hayakuilenga nchi yake.

Akifafanua alisema alikuwa akiunga mkono kauli hizo kutokana na yeye mwenyewe kuwa na imani kwamba, Watanzania wenyewe ndio walio na wajibu wa kuamua hatima ya masuala yanayohusu nchi yao na si mataifa ya nje kama Marekani.

Balozi Lenhardt alisifia hatua mbalimbali za kukabiliana na masuala yanayohusu rushwa na utawala bora hapa nchini na akasema ni vyema viongozi wanaojiuzulu uongozi kutokana na kukabiliwa na tuhuma za rushwa wakafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

“Tunaona hatua zikipigwa katika mapambano dhidi ya rushwa na kuimarisha misingi ya utawala bora. Kuna viongozi wamejiuzulu kutokana na mambo hayo, nadhani ni jambo jema baada ya kujiuzulu uchunguzi ukafuata na watuhumiwa wakafikishwa mbele ya vyombo vya sheria,” alisisitiza balozi huyo na kuongeza kuwa hatua za namna hiyo zinaonyesha namna serikali inavyopambana na rushwa ipasavyo.

Alipoulizwa ni kwa nini anaona ni vyema kwa Tanzania viongozi waliojiuzulu kwa tuhuma za rushwa wakashitakiwa ilhali nchini Marekani miaka ya 1970 wakati rais wa nchi hiyo, Richard Nixon, alijiuzulu kwa rushwa na hakushitakiwa, Balozi Lenhardt alisema kutoshitakiwa kwa rais huyo kulitokana na msamaha aliopewa na rais aliyefuata baada yake, Gerald Ford.

Wakati Balozi wa Marekani akitoa kauli hiyo, uongozi wa muda wa CCJ nao kwa upande wake uliihakikishia Tanzania Daima kwamba chama hicho kilikuwa hakijawahi hata siku moja kuwasiliana na kupata msaada wa aina yoyote kutoka nje ya nchi, kwani kinaendeshwa kwa kutumia rasilimali za wanachama na wananchi.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa muda wa CCJ, Richard Kiyabo, alisema; “Hatujawahi kuomba fedha kutoka nchi yoyote, kwani uendeshaji wa chama chetu unatokana na vyanzo vyetu binafsi. Hatutarajii kufanya hivyo hata siku zijazo kutokana na sheria mpya ya fedha iliyopitishwa hivi karibuni.”

Katika hatua nyingine, uongozi huo wa muda wa CCJ, umemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kuacha kutengeneza mazingira magumu ya kuwazuia kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Akizungumza na Tanzania Daima, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muhabi, alisema kauli za msajili huyo zinatengeneza mazingira ya kuwazorotesha katika juhudi za kupita mikoani kwa ajili ya kuwapata wanachama.

Alisema wanatarajia kuwasilisha majina ya wanachama 200 kila mkoa kwa mikoa 10 mwanzoni mwa Aprili mwaka huu, hivyo kauli za msajili huyo kwamba atafuata sheria ya miezi sita, atawanyima haki wananchi wengi wenye matumaini na chama hicho.

“Kwa kauli zake, Tendwa anatengeneza mazingira ya kutunyima usajili wa kudumu mapema ili tusishiriki kwenye uchaguzi, sasa hili si jambo jema…asitafute sababu ili baadaye apate kitu cha kusema. Mategemeo yetu ni kushiriki Uchaguzi Mkuu.

“Sisi hadi mwanzoni mwa mwezi ujao (yaani Aprili), tutakuwa tayari tumekamilisha idadi ya wanachama wanaotakiwa kwa mujibu wa sheria… hatujawahi kufanya kazi za chama kabla ya kupata usajili wa muda,” alisisitiza Muhabi.

Aidha, katibu huyo aliitaja mikoa minane ya Tanzania Bara watakayoitembelea kuwa ni Mara, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani, ambapo kwa Zanzibar watafika Unguja na Pemba.

Alisema wakati wanatengeneza chama walifanya utafiti wa kutosha hivyo haitawawia vigumu kwao kuwapata wanachama 200 kwa mikoa watakayoitembelea huku akiahidi kuzunguka nchi nzima baada ya kupata usajili wa kudumu.

Akitolea mfano kwa Dar es Salaam, Muhabi alisema baada ya kupata usajili wa muda, wamejizolea wanachama rasmi wenye kadi za CCJ zaidi ya 4,000 na kubainisha kwamba hiyo ni dalili njema kwao.

Kuhusu uvumi kwamba wanatumia teknolojia ya mtandao kuwapata wanachama wanaotakiwa, katibu huyo alikanusha maneno hayo na kusisitiza kuwa wameshaanza kwenda mikoani kutafuta wanachama na ofisi za chama chao.

“Hatuna teknolojia hiyo, ingawa tunafikiria kuwa nayo ila kwa sasa bado… tukitafuta wanachama kwa njia hiyo itakuwa kazi ngumu kwa msajili kuhakiki majina ya wanachama na kujiridhisha kama kweli wanatoka kwenye mikoa tajwa,” alisema katibu huyo akiwa na Mwenyekiti wake, Richard Kiyabo.

Juzi, CCJ ilikabidhiwa cheti cha usajili wa muda kwenye ofisi za msajili wa vyama vya siasa huku msajili wake akionyesha wasiwasi wake kwa chama hicho kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kutokana na muda wa kutimiza matakwa ya sheria.

Tendwa, alisema ili chama kipate usajili wa muda kuna sheria ya miezi sita ili kutafuta wanachama 200 kila mkoa kwa mikoa 10 nchini, ambayo kwa mujibu wake anazingatia zaidi sheria zilizopo.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
 
Mara mnasema CCJ ina uhusiano na usalama wa taifa, mara mnasema vigogo 10 ndio wako behind CCJ na sasa mnasema CCJ inauhusiano na mataifa nje. This is way i think is undergoing CCJ is either a distraction of attention from the issues surrounding CCM Richmond, Twin towers etc or just a way of killing opposition in the next election. Sijaenda bado na mkumbo wenu. Na magazeti kwakuwa yanataka kuuzwa wanaandika kwa ushabiki
 
Mara mnasema CCJ ina uhusiano na usalama wa taifa, mara mnasema vigogo 10 ndio wako behind CCJ na sasa mnasema CCJ inauhusiano na mataifa nje. This is way i think is undergoing CCJ is either a distraction of attention from the issues surrounding CCM Richmond, Twin towers etc or just a way of killing opposition in the next election. Sijaenda bado na mkumbo wenu. Na magazeti kwakuwa yanataka kuuzwa wanaandika kwa ushabiki

supported! wanataka eti washiriki uchaguzi mwaka huu! huyo CCM wa kuondoka ni nani? yaani iki chama kina uwezekano kikamjulisha mgombea wa urais siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu, wana style yao ya kuingia ikulu na kukamata viti vya ubunge , hamna kampeni wala nini!

hata mimi sijakamatwa kwenye huo mkumbo!
 
Mara mnasema CCJ ina uhusiano na usalama wa taifa, mara mnasema vigogo 10 ndio wako behind CCJ na sasa mnasema CCJ inauhusiano na mataifa nje. This is way i think is undergoing CCJ is either a distraction of attention from the issues surrounding CCM Richmond, Twin towers etc or just a way of killing opposition in the next election. Sijaenda bado na mkumbo wenu. Na magazeti kwakuwa yanataka kuuzwa wanaandika kwa ushabiki


This story is not worth the paper it's printed on; Chama gani cha Siasa Tanzania ambacho hakina uhusiano na Mataifa ya nje???

 
Ndio maana yebo yebo nasema siendi na mkumbo huo kwani too many facts to comprehend them.
 
It is still too early to tell whatCCJ is all about. It may well be our savoir, or may as well be our poison, there are many thing that we still do not know about this political animal. Tendwa satrted calling it a Hoax before CCJ made him look an idiot by putting it in the list of new parties.

Some of us are trying to rudicule this new animal, we may one day end up like Tendwa. So let us give this animal some time, and see how he walks before making any conclussion.
 
  • *WAHOJI ALIKUWA WAPI KUWAZUIA KAMA WALIKUWEPO MIAKA MIWILI NYUMA
BAADA ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kutangaza kuanza uchunguzi wa kuona kama Chama Cha Jamii (CCJ) kilifanya siasa miaka miwili kabla ya usajili; viongozi wa chama hicho wamejibu mapigo kwa kuhoji kwamba; ofisi ya msajili na vyombo vya usalama vilikuwa wapi, hadi chenyewe kifanye siasa kinyume cha sheria.

Mapigo hayo ya CCJ yanatokana na kauli ya msajili huyo aliyoitoa juzi kabla ya kuwakabidhi cheti cha usaji wa muda kwamba; ofisi yake imepata taarifa kuwa CCJ ilianza kufanya shughuli za kisiasa miaka miwili iliyopita na kusisitiza kuwa ikithibitika atakifutilia mbali.


Kauli hiyo ya kitisho inayoiweka CCJ njia panda, jana ilijibiwa vikali na Katibu Mkuu wake, Renatus Muabhi aliyehoji kwamba, kama ofisi hiyo ya msajili iko makini ilikuwa wapi kuigilia kati wakati huo kama kweli chama hicho kilianza kufanya shughuli za kisiasa miaka miwili iliyopita?


Muabhi licha ya kumshangaa Tendwa, alisema kama ikithibitika ni kweli basi msajili huyo na wasaidizi wake na hata baadhi ya vyombo vya usalama vitapaswa kuwajibika.


Juzi Msajili akizungumza na kituo cha ITV alirusha kombora kwa CCJ siku moja kabla ya kukipatia usajili na kuweka bayana kwamba, ofisi yake imepata taarifa hizo za chama kujipanga kisiasa kabla ya usajili na kuonya atakifuta.


Akijibu kombora Muabhi alisema: "Msajili na vyombo vya usalama vilikuwa wapi? Mbona msajili alijua taarifa zetu kabla ya kupeleka taarifa za maombi ya usajili ofisini kwake?" alihoji Muabhi na kuongeza:


"Hiyo siasa tulikuwa tukiifanya katika nchi gani, hivi kweli Tanzania hii unaweza kufanya siasa kwa miaka miwili kinyume cha sheria bila kujulikana?"


Kwa msisitizo, Muabhi alisema mpango huo ni njama za kukihujumu na propaganda chafu zisizokuwa na mantiki dhidi ya CCJ baada ya kuona mwelekeo wake kisiasa unaelekea kuungwa mkono na Watanzania wengi.


Muabhi alisema chama hicho lazima kitakutana na mawimbi mazito sawa na ya bahari, lakini hakitarudi nyuma, kitajiimarisha na kushikamana na Watanzania wazalendo.


Alisema tayari kimepanga vema ratiba yake ya kusaka idadi ya wanachama 2,000 nchini kote ambayo inaonyesha itakuwa katika mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Pemba, Mara, Mbeya, Shinyanga na Iringa.


Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba, kadi zao kwa wanachama zitauzwa kwa bei ya chini ambayo haitazidi Sh 400 na baadhi wasiojiweza watapatiwa bure baada ya utaratibu kukamilika.


CCJ ujio wake unaangaliwa na wadadisi wa mambo ya kisiasa kama tishio kwa CCM na Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea urais hapo Oktoba.


Tayari Spika wa Bunge Samuel Sitta, aliwahi kusema kwamba, haoni tatizo la kusajiliwa CCJ huku pia akisema hawezi kuzuia watu kumuhusisha na chama hicho kama mgombea hapo Oktoba.


CCJ imekuwa ikitikisa nchi tangu taarifa zake kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, kwani kuna majina makubwa yanatajwa kuwemo akiwemo Spika Sitta, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, John Malecela, lakini wote wamekanusha.


Hata hivyo, mwasisi wa CCM Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema bila CCM madhubuti nchi itayumba na kwamba, upinzani wa kweli utatoka ndani ya chama hichi, onyo ambalo wadadisi wa mambo ya siasa wanaona kuwa linakaribia.
 
Shida ya Ofisi ya Msajili ni kwamba inafanya kazi kwa shinikizo na maslahi ya Waliowaweka pale!...Ukimtazama Tendwa na kumsikiliza anavyoiongelea CCJ utagundua tu kuwa ana woga fulani, na kuna sumu amelishwa juu ya chama hiki.

Vilisajiliwa vyama viwili siku moja, lakini CCJ isinywe maji bana, jicho liko hapo!

Sasa kama kilinza miaka mi2 iliyopita, shida iko wapi?..Kwani chama kinamea kama uyoga siku moja, si ni lazima harakati zianze mbali?..Kama ameshakisajili tayari, kwanini kurudi nyuma na kuangalia kulikuwaje!

Uwoga mwingine tunaogopa hadi vivuli!
 
It is still too early to tell whatCCJ is all about. It may well be our savoir, or may as well be our poison, there are many thing that we still do not know about this political animal. Tendwa satrted calling it a Hoax before CCJ made him look an idiot by putting it in the list of new parties.

Some of us are trying to rudicule this new animal, we may one day end up like Tendwa. So let us give this animal some time, and see how he walks before making any conclussion.

Well said mkuu, hapa tuendelee kuchunguza ninini hasa, kwani hao wachumia tumbo ni wajanja sana wanazombinu nyingi mno za kutuvuruga watanzania hasa ukikaribia uchaguzi!
Na wala tusidharau kwamba kweli unabii huenda unaelekea kutimia.
 
Hivi ni chama gani kinaanzishwa na wanasiasa ambao sio wanasiasa??? Nani anajua historia ya hawa viongozi wa CCJ katika harakati zozote ziwe za kisiasa, kijamii au hata katika kutetea haki za group lolote katika jamii?? Kama hawajawahi kushiriki katika harakati zozote bas hawawezi kuwa wanasiasa nkwani watakua hawana wanachopigania. period.
 
I buy your idea nimejifunza mengi tangu NCCR ya 1994 kwa nini watanzania tunakuwa wepesi kukubali jambo! jibu linakuja wengi wamechoshwa na utawala uliopo watanzania ni kama tupo jangwani tunapoona mtu yeyote tunadhani ni masihi inawezekana kweli akawa masihi lakini inawezekana pia likawa dudu mtu lililotumwa kuwaangamiza kumbuka wakati wa NCCR ya Mrema mambo yalikuwa hivi hivi watu kwa mamia tulikimbilia kadi tukidhani mkombozi katelemshwa lakini tusikate tamaa tuchukue kadi ila tuwapime kabla ya kuwapa kura zetu

I can't agree more. Kuna 'ombwe' katika sera na mikakati ya vyama vya siasa hususan Chama Tawala CCM kiasi cha wananchi kuhangaika na kutamani kupata 'Mesiah' atakayewatoa kutoka Misri wanakoteseka kwa kukosa hata mlo mmoja kwa siku. That is what is all about in my opinion.
 
Hivi ni chama gani kinaanzishwa na wanasiasa ambao sio wanasiasa??? Nani anajua historia ya hawa viongozi wa CCJ katika harakati zozote ziwe za kisiasa, kijamii au hata katika kutetea haki za group lolote katika jamii?? Kama hawajawahi kushiriki katika harakati zozote bas hawawezi kuwa wanasiasa nkwani watakua hawana wanachopigania. period.

Well said muungwana. Mtu ukisimama kusema jambo lazima watu wahoji wewe ni nani? Sasa viongozi wa CCJ wengine ndio kwanza tunawajua hatujui wametokea wapi wamefanya nini. Ndio maana nasema nakaa mbali nacho haiwezekani mtu akaibuka tu tukamuona ni mtetezi wa wanyonge unaweza kuta vilevile muuwaji wa haki za wanyonge.
 
Hivi ni chama gani kinaanzishwa na wanasiasa ambao sio wanasiasa??? Nani anajua historia ya hawa viongozi wa CCJ katika harakati zozote ziwe za kisiasa, kijamii au hata katika kutetea haki za group lolote katika jamii?? Kama hawajawahi kushiriki katika harakati zozote bas hawawezi kuwa wanasiasa nkwani watakua hawana wanachopigania. period.

Naiogopa JF. Siku hizi nasita hata kuingia humu - jamvi limevamiwa na limbukeni kibao ! Eti tuendelee na watu walewale, chama kile kile, mawazo yale yale, upuuzi ule ule - duh, I hate it. Halafu twadai tunataka mabadiliko - yatapatikana vipi na kwa njia gani kama hatuko tayari kupokea mawazo mapya, eti kila siku tunajifunika ujinga wetu kwa kupiga kambi kwenye hema ile ile ya "afadhali zimwi likujualo !"
Eti CCM ikiteua hata chizi poa tu, tunamkabidhi madaraka bila kuuliza kafanya nini hapo nyuma. Lakini akitokea Mag3, ooh mara huyu naye katokea wapi. Jamani wa Tz, huu ujuha utatutoka lini ? Nakumbuka Wamarekani wengi tu ambao walimsema Obama hivi hivi, huyu naye katokea wapi, lakini mjaluo wa watu hivi sasa kakamata dola la taifa kubwa pamoja na wabaya wake kumpiga vita kila siku. Kwa kweli naanza kuichukia JF.
 
Nakumbuka kipindi fulani Mwalimu Nyerere katika hotuba zake alitoa hotuba kuhusu Chama Cha Mapinduzi kuwa karibu na wananchi.

Alisema kama Chama Cha Mapinduzi kitakuwa mbali na wananchi na kusahau maslahi yao, kuna siku wananchi wataanza kuuliza na 'sisi je'? Sasa chama kingine kimeanzishwa kinaitwa CCJ.

Je hiki kitakuwa karibu na wananchi?
 
Back
Top Bottom