Hatimae Pedeshee Ndama akiri kutakatisha fedha

Unapofungua Bureau de Change umefanya udanganyifu gani?
Ni kwamba biashara yako ya ngada itaendelea ila mapato yake utajifanya mapato ya bureau de change ambayo inawezekana isifanye vyema zile returns zake lakini wewe unaregister return safi tu na unalipia kodi ilhali 80%ya hayo "mapato ya bureau de change" yametokana na ngada! Capisce?
 
Naongezea hapo hapo ,sasa urakatishaji wenyewe ni kuwa ukipata pesa kwenye ngada zako unajifanya hayo mapato ni ya bureau de change unalipa kodi zote na unapata jeuri ya kuziweka benk kwa amani tu!
Exactly
 
Mi naona hii case ni ya kugushi vibali,
labda kama dhahabu aliiba au aliipata kwa utapeli ama kainunua kwa pesa za madawa ya kulevya.

Lakini kama dhahabu kainunua kwa pesa halali akataka kuisafirisha akagushi vibali labda ili kuepuka kodi,
sijana laundry hapa au labda money laundry ina maana pana kuliko nayoijua
Nenda kaangalie file la kesi yake upate facts za kesi yake sidhani km humu kuna file lake.
 
Biashara yoyote imepaswa kufunguliwa/kuanzishwa kwa mtaji utokanao na mapato halali na sii vinginevyo.
Unaweza kukopa bank au kwa mtu, na mkopeshaji hela anayokukopesha iwe halali.

Usijikute kwenye nafasi ukiulizwa "mtaji wa hii biashara umeutoa wapi" unataja vyanzo ambavyo havina uhalisia wowote. Kama yule jamaa wa takukuru anayeshindwa ku justify ukwasi wake.


Anhaa. Tatizo kumbe kuwekeza kwenye mradi tofauti kutumia pesa chafu.

Ukiiweka benki pesa ya madawa kwa hiyo inakuwa ni poa?
 
Mkuu safari kaingia chaka baya anaweza kupotelea hukohuko chakani kwa mvua kadhaa akirudi uraiani anakutana na flyover kibao kama Joberg kwa Madiba.
Ile kavikwa miaka 35 yuko ukonga anakula ugali wa bure
 
Lakini kama dhahabu kainunua kwa pesa halali akataka kuisafirisha akagushi vibali labda ili kuepuka kodi,
sijana laundry hapa au labda money laundry ina maana pana kuliko nayoijua


Ndio hapo sasa.

Hatujaambiwa katumia pesa chafu kufungua Chuo Cha Upadri wala Bureau De Change.

Na wala hawajasema ana pesa.

Na wala hawajasema dhahabu kaiba. For all we know dhahabu ya kwake.

Kosa kataka kuisafirisha Ausralia kwa nyaraka za kugushi kwa sababu kampuni haina vibali vya kusafirisha dhahabu.

Uwekezaji gani kafanya kwa pesa chafu?
 
Mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein (Pichani katikati) maarufu kama Ndama mtoto ya Ng'ombe amekiri mahakamani kosa la kutakatisha zaidi ya billioni 1.2.

Ndama anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 jijini Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboxi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Chanzo: Nipashe
Huyo ni mmoja kati wengi.Hata huu utitiri wa vibenki na Bureau de Change ni mkakati wa wauza unga na mafisadi kutakatisha fedha.Serikali izitupie macho.
 
Nikiiangalia tena ile Live Show ya Fally Ipupa ya Dar es Salaam na kumwona Pedeshee Ndama Mtoto wa Ng'ombe jinsi alivyokuwa anamwagia Pesa tena ' Midola ' mitupu Fally Ipupa na wale Dancers wake wote pale ' Stejini ' halafu leo namwona akiwa ' Lupango ' nasema kuwa ama kweli dunia haina dhamana na ' Sifa ' ni mbaya mno na hakuna maisha mazuri kama kuishi zako tu simple life kama GENTAMYCINE kwani utakuwa na amani sana na furaha siku zote.
Haikuwa midola mkuu Genta, ilikuwa ni misimbazi hii ya Tz.
 
Anhaa. Tatizo kumbe kuwekeza kwa pesa chafu.

Ukiiweka benki pesa ya madawa kwa hiyo inakuwa ni poa?
Uhalali wa jinsi ulivyoipata ndio utakupa credibility ya kubank.

Rejea maswali ya kwenye form unazojaza wakati wa kufungua bank account.
 
Uhalali wa jinsi ulivyoipata ndio utakupa credibility ya kubank.

Rejea maswali ya kwenye form unazojaza wakati wa kufungua bank account.


Siwajahi kujaza fomu ya kufungua akaunti benki ambayo inauliza pesa hii umeipata pataje. Benki gani hiyo?

Kwa hiyo definition ya kutakatisha fedha inazidi ku evolve. Kutunza benki hela chafu nayo ni kosa.
 


Kwa Wajanja wa Mjini 100 Million ndani ya Miezi Sita wanaweza wakazipata, sasa Ukake Jela Miaka yote hiyo ukitoka unakuwa Mgeni wa Jiji na Pengine tayari 'Mke wa Watu'!
Nduguyangu sio kipindi hiki cha mheshimiwa aliekwenda kuchukua form mwenyewe.
Kesi ya money laundering (kutakatisha pesa) ukitiwa hatiani ni kifungo jela miaka 4 au 7 sasa huyu kama kweli amekiri atakuwa ametumia technique koz angeweza kukaa rumande kwa mrefu zaidi ya miaka tajwa kama yanayomkuta wakili msomi Mwala kule Arusha yupo rumande mwaka wa saba mfululizo mpaka sasa kwa kosa hilohilo.
 
Naombeni mnisaidie maana ya hili neno "kutakatisha fedha"
" Money laundry"
Unapata pesa kwa njia isiyo halali kisha unaingiza benki, kisha unai-withdraw

Au Unapata pesa kwa njia isiyo halali, kisha unawekeza kwa kununua assets fulani, kisha unauza assets hizo

Simply, pesa chafu kununua kitu halali then kukiuza na kupata pesa safi!
 
Back
Top Bottom