Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nimeona hivi kuhusiana na hali inayofanana na hii aliyo nayo Mh. Chenge.
Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Chenge amekutwa na hatia na amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini 700,000Sh.
Sasa hatima ya Chenge inakuwaje baada ya hukumu hiyo?
Naomba wataalamu wa Sheria na katiba mtufafanulie vizuri.
ukisoma vema kifungu ulichonukuu kinasema mtu hatakuwa na sifa ya kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa mbunge.KIko wazi hakizungumzii mtu ambe ni mbunge tayari hivo kinawahusu wanaotaka kugombea au kuteuliwa kuwa wabunge. Kwa kifungu hiki Chenge tayari ni mbunge hivo hakiwezi kumbana labda kama kuna kifungu kinachosema mtu akishakuwa mbunge na akipataikana na hatia.Spika hawezi kutangaza jimbo lake wazi au vinginevyo.La pili Traffic offence ni tofauti na makosa mengineyo ndo maana hata kama ukigonga mtu akafa sio murder labda kuwe na vielelezo va kuonyesha umekusudia kuuwa.Kwa Chenge imeoneka ni kosa ndio aambalo imeanishwa ktk mojawapo ya Traffic offence na kapatikana na hatia ktk traffic offence na sio criminal offence ambayo iko ndani ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(criminal Procedure Act).Chenge bado ataendelea kutamba na vijisent vyake bungeni kama kawa. Ndo hivo nijuavo